Mtoto wa miaka 15 amuua mama yake kwa panga

Landala

JF-Expert Member
Dec 24, 2010
997
473
mtoto wa miaka 15 Frank Makombe anayesoma kidato cha kwanza huko mkoani Iringa amemuua mama yake kwa panga pale alipoenda kuamulia ugomvi kati ya baba na mama yake,siku ya tukio hilo baba yake alikuwa akimpiga mama yake na mtoto huyo alichoka na tabia hiyo ya baba yake akachukua panga kwa ajili ya kwenda kumpiga nalo baba yake ndipo alipotaka kumpiga baba yake akamgeuza mama yake na panga hilo kumpata mama yake kichwani na kutokwa na damu nyingi kisha kufariki,mtoto huyo amekamatwa na atafikishwa mahakamani siku yoyote lakini baba yake amekimbia.chanzo kipindi cha pata pata saa 1 ucku kupitia wapo radio.
 
duh....hongera dogo ulikua na Nia njema sana. Mungu atakupigania
 
Ugomvi unaamuliwa kwa panga!!! hapo majanga lazima yatokeee! rip our mama, sote tupo njia moja!
 
pole sana mama rip ivi kuna watu wanapigana mpaka siku hizi uyo baba inabidi atafutwe ndio muuaji halisi
 
rip mama inauma sana maskini chonde chonde wanaume tuache ubeberu kwa watu ambao ni pumziko letu.
 
Kumbe kuna familia ambazo ugomvi bado u!sasa huyo baba amekimbia,mtoto kakamatwa,mama kafa,familia haipo tena du kweli dunia ina yake!r.i.p our mama
 
pole sana mama rip ivi kuna watu wanapigana mpaka siku hizi uyo baba inabidi atafutwe ndio muuaji halisi

Acha kumhukumu huyo baba huwezi jua chanzo cha ugomvi wao! Sometimes wamama nao wakorofi na matatizo kibao; kwa walio kwenye ndoa wanalijua hilo.
 
Wanaume wote wenye ubeberu hebu mjifunze ktkt hili, maana asilimia kubwa inayo athirika na ubabe wenu ni watoto wadogo wasio kuwa na hatia, huyu motto hana hatia kabisa maana akili yake ilishaathirika kisaikolojia kwa matukio ya ugomvi wa baba na mama wa mara kwa mara.
 
Hili ni fundisho kubwa sana kwa wazazi kuwa mambo ya ugomvi yamepitwa na wakati tena mbele ya watoto. Mkiona maisha yenu ni ya ugomvi kila siku ni bora mpeane talaka ili watoto wawe na msimamo hata wa kuishi na mzazi mmoja pekee. So sad. Rest in peace mama ila mtoto alikuwa na lengo la kumuumiza baba maana alishawachosha kwa ugomvi. Jua ni jinsi gani watoto wetu wanaumia wakiona wazazi hawalewani. Wazazi wote na wale watarajiwa wanaosoma hapa hili ni fundisho tosha, tubadilike.
 
Back
Top Bottom