Mtoto wa Kingunge kortini kwa wizi wa mil. 400/- | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto wa Kingunge kortini kwa wizi wa mil. 400/-

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Aug 18, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,499
  Likes Received: 5,727
  Trophy Points: 280
  Mtoto wa Kingunge kortini kwa wizi wa mil. 400/-


  na Happiness Katabazi


  [​IMG]
  MTOTO wa mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Kombale - Mwiru, Tony Mwiru (36), jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na makosa ya kula njama, kuwasilisha nyaraka za uongo, kughushi na kujipatia sh milioni 424 kwa njia ya udanganyifu.
  Mbele ya Hakimu Mkazi, Gabriel Milumbe, Mwendesha Mashitaka, Inspekta wa Polisi, Emma Mkonyi, alidai kuwa mshitakiwa huyo anakabiliwa na mashitaka manne.
  Shitaka la kwanza ni la kula njama ambapo yeye na wenzake ambao hawakuwepo mahakamani jana, waliwasilisha nyaraka za uongo katika Kampuni ya SCI (TZ) Ltd na kujipatia sh 424,488,799.29.
  Inspekta Mkonyi alidai shitaka la pili ni la kughushi. Katika shitaka hilo, Mwiru anadaiwa kughushi maombi ya ujumbe kasi wa kuamishia fedha wenye namba 17 wa Agosti 27 mwaka 2008, kwa nia ya kuonyesha ujumbe huo ni halali na ulitolewa na Savishankar Resman ambaye ni Mkurugenzi wa SCI (TZ), Ltd wakati si kweli.
  Aidha, alidai shitaka la tatu ni la kuwasilisha nyaraka za uongo. Inadaiwa kuwa Agosti 29, mwaka 2008 katika Benki ya Barclays (TZ), iliyopo Mtaa wa Ohio jijini, mshitakiwa aliwasilisha nyaraka za uongo ambazo ni fomu ya maombi ya ujumbe kasi yenye namba E7 kwa mfanyakazi wa benki hiyo, Bitun Chiza.
  Shitaka la nne ni la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, ambapo inadaiwa kuwa Oktoba 9, mwaka 2008, katika Benki ya CRDB, Tawi la Kijitonyoma, alijipatia kiasi hicho kupitia akaunti namba 01j014293000, akionyesha Kampuni ya SCI (TZ), Ltd imeidhinisha ilipe kiasi hicho cha fedha kwa kampuni ya Temm Power Ltd.
  Hata hivyo mshitakiwa alikana mashitaka yote na Inspekta Mkonyi alidai upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kuomba tarehe ya kutajwa.
  Baada ya kumaliza kusikiliza mashitaka hayo, Hakimu Milumbe alimuuliza mshitakiwa kama mzee Kingunge Ngombale - Mwiru ni baba yake, naye alijibu kuwa ndiyo. “Ujue baba yako tunamheshimu sana, sasa kwanini wewe mtoto wake unajihusisha na mambo kama haya?” alihoji Hakimu Milumbe. Mshitakiwa huyo amerejeshwa mahabusu baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
   
 2. Kamaka

  Kamaka JF-Expert Member

  #2
  Aug 18, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 565
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Bado wazazi wao wanashika tu watoto
   
 3. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #3
  Aug 18, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ndio maana akina Kingunge hawataki kujiuziulu,maana wanalinda majanga kama haya.
  Je Msekwa alishalipa deni lake Foreign Affairs kwa matibabu ya mwanae?
   
 4. JAYJAY

  JAYJAY JF-Expert Member

  #4
  Aug 20, 2010
  Joined: Oct 31, 2008
  Messages: 2,495
  Likes Received: 824
  Trophy Points: 280
  nashangaa kwenye mahojiano yaliyonukuliwa na gaxeti la Mwananchi, hakimu anamuuliza mshtakiwa ''wewe ni kijana wa K.N Mwiru''?.sijui alikuwa anataka kujua hilo kwa nini. au ndio yale mambo ya kubebana?
   
Loading...