Mtoto wa miezi nane aibiwa katika mazingira ya kutatanisha mkoani Mwanza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto wa miezi nane aibiwa katika mazingira ya kutatanisha mkoani Mwanza

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by shaliza, Jul 6, 2011.

 1. s

  shaliza Member

  #1
  Jul 6, 2011
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwanamke mmoja anayesemekana ni mke wa mtu,alikuwa ametokea wa Mara willaya ya Tarime alikwenda, Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya kuomba kufanya kazi za ndani kwa mama mmojo (majina yao yamehifadiwa) inasaemekana huyO dada wa ndani walipatana na mme wake kwamba mkewe akatafute kazi za ndani ili kwenyw nyumba ambayo kuna mtoto mchanga ili azma yao ya kumwiba itimie kwa ajili ya shuguli zinazohhusiana na masuala mya utajiri.

  Mama mwenye mtoto aliondoka na kumwacha dada wa kazi wakaondoka kwenda kwenye sherehe, kitendo kile cha wao kuondoka wakawa wamefanya kosa la jinai ,yule daa mlezi akamchukua yule kichanga na kutoroka nacho,waliporudi wakakuta mtoto hayupo na yule mlezi hayupo,ndipo walipotahamaki na kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi.

  Jeshi la Polisi mkoani Mwanza likaanza kazi ya upelelezi likishirikiana na polisi wenzao mkoani MARA wakaanza kuwasaka watuhumiwa hao,iluichukua takribani siku nne wakwawa wamepatikana na mtoto alikutwa hajadhurika, walipobanwa walisema mganga aliwatuma kichwa cha mtoto mdogo ili awatengenezee dawa ya utajiri. kamanda wa polisi mkoani mwanza ametahadharisha watu kuwa makini na watu wasiowafahamu kwani wengine huwa majambazi na hata magaidi.
   
 2. A

  Aine JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Glory to God huyo mtoto amepatikana, dunia hii inakaribia kwisha, yaani unatumwa kichwa cha mtoto na wewe bila woga unamchukua mtoto ili akatolewe kichwa jamani!!!!! na walaaniwe hao waliofanya hivyo, na hongera sana kwa Polisi waliofanikisha kupatikana kwa mtoto huyo, big up kwa kweli.
   
 3. l

  lumimwandelile Senior Member

  #3
  Jul 6, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  hivi huyo mama alieiba mtoto kama kweli anapenda utajiri si angemtoa mtoto wake mwenyewe. jamani wakina mama tuwe makini sana na watoto wetu.
   
 4. s.fm

  s.fm JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2011
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 669
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kwakweli sijui anahitaji adhabu ya aina gani..!
   
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  Jul 6, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  makubwa hayo
   
 6. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #6
  Jul 6, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hii habari inanikumbusha rafiki yangu aliyeibiwa mtoto mwanza maeneo ya Karuta na msichana wa kazi mwaka 2001. Bahati mbaya mtoto yule hajapatikana mpaka leo hii na kuwa chanzo cha mtafaruku na kufilisika kwa familia ile.
   
 7. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #7
  Jul 6, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,833
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Title....kiswahili sanifu ni kusema/kuandika 'mtoto ameibiwa' ama 'mtoto ameibwa'?Wataalam lugha tafadhali!
   
Loading...