mtoto wa nje anaweza kuzuia ndoa isifungwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mtoto wa nje anaweza kuzuia ndoa isifungwe

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Joyceline, Mar 23, 2010.

 1. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kaka yangu anaoa tarehe 24 April, bado wiki 1 ndoa ianze kutangazwa, wiki 1 moja iliyopita kapigiwa simu na binti 1 akajitambulisha kwake wanajuana waliwahi kuwa na uhusiano mwaka 2004 wakaachana alimfumania msichana, kumbe wakati wanaachana msichana alikuwa na mimba hajijui wakapoteana msichana amezaa sasa hv mtoto ana miaka 6, kamtafuta kaka yangu kwa marafiki hadi kampata. wakaenda kupima DNA kweli mtot ni wa kaka na amemkubali kulipa gharama na matunzo yote na pia atampeleka shule boarding atakuwa anamuhudumia. Ila msichana hatakia anasema yeye anataka kuolewa waleee mtoto wao, mwanaume hataki kumuoa anamwambia sikupendi, masichana ametishia kwenda kupinga ndoa kanisan, la sivyoa aolewe yeye. na msichana anayeolewa alivyosiskia amekasirika amemwambia mwanume nakuacha mlee mtoto wenu, kaka yangu amechanganyikiwa ni mwanume lakini kwa mara ya kwanza nimemuona akilia kama mtoto,kwanza ameachwa ndoa inakaribia, pili hamtaki huyo aliyezaa naye. kama huyo mchumba wake atamrudia huyo mama mtoto akienda kupinga ndoa itavunjika ua kuna taratibu zitafuatwa, maana kamuambia mama mtoto kwamba nikikuoa nitakutesa sana mimi sikupendi kuzaa siyo kigezo, mimi nimekosa cha kumshauri maana ni mwanamke na wote nawaonea huruma.
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Akapinge ndoa kwa sababu gani tena ? kwani aliahidiwa ndoa au anacheti cha ndoa na huyo kakaako mmh
  Huyo aliyezaa naye amweleze tu ukweli kwamba hana mpango wa kumuoa ila atamtunza mtoto .huyu mwingine na yeye inabidi awe mpole yeye ndo amependwa na ameahidiwa ndoa hana haja ya kupanic
  Haya ni maisha tu
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Ni kanisa gani hilo litamsikiza huyo hayawani? Yaani kuzaa ndo iwe nongwa!
  Huyo kaka'ko aendelee na mipango yake ya ndoa na huyo ampendae, wala haina kwere..asimsikize kabisa huyo kizabizabina wala asimpe fursa zaidi ya kumlea mtoto.
   
 4. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hana sababu yoyote ya kupinga ndoa, na hata huko kanisani hataeleweka maana kama nimeelewa vizuri kaka yako hajawahi kuishi nae wala kumuoa in any way, they just had an affair ambayo ndani yake alipatikana mtoto, ambaye amemficha hadi six years ndo anaibuka. kimsingi hamna kesi, yeye kaka yako apige moyo konde ambembeleze mwali wake aweke hayo mambo wazi kwa wazazi wote na hata kanisani solution ipatikane aoe.
   
 5. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  kama ni mkatoliki only cheti cha ndoa ndo kinapingamizi otherwise ni ishara tosha kwa bibi harusi wetu mtarajiwa kwamba kaka yetu anatema cheche
   
 6. bht

  bht JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  2004 mpka leo ndo anaibuka na kudai mtoto ni wa kakaako.....wat if its not even true (DNA itahusu)

  hakuna ushahidi wowote wa hata waliahidiana kuoana basi walau jamaa adaiwe fidia...
  hapana hamna pingamizi la ndoa, kaako aendelee na mpango, kazi kwake kuhakikishia mchumba wake vinginevyo ili waendelee na mpango wa kufunga ndoa....
   
 7. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  hajawahi kuishi naye ni girl friend wa chuo waliachana tangu 2004, mwanamke ana mdomo balaa, anaongea wote tunajiona wadogo, anasema mtoto wake kakosa mapenzi ya baba ndo anatakiwa ayapate,, anamwambia mwenzake mimi nimezaa wewe hujazaa kaa pembeni watu walee mtot wao
   
 8. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  DNA wamepima hospital tatu tofauti na majibu yanafanana, mtot ni wake maana wamefanana sana, ila binti anataka kuolewa, na huyu mwingine ameshikilia msimamo hataki, wivu na hasira vinamsumbua
   
 9. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  siyo katoliki ni makanisa ya kiroho, ila anadai siku ya ndoa ataibuka kanisania siku hiyohiyo na mtoto mbele ya watu wote apinge si atatuharibi shughulu
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hana ubavu wa kuweka pingamizi kanisani kwani walisha funga ndoa pamoja? Si alikuwa hawala tu kaka ako alikuwa anamega tu kama ana ushahidi tosha kuwa walikuwa mke na mme kwa vielelezo thabiti kama walisha funga ndoa sasa kaka ako anafunga ya pili hapo sawa lakini kama hakuwahi funga nae ndoa mwambie kaka ako aendelee na mipango ya harusi kama kawa. huyu hawezi fanya lolote na hana madhara.
   
