Zanzibar 2020 Namba 5: Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi achukua fomu kuwania Urais wa Zanzibar

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,402
Mbunge wa Kwahani na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa katika serikali ya awamu ya Tano Dkt. Hussein Mwinyi achukua fomu kwa lengo la kuwania nafasi ya Urais wa Zanzibar katika ofisi za chama cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui mjini Unguja.

photo_2020-06-17_13-50-04.jpg


WASIFU
Dkt. Hussein Ali Mwinyi ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Kwahani, Unguja Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Alizaliwa Desemba 23, 1966 Unguja, Zanzibar..

Elimu yake
Dkt.Hussein Ali Mwinyi alisoma elimu ya Msingi jijini Dar es salaam kati ya mwaka 1972 hadi 1976 katika shule ya Msingi Oysterbay. Baadaye mwaka 1984 hadi 1985 aliendelea na masomo yake nchini Misri katika shule ya Msingi Manor House Junior, hii ilitokana na wazazi wake kuhamishiwa nchini Misri kikazi katika Ubalozi wa Tanzania ulioko Misri.

Dkt. Hussein Mwinyi alirejea nchini Tanzania na kuendelea na masomo ya Sekondari kidato cha kwanza hadi cha nne katika Shule ya Sekondari Tambaza. Dkt. Mwinyi alifaulu kidato cha nne na kupangiwa Shule ya Sekondari Tambaza kujiunga na masomo ya kidato cha tano na Sita.

Mwaka 1985 alielekea nchini Uturuki kusomea utabibu katika Chuo Kikuu cha Marmara kilichopo Istanbul nchini Uturuki na kuhitimu Shahada ya utabibu wa Binadamu mwaka 1992. Mwaka 1992 hadi 1993 Mhe. Mwinyi alikua Ofisa wa kitengo cha Nephrology cha Hospitali ya Royal Sussex Iliyoko Brighton nchini Uingereza.

Mwaka 1994-1995 Akiwa Uingereza Dkt. Mwinyi alijiendeleza Zaidi kielimu katika masomo ya utabibu ambako alihitimu shahada ya uzamivu. Mwaka 1996 Dkt. Mwinyi alirejea nchini Tanzania na kufanya kazi kama Msajili katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na baadaye mwaka 1998 hadi 2000 alihamia Hospitali ya Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hurbet Kairuki (HKMU) akiwa Mtaalam wa Viungo na Mkufunzi Mwandamizi wa wa chuo hicho.

Uzoefu Kazi.
Dkt. Mwinyi aliingia kwenye ulingo wa Siasa na kuwa Mbunge wa jimbo la Mkuranga mkoani Pwani kwa miaka 5 toka 2000 hadi 2005. Baada ya kuwa mbunge wa jimbo la Mkuranga kwa miaka 5 alikwenda Zanzibar kuwania nafasi ya Ubunge katika jimbo la Kwahani ambalo analitumikia mpaka sasa.

Akiwa mwakilishi wa jimbo la Kwahani ameshika nyadhifa mbalimbali Serikalini zikiwemo za Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii toka Novemba mpaka Desemba mwaka 2005, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) kuanzia Januari 2006 hadi Februari 2008, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii kuanzia Mei 2012-2014 na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa nafasi anayoitumikia mpaka sasa.

Nyadhifa nyingine.
Dkt. Mwinyi amewahi kuwa mjumbe wa Kamati mbalimbali za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zikiwemo za Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Kamati ya Mambo ya Katiba na Huduma za Jamii. Aidha amehudhuria mafunzo ya kitaaluma katika nchi mbalimbali ikiwemo Uturuki, Uingereza na Marekani.
 
Ifike wakati tabia ya kurithishana madaraka ya nchi ikomeshwe , Wazanzibar ambao baba zao hawakuwa viongozi hawana haki ya kuwania uongozi ?
Hongera Hussein Mwingi kuchukua fomu tunakutakia Uraisi mwema utaupata tu inshallah
Kwani vyeo vyote zanzibar vya kugombea watu wanarithishana? kama ubunge na baraza la wawakilishi? acha uzushi

Na wanaowapigia kura wawe wagombea mfano kamati kuu ya chama,halmashauri kuu na mkutano mkuu wote ni watoto wa viongozi? hoja yako haina mashiko
 
Mbunge wa Kwahani na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa katika serikali ya awamu ya Tano Dkt. Hussein Mwinyi achukua fomu kwa lengo la kuwania nafasi ya Urais wa Zanzibar katika ofisi za chama cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui mjini Unguja.

Ni jambo jema!

Muislamu wa 2025 amepatikana JMT!
 
Back
Top Bottom