Mtoto wa kwanza Mzee Aboud Jumbe afariki ghalfa India

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
Inna Lilah Waina Ilaihi Rajiun, aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania, Mzee Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi, amefiwa na mwana wa kwanza kipenzi Dk. Suleiman Aboud Jumbe Mwinyi. Dk. Suleiman amefariki ghafla hotelini nchini India alikokwenda kumsindikiza baba yake kwa matibabu.
 
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116539
E-mail: press@ikulu.go.tz
Website: Mawasiliano Ikulu
Fax: 255-22-2113425

PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemtumia salamu za rambirambi aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania, Mzee Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi, kufuatia kifo cha ghafla cha mtoto wake, Dk. Suleiman Aboud Jumbe Mwinyi.

Dk. Suleiman Aboud Jumbe Mwinyi, mtoto wa kwanza wa Mheshimiwa Jumbe, alifariki dunia mchana wa juzi, Jumatatu, Novemba 29, 2010, katika Hoteli ya MDS Lodge iliyoko Sarita Vihar mjini New Delhi, India, ambako alikuwa amempeleka baba yake kwa ajili ya matibabu katika Hospitali ya Apollo.

Kwa mujibu wa habari kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini India, Dk. Suleiman A. Jumbe Mwinyi alikutwa na mauti chumbani mwa hoteli alimokuwa amefikia, na mwili wa daktari huyo utawasili Zanzibar kesho, Alhamisi, Desemba 2, 2010, kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia (ET) tayari kwa mazishi.

Katika salamu zake, Mheshimiwa Kikwete amemwambia Mheshimiwa Jumbe: “Nashindwa kuelezea kiasi cha majozi na huzuni niliopata baada ya kutaarifiwa kuhusu kifo cha ghafla cha mwanao, Dk. Suleiman Aboud Jumbe Mwinyi, na msiba huo mkubwa uliokufika”.

Ameongeza Rais Kikwete: “Napenda kutuma rambirambi za dhati ya moyo wangu kwako kufuatia msiba huu mkubwa. Napenda kukuthibitishia kuwa mimi na wenzangu katika Serikali tuko nawe katika msimba huu mkubwa na katika kipindi hiki kigumu na cha majonzi makubwa sana.”

Ameongeza Rais Kikwete: “Nakuomba pia kwa kupitia kwako uwasilishe salamu zangu za rambirambi na wenzangu katika Serikali kwa familia yako yote na kwa jamaa na marafiki ambao kwa namna moja ama nyingine wameguswa na msiba huu”.

Amemalizia: ”Tunajua kuwa mnapitia kipindi kigumu. Tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awapeni nguvu, subira na uvumilivu wa kubeba majonzi ya kipindi hiki kwa sababu yote ni mapenzi yake.”

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

01 Desemba, 2010
 
RIP mbona hatujajulishwa kusafirishwa kwa kiongozi huyu kwenda kwa matibabu India?
 
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116539
E-mail: press@ikulu.go.tz
Website: www.mawasilianoikulu.go.tz

Innalillah wainna ilyah Rajiuun.
Nilidhani serikali imekata mawasiliano na huyu bwana. Kuna haja pia ya kumfaham vyema huyu mzee Jumbe.
 
Unafiki tuu !! hii press release haiwezi kumsafisha Kikwete hata kidogo kwamba ni mtu mwema anayejali.

Anyway, pole Mzee JUmbe na familia. Wamekutelekeza.
RIP Dr. Suleiman
 
Mkuu hebu tufunulie pazia ya hilo neno lako kwenye bold hapo

Mungu awafariji wafiwa na kuwapa faraja ktk kipindi hiki kigumu kwao.
 
Pole sana Aboud Jumbe kwa msiba huu mkubwa uliokufikia ukiwa katika kipindi kigumu - ukiwa unaugua. Bwana alitoa na Bwana ametoa, jina lake lihimidiwe.
 
Unafiki wa hali ya juu. A Jumbe hakujiuzulu kwa mazuri i.e. alitoswa sasa courage ya serikali ambayo bado ni ya Chama Cha Majambazi kujipendekeza inatoka wapi? Huu ni mfano mojawapo wa kutumia pesa za walipa kodi vibaya.
 
RIP Dr. Suleiman

Poleni wafiwa Mwenyenzi Mungu awajalie faraja kuu wakati huu mgumu
 
Poleni wafiwa na Marafiki wa karibu wa Dr Suleiman Jumbe..hivi alikuwa ni Dr wa nini?...hakuna utafiti wowote juu ya kifo chake...?
 
Alikuwa daktari wa tiba ya binaadamu.

Pole kwa Familia ya Jumbe.

Mtoto wa kiume wa marehemu alifariki huko huko India kwa ajali ya pikipiki miaka 5 nyuma. Duuuh

*Jumbe anafanya safari za matibabu India mara kwa mara na hulipiwa na serikali
 
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116539
E-mail: press@ikulu.go.tz
Website: Mawasiliano Ikulu
Fax: 255-22-2113425

PRESIDENT'S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemtumia salamu za rambirambi aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania, Mzee Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi, kufuatia kifo cha ghafla cha mtoto wake, Dk. Suleiman Aboud Jumbe Mwinyi.

Dk. Suleiman Aboud Jumbe Mwinyi, mtoto wa kwanza wa Mheshimiwa Jumbe, alifariki dunia mchana wa juzi, Jumatatu, Novemba 29, 2010, katika Hoteli ya MDS Lodge iliyoko Sarita Vihar mjini New Delhi, India, ambako alikuwa amempeleka baba yake kwa ajili ya matibabu katika Hospitali ya Apollo.

Kwa mujibu wa habari kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini India, Dk. Suleiman A. Jumbe Mwinyi alikutwa na mauti chumbani mwa hoteli alimokuwa amefikia, na mwili wa daktari huyo utawasili Zanzibar kesho, Alhamisi, Desemba 2, 2010, kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia (ET) tayari kwa mazishi.

Katika salamu zake, Mheshimiwa Kikwete amemwambia Mheshimiwa Jumbe: "Nashindwa kuelezea kiasi cha majozi na huzuni niliopata baada ya kutaarifiwa kuhusu kifo cha ghafla cha mwanao, Dk. Suleiman Aboud Jumbe Mwinyi, na msiba huo mkubwa uliokufika".

Ameongeza Rais Kikwete: "Napenda kutuma rambirambi za dhati ya moyo wangu kwako kufuatia msiba huu mkubwa. Napenda kukuthibitishia kuwa mimi na wenzangu katika Serikali tuko nawe katika msimba huu mkubwa na katika kipindi hiki kigumu na cha majonzi makubwa sana."

Ameongeza Rais Kikwete: "Nakuomba pia kwa kupitia kwako uwasilishe salamu zangu za rambirambi na wenzangu katika Serikali kwa familia yako yote na kwa jamaa na marafiki ambao kwa namna moja ama nyingine wameguswa na msiba huu".

Amemalizia: "Tunajua kuwa mnapitia kipindi kigumu. Tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awapeni nguvu, subira na uvumilivu wa kubeba majonzi ya kipindi hiki kwa sababu yote ni mapenzi yake."

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

01 Desemba, 2010

Msimba???ndio nini ??hivi hii kurugenzi ya habari ina nini?yaani matangazo yakitoka hapo lazima yakosewe..Rweyemamu unasoma kweli matangazo haya au ndo vijana wanakuwa wanakulete samaki samaki pale unasoma huku unatiririsha mi taska ya baridi huoni errors??
 
Back
Top Bottom