Mtoto wa Mwenyekiti wa CCM aliyeuawa Kibiti, naye afariki Muhimbili

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
Mtoto wa Mwenyekiti wa Tawi la CCM, Njia Nne, Kibiti, amefariki dunia katika Hospitali ya Muhimbili alipokuwa akipata matibabu.

Mtoto huyo, Nurdin Kirungi, alipigwa risasi ya tumbo Mei 17 mwaka huu katika tukio ambalo baba yake, Iddy Kirungi aliuawa kwa kupigwa risasi begani na watu wasiojulikana.

Chanzo: Mwananchi

Awali, taarifa za kupigwa risasi mtoto huyo zililetwa JF, soma => KIBITI: Mwenyekiti wa CCM, Kata ya Mtunda auawa kwa kupigwa risasi
 
Aisee inahuzunisha sana.. Raia wasio na hatia wanaendelea kuuawa na bado viongozi wa kisiasa na wa jeshi la polisi wanaendelea katika nafasi zao kama vile yanayotokea ni ya kawaida.. Wanakuja na matamko ya zimamoto kisha wanaendelea na hamsini zao.. Very sad sana..

Wapumzike kwa Amani wote waliokumbwa na kadhia hii..
 
Pole kwa familia ya Ndugu Kirungi.
Mamlaka za Juu shurti pelekeni insiders waliobobea katika mtandao wa hao Mahayawani yanayotaoa UHAI wa ndugu zetu.
Hii ndio suluhisho la kujua kiini/chanzo cha tatizo, mahali wanakopata huo ufadhili wao na mbinu ya kuwatawanya.

Wingi wa Askari mtaani pekee hautoshi kuyamaliza makundi haya haramu yanayochipuka kama Mche wa Mbuyu...
 
kibiti iangaliwe kwa macho 3 hawa wanaanza kidogokidogo mwishowe tutageuka somalia...........

instead:
serikali kukimbizana na michango yetu ya rambirambi kutukwapulia pesa tulizochanga na kutumia nguvu nyingi kuhangaika na raia wema wenye kufarijiana kwa kufiliwa na majanga mengine ingeelekeza nguvu mingi kibiti maana mpaka dakika hii haijajulikana ni mauaji gani mara ujambazi, mara ugaidi mara visasi ......................

hata mbuyu ulianzakama mchicha na ni bora kumkunja samaki akiwa mbichi......


kibiti kuna tatizo linalokuwa kila uchao
 
Ni wakati muafaka wa wale jamaa wa haki za binadamu kujitokeza na kuwaambia hao majambazi juu ya haki za binadamu na kupunguza nguvu kubwa.. Kibiti kuna nini mpaka watu wauliwe hivyo? Kama ni ugaidi, ipo siku tu! Tusiojua tuachie mamlaka husika.... Magaidi wenyewe hutumia njia zote hovyo kukamilisha dhamira zao wako radhi kufa pia. Tunayajua na tumeyaona, tuwasaidie makamanda wetu.
 
Na ccm na serikali yao walivyo wajinga wamesema kupitia waziri mwigulu kuwa wataendelea kuwapa mateso maana wauaji wako nao
 
R.I.P Mkuu nurdin KIRUNGI , ipo siku waliokufanyia unyama huo watajulikana tu
serikali ina mkono mrefu. Mamlaka hazilalali , ziko kazini kuwasaka watu hawa wasio wema
kwa jamii yetu.
 
Back
Top Bottom