Mtoto wa Kigogo Serikalini ahusishwa na mgomo wa uuzaji wa Mafuta

Patriote

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
1,718
1,047
KUKOSEKANA kwa mafuta ya petroli jana kulizua tafrani kubwa kwa wakazi wa Jiji la Dar es alaam baada ya vituo vingi vinavyouza nishati hiyo kugoma kutoa huduma hiyo. Misururu mingi ya magari hasa madogo ilionekana kila kona ya jiji, huku ikituhumiwa kuwa wamiliki wa vituo vya mafuta walikuwa wakitii agizo la mtoto wa kigogo mmoja wa serikali ambaye anadaiwa kuwashawishi baadhi ya wafanyabiashara kusitisha uuuzaji wa nishati hiyo, kama njia ya kupinga bei mpya ya kikomo iliyotangazwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).

Inadaiwa kwamba mtoto huyo wa kigogo ana uhusiano mkubwa na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wa mafuta, na inadaiwa pia kuwa ana hisa katika baadhi ya makampuni. Vituo vingi juzi na jana vilikuwa vikiuza dizeli na mafuta ya taa tu, huku vikidai kutokuwa na mafuta ya petroli kwa madai ya kuishiwa.

Hata hivyo, EWURA imetishia kuvichukulia hatua kali vituo vya mafuta vitakavyobainika kugoma kuuza nishati hiyo, na kudai kuwa ndio pekee wanaoweza kutamka kukosekana kwa mafuta, hivyo basi hakuna haja kwa umma kupata hofu na kuanza kujazana kwenye vituo vya mafuta kujaza mafuta zaidi, kwani kwa kufanya hivyo, kunaharibu mfumo mzima wa usambazaji wa mafuta.

Tanzania Daima 20/12/2011

Maoni yangu

Hatukatazi mtoto/ndugu/jamaa wa kigogo yeyote serikalini kufanya biashara, hasa biashara halali, ila utata unajitokeza pale tu ambapo mtoto/ndugu/jamaa ya kiongozi yeyote awaye nchini anayetumia influence/wadhifa wa mzazi/ndugu yake kutusumbua /kutunyonya/kutuibia. Ikifikia point hiyo ya mtu kutumia wadhifa wa mzazi wake kuinyonya nchi, ndipo wanawanchi huanza kuchoka na hata kuanziasha chuki dhidi ya watu hawa. Wahenga walisema ukila na kipofu usimshike mkono, ila kwa staili hii naona wameamua kukamata kabisa mkono wa kipofu usiingizwe tena kwenye bakuli. Ole wenu mnaotufanyia mchezo huu, naimani ipo siku tutaamua kuharibu hizo biashara zinazowapa jeuri hii ya kifisadi. Kwanza mitaji ya biashara hizo most likely mmetuibia, pili biashara hizo mnaendesha kwa magumashi so hatutasita kuziharibu mana zinatokana na fedha za kifisadi mnazotuibia kila kukicha. Hivyo ni vyema mkajua kuwa tunafahamu A to Z kuhusu mnayoyafanya na hivyo ni vyema muoperate in low profile.
 
Nchi ya tuhuma juu ya tuhuma na tetesi... na tunajidanganya kuwa tupata maendeleo...
 
Tuhuma hizi ndizo zenye uhusiano wa moja kwa moja wa sisi kutokuwa na maendeleo, hivyo tunaimani kuwa nchi ikiwa free from tuhuma za ufisadi n.k, maendeleo ni lazima. Ni jukumu letu wanawanchi, kupambana na haya majizi ili nchi yetu ipate maendeleo ya kweli badala ya haya tunayoambiwa sasa kwenye makaratasi na viongozi wetu kuwa Msongamano wa magari na traffic jam ni maendeleo.
 
hivi hii nchi imefikia watoto wa vigogo kutuumiza sisi watanzania tulio wengi na bado tumekaa kimya,jamani ipo siku hawa watoto wa vigogo tunaowaita watatuingiza majiti sehemu furani,tumekuwa wapore sana

\Nawapenda walibya wamewafanyia mbaya hao wanaojiita watoto wa vigogo
 
mimi hapa ndio niliwashawishi.
na baba yangu si kigogo wala nini,mpaka mueleze kwa nini mlipunguza kura za chama changu kutoka 81%hadi 61%.
mtuahidi 2015 kama mtatupa 95% tuwapunguzie maumivu.
 
Ni ugomvi wa JAIRO na MASEBU:

Fact: Jairo alikuwa ana mpago wa KUIFUTA EWURA kama angeendelea kuwa PS wa Wizara na kuunda chombo chenye "MENO"! EWURA hawana "MENO" zaidi ya blah blah na kujilipa POSHO za vikao TU! kwa lugha rahisi EWURA hawana KAZI wanayoifanya zaidi ya "kuongea na waandishi wa habari"!

JAIRO bado anaendesha ile WIZARA remotely na kwa usaidizai wa Mkuu wa Kaya, na kwahiyo, wafanyabiashara wa mafuta wanapewa "kichwa" na Wakuu ili ku-sabotage MASEBU and Co!
 
Kazi ipo, kama watu wanajadili suala muhimu hivi kwa uchumi wa taifa na wengine mnakejeli Mungu atunusuru.
 
Hawa wazazi wao ndio wezi wa Taifa letu ndo mana unaona wanaleta mzaha kwenye mambo ya maana.
 
