Mtoto wa miaka 8 apakwa chumvi makalioni na kupigwa kwa waya na Baba yake mzazi kwa tuhuma za kuiba 1,200

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mtoto mwenye umri wa miaka minane (jina linahifadhiwa) mkazi wa mtaa wa Mission jijini Mwanza anaugulia majeraha kwenye makalio baada ya kuchapwa kwa waya huku akiwa amepakwa chumvi kwa tuhuma za kuiba Sh1, 200.

Ukatili dhidi ya mtoto huyo anayesoma darasa la pili katika shule ya msingi Sahara jijini Mwanza unadaiwa kutendwa na baba yake mzazi.

Mwalimu wa darasa ndiye aliyebaini majeraha ya mtoto huyo kwenye makalio yote mawili baada ya kumtilia shaka kutokana na kuchechemea kila alipotembea.

Mwenyekiti wa mtaa wa Mission, Musa Fereji amesema baada ya kuhojiwa, mtoto huyo alieleza jinsi alivyopata majeraha hayo katika tukio lililotokea Februari Mosi, 2021.

“Baada ya kumpokea mtoto huyo ofisini alipoletwa na mwalimu wake, tulimhoji ndipo tukabaini kuwa majeraha hayo yalitokana na fimbo aliyochapwa na baba yake mzazi,” amesema Fereji

Akizungumza akiwa chini ya ulinzi, mama wa kambo wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina la Auliditensia Bwire amesema siku ya tukio, mume wake aliyemtaja kwa jina la Rahman Suleiman alimtuhumu mtoto wake kuiba Sh1, 200 ndipo alipoanza kumchapa huku akimpaka chumvi kwenye makalio.

“Mwanzoni alianza kumchapa akitumia fimbo ya mti lakini ulipokatika akaanza kumchapa kwa kutumia waya ambao naamini ndiyo umemsababishia mtoto madhara kutokana na ile chumvi aliyopakwa,” amesema Auliditensia

Baba mzazi anayetuhumiwa kutenda kosa hilo alitoroka muda mfupi kabla ya mgambo waliotumwa na uongozi wa mtaa kufika nyumbani kwake.

Mwalimu mkuu msaidizi shule ya msingi Shahara, Beata Lema amesema baada ya kumwona mtoto huyo akipata shida kunyanyua miguu wakati wa kutembea aliamua kumhoji ndipo akagundua ukatili huo na kutoa taarifa kwa uongozi wa mtaa.

Mhuduma wa afya ngazi ya jamii kata ya Pamba, Zabina Wandwi amewashauri wazazi na walezi kuepuka kutoa adhabu za kikatili kwa watoto kwa sababu licha ya kuwaathiri kimwili, pia huwasababishia madhara ya kisaikolojia.

Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro kuzungumzia tukio hilo zinaendelea.
 
Nilipokuwa mdogo niliwahi muibia bimkubwa shilling 200 aliyoweka mezani nikaenda kula chocolate na kuwatambia shule darasa la pili hio maana alikuwa ananipa shilingi 30 za kutumia shule nilikuwa sishibi na akasema haongezi.

Kimbembe niliporudi alijua nitandakiwa kweli kweli .

Asingenichapa Leo ningekuwa napiga watu roba za mbao na bisibisi au bunduki kabisa

Samaki mkunje angali mbichi
 
Mimi nilimuibia antie yangu shilingi 100,zilikuwa nyingi sana mezani kwake karibu na kitanda maana alikuwa akiuza pombe.

Kilichofanya anishtukie nilirudi home sina time na msosi kabisa,akaniita na kuniuliza wewe siku hizi unaniibia hela eh???mimi kimya.

wala hakunigusa,sikuwahi kuchukua tena.
 
Nilipokuwa mdogo niliwahi muibia bimkubwa shilling 200 aliyoweka mezani nikaenda kula chocolate na kuwatambia shule darasa la pili hio maana alikuwa ananipa shilingi 30 za kutumia shule nilikuwa sishibi na akasema haongezi.

Kimbembe niliporudi alijua nitandakiwa kweli kweli .

Asingenichapa Leo ningekuwa napiga watu roba za mbao na bisibisi au bunduki kabisa

Samaki mkunje angali mbichi
Una uhakika kama dogo kaiba iyo pesa?

Iyo pesa ni nyingi sana kwa umri wake angekuwa kachukua kweli wangemkuta nayo au watoto wenzie wangemuona nayo anatumia,

Na hata kama kachukua wewe unaona iyo adhabu aliyopewa ni sawa?
 
Wewe unao uhakika kuwa hajaiba ?

Unaishj nao nyumba moja
 
Ugumu wa maisha akamzaa stress

Stress akamzaa maamuzi ya ajabu

Maamuzi ya ajabu akamzaa majuto

Majuto akamzaa hasara.

Usitoe adhabu nzito kwa mtoto hata kama kakosea mwishowe utakunywa hasara.
 
Me nilimuibia bibi shilingi 10 za tano tano mbili miaka hiyo ya 97s
Aisee nilichezeq kipigo sana
Hatua ya mwisho bibi akachukua kisu ili anikate mdomo nikacholopoka nilikimbia mpaka kazini kwa mama
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom