Mtoto wa kike huitwa "BINTI" wa kiume anaitwaje?

Naomba kuondolewa ujinga, nimeulizwa na mtoto mdogo anayesoma darasa la tatu nimeshindwa kumjibu na kuishia kumpigia stori nyingine ili asahau swali lake, lakini kamekomaa kila muda kananikumbusha.....sijui nani amekatuma!! Msaada tafadhali...

Inategemea na muktadha wenyewe na unakusudia kusema kitu gani. Kama kwa mfano unaongea na rafiki yako na unataka kumpa taarifa kuwa mwanao mgonjwa; unaweza kusema hivi:
- Kijana wangu ana homa
- Binti yangu ana homa
 
Bin au Ibn na Bint ni maneno yanayotokana na lugha ya Kiarabu, mnatakiwa kuwa makini na jinsi mnavyotaka kuyatumia.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Bin au Ibn na Bint ni maneno yanayotokana na lugha ya Kiarabu, mnatakiwa kuwa makini na jinsi mnavyotaka kuyatumia.
Ni kweli mkuu, lakini pamoja na maneno kama hayo kutokana na kiarabu lakini kiswahili kimeyabadilisha na kuna uwezekano yakawa yanabeba maana tofauti kabisa na ilivyo kwa kiarabu. Sasa kwa wazungumzaji wa kiswahili wa sasa neno 'binti' lina maana ya 'mtoto wa kike'....ama siyo?
 
Na kwa Kiarabu maana yake ni hiyo hiyo.... Ni matumizi tu.
 
Nahisi jibu la swali halijapatikana Binti= msichana = mwanamke = mama = bibi
KIVUMBI tunataka kujuzwa ........= mvulana = mwanamme = baba = babu
Mtazamo tu wandugu tujuzeni
 
Nahisi jibu la swali halijapatikana Binti= msichana = mwanamke = mama = bibi
KIVUMBI tunataka kujuzwa ........= mvulana = mwanamme = baba = babu
Mtazamo tu wandugu tujuzeni
soma kuanzia mwanzo utaona jibu.
 
Hata wa kike nae anaitwa kijana....
nikweli, lakini kuna nyakati linatumika kuashiria mtoto wa kiume. Ni kama neno 'mzee' mfano linapotangulia jina. Hata katika familia mara nyingi baba ndio anaitwa 'mzee'.
 
Mkuu wacha na mimi nidandie hapo hapo:Dume la Ng'ombe huitwa FahariDume la Mbuzi huitwa BeberuDume la Kuku huitwa JogooJe dume la mbwa huitwaje?Nawasilisha wakuu.
Bila shaka dume la paka wafaham linaitwaje! Naomba unijuze mwanajamii.....!
 
Back
Top Bottom