Mtoto wa kike huitwa "BINTI" wa kiume anaitwaje?

Wakike ni "binti" wa kiune ni "bin/ibun/ibn"

Even a black folk hate to see another nigga made it..
 
Bin au Ibn na Bint ni maneno yanayotokana na lugha ya Kiarabu, mnatakiwa kuwa makini na jinsi mnavyotaka kuyatumia.
Tukubaliane kuwa kiswahili kimetohoa maneno mengi toka kiarabu. Tunadai siku zote kuwa kiswahili ni kibantu lakini bado kuna ule uarabu ndani ambao utatufanya baadaye kiswahili kiitwe kreori sababu maneno mengi tumetohoa. Basi tungechukua kwenye makabila yetu sema kuwa msichana utamuita kigori wangu na mvulana utamuita morani wangu au kabila lolote otherwise tukubali tulishakubali kamusi ya kiswahili ambayo imeandaliwa na watu wa pwani ndo official tusipinge. Juma bin Kiute au Jamila binti mafuta.
 
Ama kweli anaitwa "njemba "sina jibu o level nilipata zero kiswahili. Nasubiri wataalamu waje. Watoto wadogo wanatuuliza maswali ya msingi hatuna majibu. Akikuuliza kwa nini jua linaning'inia angani lisianguke utamjibuje mpaka akuelewe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tukubali ukweli kwamba mtoto wa kiume ni mvulana na wa kike ni msichana.lakini unapotaka kuwatambulisha kwa nasaba iwe mtu mzima wa jinsi a ya kike au kiume ndo maneno binti au bin yanapotumika.. mwana=mtoto wa fulani
 
Tukubali ukweli kwamba mtoto wa kiume ni mvulana na wa kike ni msichana.lakini unapotaka kuwatambulisha kwa nasaba iwe mtu mzima wa jinsi a ya kike au kiume ndo maneno binti au bin yanapotumika.. mwana=mtoto wa fulani
Sawa sawa kabisa , niongezee kidogo
Bin ni kiunganishi cha uzawa wa mwanaume kwa maana ya Juma Bin Hussein ikimaanisha Juma aliyezaliwa na Hussein. Asaha binti Maftaha kwa maana hiyo hiyo lakini kikeni

Mtoto anazaliwa kama mtoto wa kiume kwa maana yake na wa kike vivyo hivyo
Wanapoelekea umri wa balegheh au kuvunja ungo wanaitwa Wavulana au Wasichana

Katika umri wa balegheh na ungo huitwa Kijana na Binti
Ndiyo maana utasikia Kijana wa Katavi kamdunga mimba binti Mbonde

Baada ya umri wa kuzaa hadhi zao hubadilika na kuwa mwanaume na Mwanamke
Utasikia mwamaume huyu mkware au mwanamke yule mwingi, ushamfaham eeh

Ukienda Ushirombo au Machame kidogo utatatizika. Unaweza kusikia 'kuna mwanamke kapita hapa amebebe mwanaume' kwa maana ya mwanamke kabeba mtoto wa kiume
Kule hakuna category ni mwanaume na mwanamke! period
 
Back
Top Bottom