 11. bht

  bht JF-Expert Member

  #11
  Mar 23, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  kwenye red nawapenda sana wa hivo.......angechuna brake za mbuzi hapa
  kwenye blue miaka sita baadae ndo analiona hilo....alipokuwa apoozea imekuwaje  hata kama mtoto ni wenu bana, hakuna pingamizi hapo hebu endeleeni na mipango yenu na siku ya siku akileta show off wekeni mlinzi ampe kibano.....huyo dada anataka kumkomoa jamaa tu hamna la ziada lakini kw avile mmeshajua mpango wake mie sioni tatizo
   
 12. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #12
  Mar 23, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
   
 13. Noname

  Noname JF-Expert Member

  #13
  Mar 23, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,269
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  sasa hii ya kuwa na illegitimate child imekuwa common ehh? ppl are not responsible at all and those poor kids have to pay... My heart goes to the kid poor little thing...

  that was off topic... anyway back to the topic... naona huyo mchumba mwenyewe hana msimamo... kwanini anaanza kuzira?
   
 14. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #14
  Mar 23, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  sawa mtoto anaumia, lakini mbona mama ndo alifumaniwa na uhusiano ukafa? na bahati mbaya kumbe ana mimba ambayo kakaa kimya hadi six years later. mama ndo ana makosa,angekuwa mwadilifu basi angeomba msamaha waendelee na uhusiano japo isingeguarantee ndoa.
   
 15. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #15
  Mar 23, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Wifi taratibu!
   
 16. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #16
  Mar 23, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Huyo anatishia tu, hakuna kanisa linalotoa pingamizi la ndoa sababu ya kuzaa na mtu, ni proof ya kuoa tu ndo inakubalika.
  huyo wifi mpya naye sasa mi nina mashaka naye, ni kweli anampenda huyo kakako na anataka kuwa naye au vipi? alichotakiwa kufanya kwa sasa ni kuwa karibu na huyo mtarajiwa ili amsaidie mawazo nini cha kufanya. kama mume amemhakikishia kuwa anampenda yeye sasa hasira za nini?
   
 17. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #17
  Mar 23, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Mwenye kupinga ndoa ni mwanamke katika mazingira haya:

  1. Mwanamke uliyeishi naye mfululizo kwa kipindi cha miezi sita (awali ilikuwa miaka miwili) na kuendelea na ambao mnafanya tendo la ndoa kama mume na mke, kusheria anatambulika kama mke hata kama hamjafunga ndoa, hivyo ni lazima muachane kisheria. Kwa huyu binti na taarifa ya mleta mada inaelekea kuwa hawakuwahi kuishi pamoja na huyu ndugu yako zaidi ya kupeana mimba,

  2. Mwanamke uliyezaa naye bila ndoa hata kama hamjaishi pamoja lakini hutunzi yule mtoto. Huyo mwanamke ana haki ya kuzuia ndoa kwa muda ili aweze kupata hatima ya matunzo na malezi ya mtoto yule. Kwa binti huyu si tatizo kwani nduguyo amekubali kumtunza na kumelea mtoto. Pingamizi la ndoa hapa hakuna.

  3. Mwanamke uliyefunga naye ndoa, hata kama mmeishi kwa sekunde na mkaachana, hili ni pingamizi tosha hadi pale talaka itakapotolewa mahakamani/au vyombo vingine vyenye mamlaka ya kutengua ndoa. Huyu binti hana ndoa hivyo pingamizi hakuna.

  Kwa yote hapo juu huyu binti hawezi kuwa pingamizi kwa ndoa hii na hii ni lazima iwekwe wazi kwa wachungaji/mapadre kabla ya siku ya ndoa il asije akavamia ile ibada maana inawezwa kusitishwa ili kusikiliza malalamiko hivyo itakuwa imeharibu gharama zenu.
   
 18. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #18
  Mar 23, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
   
 19. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #19
  Mar 23, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  hawajawahi kufunga ndoa.
  Unajua mtarajiwa ni mgeni hapa dar amezaliwa na kukulia Arusha, ndo mara yake ya kwanza kuja dar, kaja kujiandaa na ndoa yake, kufika tu kakutana na mgogo yeye anaongea moja mwenzake mia, kwanza hakutegemea, pili imemshtua alivyopata hizo taarifa alizimia masaa 2 ndo akashtuka, mama mtoto anamwambia hii ni dar unafikiri upo Arusha hapa 2one hiyo ndoa kama utafunga.
   
 20. Noname

  Noname JF-Expert Member

  #20
  Mar 23, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,269
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  both are wrong...having unprotected sex is being irresponsible...whatever goes around comes back...thats Karma... lakini huyu mamii ndo anamakosa zaidi halafu she dont stand a chance... so mchumba wa huyu baba should be smart and go ahead with marriage...
   
Loading...