Mtoto wa Mungai mbaroni ni Kuhusu Saga la Kugushi Vyeti vya Elimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto wa Mungai mbaroni ni Kuhusu Saga la Kugushi Vyeti vya Elimu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mtanganyika, Sep 22, 2008.

 1. Mtanganyika

  Mtanganyika JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2008
  Joined: Jul 18, 2007
  Messages: 1,613
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 180
  Na Richard Bukos
  Mtoto wa aliyekuwa Waziri wa Elimu wa zamani Joseph Mungai aitwae Justina Mungai na wenzake saba ambao ni wafanya kazi wa benki Kuu ya Tanzania (BoT), Jana (Ijumaa) walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam baada ya kutiwa mbaroni wakidaiwa kuwa na vyeti feki....

  Vijana hao waliotiwa mbaroni na kufikishwa mahakamani hapo ni mtoto huyo wa kigogo wa zamani na watoto wengine wa vigogo ambao ni Christina G. Ntemi, Siamini E. Kombakono, Janeth Mahenge, Betha C. Massawe, Jacqueline D. Juma, Philimina P. Mutagurwa na Amina M. Mwinchumu.

  Akiwasomea mashtaka yao Mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo Abubakar Mbangi alidai watuhumiwa walitenda kosa la ‘kufoji’ vyeti vya elimu ya sekondari kwa nyakati tofauti ambapo washitakiwa wote walikana mashtaka dhidi yao.

  Baada ya kukana makosa hayo watoto saba wa vigogo hao walipelekwa rumande katika Gereza la Segerea hadi kesi hiyo itakapotajwa tena Octoba 6, mwaka huu isipokuwa Philimina Mwinchumu ambaye alitimiza masharti ya dhamana na kutolewa.

  Source na Global Publisher
   
 2. Sita Sita

  Sita Sita JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2008
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 1,196
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mtanganyika hiyo habari nzuri sana. Naomba kama una habari zaidi ututumie. Mfano;- Dhamana ilikua kiasi gani (kwa nini washindwe kulipa) na utupatie majina ya hao vigogo ambao watoto wao wameburuzwa mahakamani.

  kama kuna mtu ana taharifa za hawa watoto ni vyema muziweke hapa.
  Waliajiriwa mwaka gani?
  Walikua wanafanya kazi katika idara gani hapo BOT?
  wana vyeo gani?
   
 3. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2008
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Fanya utafiti wa kutosha mkuu mtoa hoja huyo si bint yake bali dada yake aitwae justina james mungai. Mh. Mungai (joseph james mungai) ni hilo tu muungwana
   
 4. Utamaduni

  Utamaduni JF-Expert Member

  #4
  Sep 22, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 1,198
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Kama kweli vile!!

  kama kweli hawa hatua za ksheria zitachukuliwa dhidi ya hawa watoto na haki kutendeka ya wao kuhukumiwa adhabu sawa kadiri ya kosa lao, huo utakuwa mfano na kwa wengine walioghushi vyeti hapo BoT waache kazi wao wenyewe mapema.

  Lakini kwa ninavyoijua sirikali hii, utashangaa tu kesi inatajwa mara 2 au 3 kisha huisikii tena labda uje kuwaona hao watoto mtaani ktk idara nyingine nyeti nchini. hii ndo nchi ya mafisadi bwana
   
 5. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2008
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  mWINCHUMU HUYU YUKO RELATED NA MH.MSOMI MWINCHUMU (MB) KIGAMBONI?
   
 6. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #6
  Sep 22, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  thamana ilikuwa ni mil 5 mmoja kati ya hao ndio alifanikiwa hiyo dhamana wiki iliyopita sijui wenginekama walitolewa na dhamana au la
   
 7. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2008
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,982
  Likes Received: 20,372
  Trophy Points: 280
  Wakati mwingine wengine tunashindwa kutambua na kuamini kuwa unaweza kukaa darasani na bado ukapata kazi inayohitaji mtu aliyekaa darasani. Kusoma naelewa kabisa ni jambo moja na kupata kazi ni jambo jingine (na hasa kama unasoma ili uajiriwe kama hawa watuhumiwa ambao wanatuhumiwa kutumia vyeti ambavyo hawakuvisome!)

  tatizo kubwa la ajira zetu hapa nchini kwa baadhi ya ofisi suala limekuwa si unajua nini 'technical know how' bali unamjua nani na wewe unafahamiana na nani 'know who'. hii haiwahusishi watoto wote wa vigogo ambao kiukweli kabisa wapo ambao wameajiriwana wanashika nafasi si kwa kujuana bali kwa uwezo na weledi wao katika mambo mbalimbali.