KUKOSEKANA kwa mafuta ya petroli jana kulizua tafrani kubwa kwa wakazi wa Jiji la Dar es alaam baada ya vituo vingi vinavyouza nishati hiyo kugoma kutoa huduma hiyo. Misururu mingi ya magari hasa madogo ilionekana kila kona ya jiji, huku ikituhumiwa kuwa wamiliki wa vituo vya mafuta walikuwa wakitii agizo la mtoto wa kigogo mmoja wa serikali ambaye anadaiwa kuwashawishi baadhi ya wafanyabiashara kusitisha uuuzaji wa nishati hiyo, kama njia ya kupinga bei mpya ya kikomo iliyotangazwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).

Inadaiwa kwamba mtoto huyo wa kigogo ana uhusiano mkubwa na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wa mafuta, na inadaiwa pia kuwa ana hisa katika baadhi ya makampuni. Vituo vingi juzi na jana vilikuwa vikiuza dizeli na mafuta ya taa tu, huku vikidai kutokuwa na mafuta ya petroli kwa madai ya kuishiwa.

Hata hivyo, EWURA imetishia kuvichukulia hatua kali vituo vya mafuta vitakavyobainika kugoma kuuza nishati hiyo, na kudai kuwa ndio pekee wanaoweza kutamka kukosekana kwa mafuta, hivyo basi hakuna haja kwa umma kupata hofu na kuanza kujazana kwenye vituo vya mafuta kujaza mafuta zaidi, kwani kwa kufanya hivyo, kunaharibu mfumo mzima wa usambazaji wa mafuta.

Tanzania Daima 20/12/2011

Maoni yangu

Hatukatazi mtoto/ndugu/jamaa wa kigogo yeyote serikalini kufanya biashara, hasa biashara halali, ila utata unajitokeza pale tu ambapo mtoto/ndugu/jamaa ya kiongozi yeyote awaye nchini anayetumia influence/wadhifa wa mzazi/ndugu yake kutusumbua /kutunyonya/kutuibia. Ikifikia point hiyo ya mtu kutumia wadhifa wa mzazi wake kuinyonya nchi, ndipo wanawanchi huanza kuchoka na hata kuanziasha chuki dhidi ya watu hawa. Wahenga walisema ukila na kipofu usimshike mkono, ila kwa staili hii naona wameamua kukamata kabisa mkono wa kipofu usiingizwe tena kwenye bakuli. Ole wenu mnaotufanyia mchezo huu, naimani ipo siku tutaamua kuharibu hizo biashara zinazowapa jeuri hii ya kifisadi. Kwanza mitaji ya biashara hizo most likely mmetuibia, pili biashara hizo mnaendesha kwa magumashi so hatutasita kuziharibu mana zinatokana na fedha za kifisadi mnazotuibia kila kukicha. Hivyo ni vyema mkajua kuwa tunafahamu A to Z kuhusu mnayoyafanya na hivyo ni vyema muoperate in low profile.

Huyu dogo anakiburi sana,nasikia ameagiza mabasi china na anataka ya operate arusha dar na ameshaanza kumeletea zengwe Dar expree sababu ndio amekamata hiyo njia! Si hayo tu,ana kiburi flani hivi cha kifisadi hata ndani ya chama kuna mambo anayaendesha yeye kama yeye na kwa kufuata katiba ya chama! Mimi nadhani bora tupange tufanye nini kwa sababu hii hali hata mimi imenichosha ni mwaka mmoja tu atamaliza miaka minne huyu baba kama mwana nae anakuja na vituko vya aina hii? Hawajifunzi kutoka kwa watoto wengine wa viongozi? Hii ni shida
 
Kumbe tatizo ni huyu young bilionea! Siku babako akiachia ngazi tafuta pakwenda.
 
Shida yetu ni maneno mengi pasipo kuchukua hatua. Ifike mahali tuanze kuchukua hatua maana bila hivyo hatuendi kokote!
 
Ni ugomvi wa JAIRO na MASEBU:

Fact: Jairo alikuwa ana mpago wa KUIFUTA EWURA kama angeendelea kuwa PS wa Wizara na kuunda chombo chenye "MENO"! EWURA hawana "MENO" zaidi ya blah blah na kujilipa POSHO za vikao TU! kwa lugha rahisi EWURA hawana KAZI wanayoifanya zaidi ya "kuongea na waandishi wa habari"!

JAIRO bado anaendesha ile WIZARA remotely na kwa usaidizai wa Mkuu wa Kaya, na kwahiyo, wafanyabiashara wa mafuta wanapewa "kichwa" na Wakuu ili ku-sabotage MASEBU and Co!

Kilichotakiwa ni walaji/watumiaji wa hiyo nishati ndio wangeunda regulatory board badala serikali maana watoa maamuzi hawawezi hata siku moja kumkana au kumtendea kinyume mwajili wake,mfano imekataliwa upandishaji wa bei ya umeme lakini hao waliongoza mjadala ambao ndio wangalizi wanahangaika na lugha ya kuwadanganya Wadanganyika eti wanachi wa kawaida hawataumizwa na ongezeko hilo sasa huu si uhuni? serikali inaingia gharama kubwa kuhakikisha umeme unapatikana wakurejesha hizo gharama ni mtumiaji ambaye ni wewe na mimi unafikiri bei haitapanda, itapanda tu tutake tusitake.
 
Kwa akili za kawaida ambazo Ritz 1 najua anazo, hawezi akafanya hayo anayoshutumiwa kwa kuwa kitendo hicho kinayumbisha utawala wa faza ambapo kamwe asingependa!
 
Back
Top Bottom