Deejay nasmile
JF-Expert Member
- Nov 8, 2011
- 5,759
- 5,289
Wakuu naomba kuuliza hili swali?
Mtoto wa nje ya ndoa anaweza kurithi mali ya mama yake aliyefariki akiwa ndoani na baba mwingine? Ikiwa baba ndio aliwakuta mtoto na mama wanajitegemea
Iko hivi wakuu
Ikiwa mama anaishi na mtoto wake baada ya baba mtoto kufariki, wakawa na maisha yao ya kawaida tu.
Baadae mama anaolewa (funga ndoa) na baba mwingine..maisha yanaendelea,familia inakua na mali wanachuma vizuri.
Ikatokea mama kafariki gafla bila kuacha wosia ..je yule mtoto wa kwanza anaweza kurithi sehem ya mali za mama yake zilizochumwa pamoja na baba wa pili?Sheria hapo inasemaje?

Kwa kifupi hiyo sheria haipo kwa hapa Tz. Kwa mujibu wa sheria ya mtoto ya Tz iliyofanyiwa mapitio mwaka 2019, kifungu cha 10 cha sheria hiyo chenye "marginal note" isemayo "right to parental property" kinasema...
"A person shall not deprive a child of reasonable enjoyment out of the estate of a parent."
Yaani kwa kiswahili ni kusema kuwa
"Mtu hatamzuia mtoto yeyote kufurahia(kunufaika) mali ya mzazi wake"
Hilo neno "mtoto" tafsiri yake kwenye sheria hiyo halijabagua mtoto wa ndani au nje ya ndoa. So hao watoto wana haki ya kurithi mali ya mama yao.