Mtoto wa Mkulima Mizengo Pinda kumjibu Lowassa Ijumaa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto wa Mkulima Mizengo Pinda kumjibu Lowassa Ijumaa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fareed, Jun 28, 2011.

 1. F

  Fareed JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda, maarufu kama "Mtoto wa Mkulima," Ijumaa wiki hii (Juni 30, 2011) atahitimisha mjadala wa bajeti ya ofisi yake ya 2011/12 Bungeni. Hii itakuwa ni fursa nzuri kwa Pinda kujibu mapigo kufuatia Waziri Mkuu wa zamani aliyejiuzulu kwa kashfa ya ufisadi ya Richmond, Edward Lowassa, kuinyooshea kidole serikali ya Rais Jakaya Kikwete na Pinda kuwa inaugua ugonjwa wa kuogopa kufanya maamuzi magumu.

  Lowassa, huku akishangiliwa na kundi la wabunge njaa wa CCM wanaomuunga mkono, alijitapa kuwa alipokuwa PM alithubutu kufanya maamuzi magumu kama kuvuta maji kutoka Lake Victoria mpaka mikoa ya kanda ya ziwa licha ya Misri kupinga mradi huo.
  Ijumaa itakuwa ni fursa muafaka kwa Pinda kukabiliana na Lowassa moja kwa moja kwa kujibu kitendo chake cha kuifokea serikali eti inashindwa kuthubutu na kufanya maamuzi magumu.

  Swali la kujiuliza, Je Pinda ana ubavu (guts) za kumjibu Lowassa au atanywea na kuogopa kupambana naye? Kuna uwezekano kuwa Pinda atawapa mawaziri wa ofisi ya Waziri Mkuu kumjibu Lowassa, badala ya yeye mwenyewe kufanya hivyo ambayo itakuwa ni kosa kubwa la kiufundi na ataonekana kumuogopa Lowassa.

  Kama Pinda kweli ni kiongozi makini, atamjibu Lowassa kwa umakini mkubwa na kumwambia kuwa serikali imekuwa ikichukua maamuzi magumu kama kuhakikisha kuwa viongozi wakubwa wakiwemo mawaziri wanaohusishwa na kashfa za ufisadi wanalazimishwa kujiuzulu nafasi zao za uongozi kwenye serikali na chama.

  Pinda inabidi aseme sasa serikali imefikia uamuzi mgumu wa kuiruhusu TAKUKURU iwachunguze kikamilifu na kuwafikisha mahakamani viongozi wote wa zamani waliojiuzulu kutokana na tuhuma za ufisadi. Hii ni pamoja na kuwafikisha mahakamani viongozi wa umma wenye utajiri wa mashaka (unexplained wealth) ili waeleze utajiri wameupata kwa njia zipi halali.

  Je, Mtoto wa Mkulima yuko tayari kupambana na fisadi Lowassa? Jibu tutapata Ijumaa wiki hii!
   
 2. N

  Ngao One Member

  #2
  Jun 28, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Kweli Ijumaa Bungeni itakuwa hapatoshi. Lakini kwa tabia ambayo Pinda amekuwa akiionesha tangu apewe cheo cha PM mwaka 2008, sitarajii kama atatoa kauli kali yoyote. Pinda is a weak leader ndio maana fisadi kama Lowassa anakuwa na audacity ya kuinyooshea kidole serikali pasipo kuwa na wasiwasi wowote ule.
   
 3. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  thubutuu!unacheza na EL nini wewe,i can bet!
   
 4. POSHO MAVYEO

  POSHO MAVYEO JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 377
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  --wao wakae kimya huyo ni mfadhili wao sana hatakuja na porojo na kusema anaona BONGE
  nina hakika lowasa alitoa hiyo kauli baada ya kuwashinda huko kwenye vikao vya siri kumtaka avue gamba na yeye kutishia kumvua jk
  --- kama mtu umezaliwa jana unaweza kusema jk anaubavu wa kufanya hivyo na serikali yake lakini kama kwenye ni mtu mwenye umri wa kutosha kwenye siasa za bongo utajua kabisa jk ni sehemu ya wapambe wa lowasa kwa muda wa maisha yao yote , mtoto hawezi kumza baba kiboko ya lowasa ndani ya CCM ni SITTA mpaka sasa ni yeye tu aliyekwisha mpaka huyo bwana machungu kwa kumng'oa uwaziri mkuu
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Jun 29, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Mnajua watu wanampa Lowassa nguvu kubwa ambayo hana. Inanikumbusha simulizi ka yule jamaa aliyesifiwa kuwa "ameua saba kwa mpigo".
   
 6. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  in ur dreams ndugu! kuna mbunge nilimsikia jana akisema kuhusu takukuru kubadilishwa all possible names and yet failing to deliver. Yaani unataka takukuru iwachunguze mabosi wao (waliowapa ugali)? i am yet to see that to blv it is practically possible in bongoland!

   
 7. F

  Fareed JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mzee Mwanakijiji, asikwambie mtu Lowassa ana nguvu sana CCM kwa vile yeye na Rostam wanatumia pesa nyingi sana kuhonga wabunge, wajumbe wa NEC, wajumbe wa Kamati Kuu na wajumbe wa Mkutano Mkuu. Ungeona jinsi wabunge wa CCM walivyokuwa wanaripuka kumshangilia wakati anaongea Bungeni ndiyo ungepata kipimo halisi. Tafadhali tafuta footage ya mchango wa Lowassa Bungeni.

  I can assure you that kama Lowassa atajitokeza kuwa mgombea Urais wa CCM mwaka 2015 na Kamati Kuu ikafanya kosa la kupitisha jina lake miongoni mwa wanachama watatu ambao wapigiwe kura na NEC na Mkutano Mkuu wa chama, Lowassa ataibuka mshindi kwa kura nyingi dhidi ya mgombea yoyote yule licha ya kuwa amechafuka sana na tuhuma lukuki za ufisadi kwa kuwa ana nguvu kubwa ya pesa na CCM kimetota kwa rushwa kwa sasa.
   
 8. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Yeye as personal, anaamini nguvu hizo hana na ndo ilivyo. Issue ni kwamba njia zilizotumika na watu aliosaidiana nao kufika hapo alipo.
   
 9. F

  FUSO JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,855
  Likes Received: 2,331
  Trophy Points: 280
  nani ndani ya CCM nitajie mwenye nguvu kuliko lowassa, hata mmoja tu? kumbukeni mtandao ulioshinda na unaoendesha serikali ndio yeye alikuwa engineer mkuu chini ya uzimamizi wa chief RA, leo hii ccm wakitaka kuvurugana wajaribu kumnyakanya uanachama hapo ndiyo mpira utanoga.

  Mwaga mboga nimwage ugali phylosophy itatumika, na ndiyo maana magamba bado wanafikiri njisi ya kumwaga mboga kwenye sahani.
   
Loading...