Mtoto wa mwenzio ni wako na si mwenzio | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto wa mwenzio ni wako na si mwenzio

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Nov 21, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,606
  Likes Received: 5,781
  Trophy Points: 280
  Nyie wazazi,jamani embu badilikeni kidogo mbona hivi
  yaani damu zenu sikuzote zilikuwa wapi mpaka mmeanza kuparamia watoto
  wa wenzio...leo hii unamkuta mzee mtu mzima akiwa na katoto kadogo
  jamani hembu fikirieni na nyie watoto wenu waanzwe kufanywa na watu wzima mnajisikiaje???hivi ni hamu ni matatizo ya familia ama??kwa nini msifwate majimama walioachika ama wenye matatizo ya familia wanaotafuta mabwana....jamani waachieni vijana wenu damu zao zichanganyike ..sasa wewe mzee unakimbizana na damu changa matokeo yake unakufa na shinikizo la damu huku mama ama mkewe ajui source..,tuache akili za kusema mtoto wa mwenzio mwenzio..jamani embu waangalieni na hao vijana imagine huu ugonjwa wa ukimwi utawamaliza wangapi kwa style hii.....???ambu angali watoto wangapi wanavijiboyfriend huku wanavizee vinapunguza matatizo yao.... nanyi madada zetu jamani tunajua kuna shida duniani embu zikimbizie kwa vijana wenzako basi jamani????mtawaua vijana wenzenu kwa hali hii...maana najua ile mizee inaflow kavu...haya jamani mwenye macho ambiwi tazama....
   
 2. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,189
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  MM umenena vizuri sana.
  Mtoto wa mwenzio ni mkubwa mwenzio ni kauli inayotolewa na mapunguwani. Maadili ktk jamii yetu yameporomoka kwa kiwango kikubwa sana.. fikiria zee zima au mama mtu mzima anatoka na katoto tena bila hata soni machoni au dhamira kumsuta moyoni! Mtu mwenye akili timamu hawezi kuacha watu wa rika lake na kwenda kuparamia vitoto. Ni wajibu wetu kuwalinda watoto wetu ili wasidanganywe na sugar dady/mumy. Na watoto nao waache tamaa.
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Nov 21, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,606
  Likes Received: 5,781
  Trophy Points: 280
  kweli mkuu hilo litasaidia kurekebisha maadili ya jamiiw acha vijana waumizane wenyewe kwa wenyewe kama nyie wazee amkuutumia ujana wenu vizuri waacheni vijana warekebishe makosa yenu na si kuanza kuparamia vitoto vya shule...inasikitisha sana niiikiwa azani sec pale ukiwa unaenda tafuta mlo wa usiku unakuta vitoto vya jangwani vinarushwa ukutani kama paka akiamungu...na huku nje walinzi wanawapokea kwa heshima na taadhima huku VX,VOG zinawasubiri nakumbuka mlinzi mmoja aliniiacha hoi pale alipoamua kuja usiku na ngazi anasema kila ngazi anaetuma anatoa 3000 kwenda kurudi 2000...ila ukidondoka unajiiudumia ilikuwa kazi kweli kweli...sasa maisha kama haya yakiendelea kuachiwa ni hasara na hatari kwa jamii....na ndio maana hatushangai ma profesa na elimu zao kuanza kukimbizana nao wadogo wetu kisa wakiamini wenzao na si watoto wa wenzao...mmmhhh jamani Jibaba la miaka 55 = na 17/18 haya tuwaachie jamhuri
   
 4. IronBroom

  IronBroom JF-Expert Member

  #4
  Nov 21, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 524
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  M100,talking from experience....?
   
 5. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #5
  Nov 21, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135


  ..........Mimi yalinitokea kabisa haya mambo, kabla ya kumaliza form six kuna project unatakiwa kufanya. Basi mimi na wenzangu tukaamua kufanya project yetu pale muhimbili.
  Kuna huyo mbaba mkuu wa idara flani pale muhimbili, ni mbaba mtu mzima na mashavu yameshaanza kumporomoka, akaanza kunitaka mie kimapenzi. Kipindi hicho mie ndio kwanza nina 19 yrs. Huyo mbaba akasema tuandike namba zetu za simu ili atakapotuhitaji kutuelekeza mambo ya idara yake atuite.
  ........Basi yule mbaba kumbe akashika namba yangu, jioni yake nipo shule naona simu inaita kumbe alikuwa yule baba, ndio hapo akaanza zake za kuleta za kunitaka. Mie nikamwambia wewe ni kama baba yangu, akanijibu wewe sio mwanangu, na mtoto uliyemzaa, usiyemzaa mkubwa mwenzio. Nikastaajabu ati!!!! Mtu mzima kunijibu hivyo.

  Basi yule baba akaanza kutuma vocha za simu, mara aniwekee dola kumi mara 20, yaani alikuwa hana hata haya mzee mzima.Akanifuatilia hadi mwenywewe akashindwa maana nilikuwa sina hata mpango naye.

  Enyi wababa hebu mjiheshimu, msipende kuparamia wanafunzi.Tafuteni wakubwa wenzenu.
   
 6. Sokwe Mjanja

  Sokwe Mjanja JF-Expert Member

  #6
  Nov 21, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Pretty jamani mbona 19 ulikuwa mkubwa kabisa jama, sema tu labda ulikuwa unasoma ila mambo ya umri jamani mbona ulikuwa unatosha kabisa.......
   
 7. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #7
  Nov 21, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,606
  Likes Received: 5,781
  Trophy Points: 280

  mmmmmmmh kwa style hiyo mtatumaliza jamani!!!!
   
Loading...