Mtoto wa miaka minne aiba gari la mama yake aingia nalo mtaani

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,458
Mtoto 1.JPG

Mtoto mwenye umri wa miaka minne amenusurika kuumia baada ya kupata ajali ya gari alilokuwa akiendesha mtaani bila ruhusa kutoka kwa wazazi wake Nchini Uholanzi.

Polisi wa Kituo cha Utrecht wamesema mtoto huyo akikwangua gari hilo katika maeneo mawili ya kuegesha magari baada ya hapo akaondoka akilitelekeza huku akiwa peku.

Polisi wamesema, mtoto huyo alichukua funguo ya gari la mama, akaondoka nalo bila wazazi wake kujua. Polisi walipomkamata wakaenda naye kituoni, akajieleza, wakampa chokoleti kisha kumrudisha kwa mama yake ambaye hakuwa anajua mwanaye alipoelekea.

Alipoulizwa aliwezaje kuendesha gari akawaonesha alivyofanya kuanzia mwanzo ambapo alisema alikuwa akiona wazazi wake wanavyofanya. Wazazi wa mtoto huyo wameshauriwa kutoweka funguo za gari sehemu ya wazi.
mtoto2.JPG


Source: BBC
 
Huyu ingekuwa ni familia zetu za uswahilini,baada ya kurudishwa angekula bokora za kutosha mpaka akili ingemkaa vizuri...
Kweli, hapa jirani watoto 2 mmoja 3 years mwingine tuseme 2.5 years, walibeba mabegi yao ndani hamna kitu wakaja tuition yaani walichapwa we acha kabisa eti watapotea vile wametoka wenyewe.

Wazazi wengine wanatisha.

Huko mbele watoto wana akili kubwa.
 
Ulaya Ulaya tu kweli... wakati mimi mwanangu wa 4 yrs ndo anajifunza kuendesha baiskeli, Uholanzi kuna kitoto kinanyosha goti vizuri, kanakamatwa na polisi kanajieleza vizuri hadi kanapewa chokoleti na kurudishwa nyumbani salama salimini bin kuhakikishiwa usalama!
 
Back
Top Bottom