Lekachonka
Member
- Dec 17, 2016
- 35
- 17
Kuna jambo kubwa sana la kujifunza kupitia kauli hiyo ya mzee Pinda. Alitoa mfano wa China,anasema alijiuliza kuwa China inao watu takribani 1.3 B ,akataka kujua Communist Party (CP) itakuwa na wanachama wangapi? Anasema alistaajabu sana pale alipokuta chama kina wanachama milioni 80 tu. Ambayo hii 6% ya wachina wote walio wanachama wa CP.
Hapa kwetu Tanzania,CCM inao takribani wanachama milioni 6,ambao ni kama 11.5% ya Watanzania wote walio wanaCCM. Akazidi kusema kuwa kinachofanya chama kipendwe si kuwa na wanachama wengi,ni chama kujikita zaidi katika kutatua matatizo ya Wananchi,chama kuwa na viongozi waadilifu. Akasisitiza kwa kusema....Mzee hawa wanaCCM ulionao wanatosha!! Hapa lazima tujiulize kidogo.
1. Kwanini mzee huyu kaamua kuzungumza hivo katika wakati huu ambapo tunaona wimbi kubwa la usajili wa wanachama wapya kutoka upinzani?
2. Kwanini anaona hamna umuhimu wa kuwa na wanachama wengi zaidi iwezekanavyo?
3. Mzee alikuwa anamwambia Rais kuwa upinzani kuwepo ndiyo uhai wa CCM na Taifa kwa ujumla?
Aliyeielewa kauli ile ya Mzee pinda,tusaidiane kuitafakari.