Mtoto wa miezi minne azungumza mazito

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
May 9, 2007
3,831
2,790
Mtoto wa miezi minne azungumza mazito

Na Mashaka Mhando, Tanga

MTOTO wa miezi minne aliyezaliwa kwenye hospitali teule wilayani Muheza, amekuwa gumzo na kustaajabisha wakazi wa mji huo, wakiwamo wazazi wake, kutokana na kuzungumza akiwa na umri huo.

Mtoto huyo pichani aliyezaliwa Julai 16 mwaka huu, licha ya kuzungumza, pia amekuwa kituko kutokana na kutaka aitwe majina matatu ya Glory, Halima na Upendo, pindi anapoitwa na mtu yeyote akitaka kumsalimia.

Akizungumza juzi kwenye ofisi za gazeti hili barabara ya 15 Jijini hapa, mama wa mtoto huyo Bi Rosemary Mhina, mkazi wa mtaa wa Bin Seif, wilayani Muheza, alidai kuwa mtoto wake huyo ni wa ajabu kwani tangu akiwa mjamzito wa miezi saba, alikuwa akilia tumboni.

"Kwanza nilipokuwa na mimba, tumbo lilikuwa linaniuma sana, nilipofikisha miezi saba tumbo likiniuma, utamsikia mtoto analia tumboni, nikaenda hospitali, nilianzia Teule, nikaja huku Bombo na Tumaini, nilipopigwa 'ultra-sound' madaktari wakanieleza kuwa nitajifungua mtoto wa kiume, waliyemwona tumboni kwa kifaa hicho," alisema Bi Rosemary.

Akielezea zaidi kuhusu namna alivyobaini mtoto wake kuwa na mawasiliano na watu, mama huyo alidai kuwa mara baada ya kuzaliwa, alipofikisha miezi miwili, siku moja alilia sana wakati akimbembeleza "Nyamaza mwanangu usilie ngoja nikupewa maziwa".

Alisema baada ya kumweleza hivyo, mtoto huyo alitamka maneno yaliyomtisha mama yake huyo: "Mama usione nalia, nalizwa na mengi, kwanza baba alitaka uniue nikiwa tumboni, halafu maisha yako si mazuri mama nakuonea huruma."

Bi Rosemary alikiri kwamba baada ya kupata ujauzito kutoka kwa mwanaume (jina tunalihifadhi) ambaye amedai kwamba anafanya kazi katika hospitali ya Mount Meru, Arusha, alimpa sh. 30,000 ili akaitoe hospitalini wakati mimba hiyo ilipofikisha miezi sita.

"Yule baba alitaka nikatoe mimba ya mtoto huyu nikakataa, hata hivyo wazazi wangu hawakutaka mimi nizae baada ya kuwa na watoto wawili, niliogopa pengine ningefanya hivyo ungekuwa mwisho wangu," alidai Bi Rosemary.

Aliendelea kudai kuwa tangu mwanawe huyo awe naye amekuwa akitokewa na miujiza mingi na kipindi alichoanza kuzungumza, alimpeleka kwa wachungaji mbalimbali ili kumwombea, lakini kila anapokwenda huko akirudi anatokewa na vituko.

"Kipindi kimoja nilimpeleka kuombewa, usiku niliona paka wengi ndani nilimolala wakaniparura huku mwanangu Upendo akinicheka," alidai.

Mama huyo ameomba watu wamsaidie ili mtoto huyo asiwe na vituko hivyo kwani hivi sasa baba wa mtoto amemkimbia na hana mawasiliano naye tena.

HAKIKA DUNIANI KUNA MAMBO
 
Last edited:
Hii ni kali kuliko. Huyo mama asaidiwe the boy is extra ordinarly genius. Ujiniasi wake unatokana na un even mutiplication ya chromozone zilizomuumba. Afanyiwe uchunguzi zaidi na utafiti wa kisayansi ya kibailojia kabla waKiristu na waIsilamu hawajaanza kumgombania kila mtu akivutia kwake waKristu wakidai ni Nabii na Waisilamu wakidai ni Sharrif.
 
..Hamna kitu hapo.. Huyo muandishi wa habari alishuhudia huyo mtoto akiongea au ndio amesimuliwa na yeye ameshika bango? Mbona kila anayedai ana mtoto wa ajabu anaishia kuomba msaada tu kwa nini??? Aendelee kuomba mapadri na wachungaji huko aliko waendelee kumfanyia maombi ikishindikana aombe na mashehe wajaribu kumsaidia...
 
huyo mwandishi anapaswa kuwa amesafiri kwenda huko kumwona mwenyewe na sio kusimuliwa ofisini...pia kuwahoji majirani nk
 
I wish I could get more details about this issue. It might end up to be like the story of women who move around pubs with babies begging for money pretending that they just came from labour wards... but do it everyday. Let me try to investigate.
 
Nimeongea na jamaa toka Hospitali ya Teule, Muheza, Tanga. Anasema ni kweli mtoto alizaliwa hapo ila habari za mtoto huyo kuongea zimetokea mitaani. Hapo hospitali hakuna taarifa kama hizo. Nitazidi kufuatilia.
 
Hivi ni vitendo vya kishirikina visiwababaishe.Shetani anaweza kucheza na mwili wako kama anavyotaka 'especially if you have not submitted your life to Jesus Christ. 'Kaa chonjo hili linaweza hata wewe kukutokea kama bado hujampa Yesu maisha yako!
 
Hiyo most likely ni uzushi wa mama wa mtoto, kama sivyo ana tatizo la akili na hizo ni hallucination zake! Hizo za Dr ku-confirm possibly ni uzushi vilevile, ukichaa sometimes uko infectious, hasa ukiwa unaamini mambo ya kishirikina.
 
Mimi si muumini wa haya mambo ya miujiza ila habari nilizopata hivi punde ni kuwa huyo mtoto yupo. Na pamoja na kuongea, wanasema anatembea pia. Hata hivyo hakuna mtu ambaye amemuona. Nazidi kufuatilia nitapakua hapa mara nikipata habari za uhakika.
 
Mtoto wa miezi minne azungumza mazito

Na Mashaka Mhando, Tanga

MTOTO wa miezi minne aliyezaliwa kwenye hospitali teule wilayani Muheza, amekuwa gumzo na kustaajabisha wakazi wa mji huo, wakiwamo wazazi wake, kutokana na kuzungumza akiwa na umri huo.

Mtoto huyo pichani aliyezaliwa Julai 16 mwaka huu, licha ya kuzungumza, pia amekuwa kituko kutokana na kutaka aitwe majina matatu ya Glory, Halima na Upendo, pindi anapoitwa na mtu yeyote akitaka kumsalimia.

Akizungumza juzi kwenye ofisi za gazeti hili barabara ya 15 Jijini hapa, mama wa mtoto huyo Bi Rosemary Mhina, mkazi wa mtaa wa Bin Seif, wilayani Muheza, alidai kuwa mtoto wake huyo ni wa ajabu kwani tangu akiwa mjamzito wa miezi saba, alikuwa akilia tumboni.

"Kwanza nilipokuwa na mimba, tumbo lilikuwa linaniuma sana, nilipofikisha miezi saba tumbo likiniuma, utamsikia mtoto analia tumboni, nikaenda hospitali, nilianzia Teule, nikaja huku Bombo na Tumaini, nilipopigwa 'ultra-sound' madaktari wakanieleza kuwa nitajifungua mtoto wa kiume, waliyemwona tumboni kwa kifaa hicho," alisema Bi Rosemary.

Akielezea zaidi kuhusu namna alivyobaini mtoto wake kuwa na mawasiliano na watu, mama huyo alidai kuwa mara baada ya kuzaliwa, alipofikisha miezi miwili, siku moja alilia sana wakati akimbembeleza "Nyamaza mwanangu usilie ngoja nikupewa maziwa".

Alisema baada ya kumweleza hivyo, mtoto huyo alitamka maneno yaliyomtisha mama yake huyo: "Mama usione nalia, nalizwa na mengi, kwanza baba alitaka uniue nikiwa tumboni, halafu maisha yako si mazuri mama nakuonea huruma."

Bi Rosemary alikiri kwamba baada ya kupata ujauzito kutoka kwa mwanaume (jina tunalihifadhi) ambaye amedai kwamba anafanya kazi katika hospitali ya Mount Meru, Arusha, alimpa sh. 30,000 ili akaitoe hospitalini wakati mimba hiyo ilipofikisha miezi sita.

"Yule baba alitaka nikatoe mimba ya mtoto huyu nikakataa, hata hivyo wazazi wangu hawakutaka mimi nizae baada ya kuwa na watoto wawili, niliogopa pengine ningefanya hivyo ungekuwa mwisho wangu," alidai Bi Rosemary.

Aliendelea kudai kuwa tangu mwanawe huyo awe naye amekuwa akitokewa na miujiza mingi na kipindi alichoanza kuzungumza, alimpeleka kwa wachungaji mbalimbali ili kumwombea, lakini kila anapokwenda huko akirudi anatokewa na vituko.

"Kipindi kimoja nilimpeleka kuombewa, usiku niliona paka wengi ndani nilimolala wakaniparura huku mwanangu Upendo akinicheka," alidai.

Mama huyo ameomba watu wamsaidie ili mtoto huyo asiwe na vituko hivyo kwani hivi sasa baba wa mtoto amemkimbia na hana mawasiliano naye tena.

HAKIKA DUNIANI KUNA MAMBO

haiwezekani...that news would be all over place!!! Urban legend!!! somebody is tyring to make a name and hela... la sivyo ni jinn
 
That's why we are trying to confirm. You will be informed. This is not an era of darkness. Everything has to be empirically proved. This issue is being handled keenly.
 
Hiyo most likely ni uzushi wa mama wa mtoto, kama sivyo ana tatizo la akili na hizo ni hallucination zake! Hizo za Dr ku-confirm possibly ni uzushi vilevile, ukichaa sometimes uko infectious, hasa ukiwa unaamini mambo ya kishirikina.

Kuna uwezekano wa hayo yaliyo tokea, au ikawa ni mambo ya kuumua kwa maslahi binafsi. Ila tukumbuke shetani yupo, na kama biblia inavyo sema kwenye yoh 10:10, shetani yupo kwa ajili ya kuua na kuangamiza. kutokana na maelezo ya mama wa mtoto, huyo ni shetani wala si-nabii kwa sisi wakristo. mtoto na mama wanahitaji ukombozi wa yesu kristo, kwani shetani hujigeuza wakati mwingine kuwa kama malaika wa nuru.shetani kazi yake ni kuleta vitisho, woga hofu. ila Mungu wetu ni Mungu wa amani.
 
Mungu ana mabo mengi na tusipende kubisha mambo tusiyoyajua inawezekana ni kweli kabisa huyo mtoto anaongea kwani kuna watu wameshudia hayo. acha wafu wazike wafu wao.
 
That's why we are trying to confirm. You will be informed. This is not an era of darkness. Everything has to be empirically proved. This issue is being handled keenly.

Kwa kweli...I do not know what can convince me about such stuff. In this era of graphic design and photo shop I cannot believe it until i witness it... kwa macho.
At this rate I doubt that i will witness it and by the grace of God i do not want to witness the handiwork of the devil.

Sensationalism tu! make news and most possibly get some money out of it.

Yeah, mkuu I'm a sceptic. ( a good example ni kama wale wahubiri wa kufanya miracles that cannot be medically proven or be substantiated...kila leo mpofu kaona, mara sijui a born cripple katembea...yaani it's alot of unbelievable stuff, binadamu wako so destitute wanatafuta cheap thrills...la sivyo the serpent is busy, very very busy and we need to be very afraid and look to the Almighty God.)
 
Last edited:
Baada ya kuona wengi wanadhani mimi Bubu natafuta umaarufu wa kuiweka habari hii hapa kumbe siyo nimeona bora niweke kink waweze kusoma wenyewe toka gazeti la majira, haya akina Tomaso chukua....

Majira
 
Bubu,

Pamoja na kwamba hii habari iliandikwa kwenye Majira na magazeti mengine, ufuatiliaji uliofanywa na watu wanaoishi Muheza umeonesha pasi na shaka kwamba hakuna mtoto wa namna hiyo. Kama nilivyoahidi, niliwaomba jamaa zangu zaidi ya watatu wanaoishi Muheza wanisaidie kumtafuta hadi wamwone huyo mtoto. Wote wamesema kuwa hakuna mtoto wa namna hiyo. Sina shaka hii hadithi ni kama ile ya Mama Mchawi aliyekamatwa Dar kumbe ni usanii na wizi mtupu!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom