Mtoto wa Miaka 13 Amgonga na Kumuua Baba Yake Aliyekuwa Akimfundisha Kuendesha Gari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto wa Miaka 13 Amgonga na Kumuua Baba Yake Aliyekuwa Akimfundisha Kuendesha Gari

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Aug 23, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Saturday, August 22, 2009 8:33 AM
  Baba mmoja wa nchini Marekani ambaye alikuwa akimfundisha mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 13 kuendesha gari, amefariki baada ya mtoto wake kumgonga na alilokuwa akimfundishia. Mashahidi wa tukio lililotokea kwenye kitongoji cha Bronx jijini New York, Marekani walisema kwamba baba wa mtoto huyo aliyejulikana kama John Cedeno, 45, alikuwa akimfundisha mtoto wake mwenye umri wa miaka 13 jinsi ya kuendesha gari.

  Siku ya tukio baba huyo alimpa ruhusa mtoto wake alipaki gari lake na ndipo mtoto huyo alipomgonga na kumuua hapo hapo.

  Familia ya mzee huyo ilikuwa imetoka kwenye mgahawa mmoja wa vyakula vya kilatino wakati mtoto huyo alipomuomba baba yake alisogeze gari lake aina ya Porsche.

  Mtoto huyo alikaa kwenye usukani wakati baba yake akisimama pembeni ya mlango wa gari hilo ambao ulikuwa wazi.

  Mtoto huyo aliirudisha gari hiyo nyuma ghafla na mlango huo wa gari ulimgonga baba yake na kumminya kwenye mti.

  "Baba yake alitokwa na damu nyingi sana mdomoni" alisema shuhuda mmoja.

  Mtoto wake huku akiwa amepagawa alianza kulia huku akipiga kelele "Nimemuumiza, nimemuumiza" alisema shuhuda mwingine.

  Baba huyo alitangazwa amefariki hapo hapo kwenye eneo la tukio.

  "Huu ni mkasa wa kusikitisha, bila shaka mtoto huyu ataishi maisha yake yote akikumbuka kuwa amemuua baba yake" alisema mwanamke mmoja aliyekuwepo eneo la tukio.

  Vyanzo vya habari vilisema kwamba hakuna uwezekano wa mtoto huyo kushtakiwa. http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=2884290&&Cat=2
   
 2. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2009
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  So sad!
   
 3. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  It's a sad story indeed. You also have to feel sorry for the son who has to live the rest of his life knowing he killed his father and you also have to look at other members of the family who will look at the boy and remember that he killed their husband/father. May God grant them strength during what is surely a very traumatizing event.
   
Loading...