Mtoto wa miezi minne anatakiwa anywe kiasi gani cha maziwa ya mama?

victory02

JF-Expert Member
Nov 18, 2015
1,146
1,548
Wakuu, mtoto wa miezi minne anatakiwa anywe at least kiasi gani cha ujazo wa maziwa ya mama kuanzia saa moja asubuhi hadi saa tisa mchana. Tunatumia chuchu za watoto
 
Anywe akitosheka, Unamuondelea ziwa.

Mkuu dogo hapendi chuchu(chupa ya maziwa) kabisa,ila kwa mama yake ananyonya fresh tu. Tatizo mama akienda kazini,dogo anakunywa kwa mbinde sana ndiyo maana nilitaka kujua wastani anaotakiwa kunywa tusije kumpa chini ya kiwango
 
Wakuu, mtoto wa miezi minne anatakiwa anywe at least kiasi gani cha ujazo wa maziwa ya mama kuanzia saa moja asubuhi hadi saa tisa mchana. Tunatumia chuchu za watoto
Kwanini utumie chuchu za watoto, mama mtu kazi yake ni nini kwa mtoto mimi nafaham mtoto anatakiwa anyonye angalau kwa miaka 2...enough.
 
Kwanini utumie chuchu za watoto, mama mtu kazi yake ni nini kwa mtoto mimi nafaham mtoto anatakiwa anyonye angalau kwa miaka 2...enough.

Mama mfanyakazi mkuu anatoka asubuhi anarudi mchana
 
Tatizo hapendi ile chuchu ya watoto ya maziwa,inabidi akabiwe na anakunywa kidogo sana
Huyo itakuwa mlichelewa kumuanzishia chuchu ilibidi aanze mapema hata kabla maternity haijakaribia kuisha...
Mnaweza kujaribu kumpa kwa kijiko kuna sehemu niliona wanatumia njia hii ikafanikiwa
Kuhusu kiasi sina uhakika
 
Shukrani mkuu,ni kweli tulichelewa kumuanzishia chuchu. Ngoja tujaribu hii ya kijiko,ila usafi unatakiwa kuwa wa hali ya juu sana sijui kama dada wa kazi ataweza
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom