Mtoto wa miezi 10 hakui wala hatambai

mabwiku

JF-Expert Member
Jun 7, 2015
447
389
Habari mkuu,

Nimebahatika kupata mtoto wa kike mrembo kweli kweli, lakini mpaka Sasa ana miezi 10 lkn ukimwangalia ni kama anamiezi 5.

Bado hajakaza kukaa vizuri, akikaa kwa muda anaanguka, hawezi kutambaa zaidi ya kukaa na kutambaa.

Nahitaji msaada wa kitaalamu ndugu zangu sababu hospital hawana majibu ya kueleweka.
 
Huyo mtoto atakua alipata matatizo wakati wa kuzaliwa inawezakua alipata Cerebral palsy (CP) Ambayo ndio imesababisha matokeo hayo ya ukuaji.

Jaribu kwenda hospitali ukaonane na daktari wa watoto kwa ajili ya uchunguzi ili aweze kupatiwa huduma stahiki pamoja na wataalamu wa viungo (physiotherapist).
 
Kama alizaliwa bila tatizo lolote
Hakuchelewa kulia
Hakusaidiwa kupumua wala kusumbuliwa na magonjwa katika huo mda

Na ananyonya vizurii muwaishe hospitali kwa uchunguzi zaidi
 
Kwani huko hospital walisemaje
Km huwaamini huko hospital una uhakika huku jf utapata majibu sahihi?
....ulichoambiwa na madaktari kifanyie kazi.
 
Back
Top Bottom