Mtoto wa miaka miwili amuua mama yake kwa bunduki..

STUNTER

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
13,077
17,208
Mvulana wa umri wa miaka miwili amempiga risasi na kumuua mamake kimakosa katika mji wa Milwaukee, Marekani.

Mtoto huyo alipata bunduki hiyo sehemu ya nyuma ya gari. Mwanamke huyo, Patrice Price, 26, alikuwa akiendesha gari la mpenzi wake ambaye ni mlinzi na ambaye alikuwa ameacha bunduki yake kwenye gari, babake Andre Price amesema.

Polisi wa Milwaukee wanasema mwanamke huyo alipigwa risasi moja kutoka nyuma akiendesha gari mapema Jumanne asubuhi. Mamake Price na mwanawe mwingine wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja walikuwa kwenye gari hilo wakati wa kutokea kwa kisa hicho.

Bw Price alisema ana binti mwingine mkubwa, lakini akasema Patrice alikuwa na bidii sana. “Sasa hayupo nasi tena. Inaniuma sana,” Bw Price aliambia kituo cha habari cha WISN, Milwaukee. Mwezi uliopita, mvulana wa umri wa miaka minne alimpiga risasi mamake Jamie Gilt katika jimbo la Florida
katika hali sawa. Bi Gilt alinusurika na majeraha.
 
Back
Top Bottom