  Nitmshangaa mdau (tukirejea katika suala la binti wa Mungai) anayemtofautisha Mungai na huyu binti kwa kuwa tu eti ni mtoto wa dada yake. sisi tunajijua na kwa mfano ni ngumu sana kunitofautisha mimi na mtoto wa mjomba wangu kunapokuja sualal la kazi na kama hayo, hakika 'bado huyu binti ni mtuhumiwa' haishangazi kwa mtu asiye na sifa kuajiriwa sehemu ambayo 'anajulikana' mazingira yetu Watanzania ni mashahidi.

  Jaribu kuifikiria ile iliyokuwa NYANZA yenye nguvu pale Mwanza, usiisahau iliyokuwa bodi yawakulima iliyokuwa ikiongoza shule nyingi sana za sekondari karibu katika kila wilaya. waajiriwa wa hapa wengi na hili neno 'wengi' ninalimaanisha walikuwa ni wafanyakazi wenye mahusiana ya karibu sana na mwenyekiti wa bodi ambaye alikuwa akitoka katika wilaya moja mkoani mwanza ambayo kufika pale lazima uvuke maji.

  Hii inaathiri sana na labda pia inatukumbusha kuwa KUNA BAADHI YA OFISI SI ZA WOTE.  UKIYAJUA MENGI YA NJE NA KUJIFUNZA MACHACHE YA NDANI, HAKIKA HUFAI KUITWA MZALENDO, NA HAIJALISHI KAMA UNAJUA KUIMBA WIMBO WA TAIFA LETU
   
 8. Gelange Vidunda

  Gelange Vidunda JF-Expert Member

  #8
  Sep 22, 2008
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 312
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Habari zinasema eti they are mere scapegoats as they work in the old notes counting department.

  Still, though, kugushi vyeti ni noma. Swali linakuja: What about people in government and legislative body, Bunge, will they be buruzwad mahakamani kujibu mashtaka? Baraza la JK limekaliwa na mawaziri kama wanne hivi ambao wana questionable qualifications kama doctorate from known diploma mills. Hawa je?

  Nimesikia interesting mails into Clouds FM this morning when busing into the city. Someone wrote: mbona hizo kazi hatukuziona zikitangazwa iweje sasa waje wanatupigia kelele eti watoto wa vigogo wamefoji vyeti - ina maana ajira za huko ni za hawa vigogo na watoto wao!

  Obe, FDR. Jr wrote that she is Mungai's sister and not "mtoto wa dada yake...."
   
 9. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #9
  Sep 22, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  ....Mbona sioni kama kuna dalili ya hao kuwa watoto wa vigogo zaidi ya hilo jina la Mungai??? Vipi wale akina Lowassa, Mahita, Mkapa, Sumaye na wengine???
   
 10. m

  mTZ_halisi Member

  #10
  Oct 3, 2008
  Joined: Oct 26, 2007
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  i am wondering the same??? kigogo yuko wapi hapo?
   
 11. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #11
  Oct 4, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  Hakuna kesi hapo!!!!huyo ngono ndulu anawaafanya watu makenge!!!!!!!!!
   
 12. k

  kipanga mweupe Member

  #12
  Oct 4, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Changa la macho hilooooooooooooo.......!

  Hamna mtoto wa kigogo yeyote yule hapo, na wamechukua wahesabu noti tu.....mbonahawajachukua huko juu?

  Hapo tunadanganyana tuu!! Nadhani wanakijiji tunaliona hilo.....na Mungai yule si mtoto wake!!!!
   
 13. Tonga

  Tonga Senior Member

  #13
  Oct 4, 2008
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 175
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hilo jina Mungai limewekwa chambo tu hapo kufunika zali la hao watoto halisi wa vigogo tunaotaka kusikia qualification zao zilizowafikisha hapo walipo na hao ni watoto wakina lowassa, Sumaye, Kigoda,JK, na wengineo hao ndio tunawahitaji achana na hawa vidagaa.
   
 14. M

  Mage Member

  #14
  Oct 4, 2008
  Joined: Sep 2, 2008
  Messages: 42
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kweli, nakubaliana na wewe asilimia mia moja kuna office zingine haziendewagi na ujuzi kabisaaaaa, kujuana mbele hata uqualify vipi no one see u,matokeo yake watoto wa wakulima tunajuta tulienda kusoma ili iweje coz hata ukitaka kuwa mjasiriamali huna starting point.Sio siri washughulikie ili swala litokomezwe kabsaaa.
   
Loading...