Mtoto wa Kigogo ahonga sh.40m/= na kukabidhiwa Faili la Ugonjwa wa Mwakyembe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto wa Kigogo ahonga sh.40m/= na kukabidhiwa Faili la Ugonjwa wa Mwakyembe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kalengamab, Feb 1, 2012.

 1. k

  kalengamab Member

  #1
  Feb 1, 2012
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mtoto mmoja wa kigogo anayetamba kwa utajiri nchini amefanikiwa kupata faili la ugonjwa unaomsumbua Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe kwa kuwahonga maafisa wa Wizara ya Afya sh. mil. 40/= na sasa anafikiria kuichapisha kwenye moja ya magazeti yanayomilikiwa na tajiri mmoja nchini ili kuthibitisha kama mwanasiasa huyo alipewa sumu au la.

  Ingawa hatua hiyo si salama sana kwa mtoto huyo wa kigogo na wenzake kwa maana ya kuwa taarifa hiyo inaweza kuwa ni interim au ya mpito maana Mwakyembe bado anatibiwa na yuko chini ya uangalizi wa madaktari wa Apollo, au inaweza kuwa "imemtengenezwa" , hivyo ni feki au imechakachuliwa, lengo lake kuu ni kumyamazisha Waziri Sitta, angalau kwa muda, asipige kelele sana kuwa Mwakyembe alilishwa sumu.

  Pamoja na kwamba mtoto huyo wa kigogo anadai kuwa baba yake hana mkono kwenye ugonjwa wa Mwakyembe, anapata kigugumizi kikubwa kuelezea kwa nini atoe fedha zote hizo kupata taarifa ya ugonjwa wa Mwakyembe na kwa nini ni wao tu wanaoweweseka Sitta anaposema Mwakyembe alilishwa sumu.

  Kuanzia jana mtoto huyo wa kigogo amekuwa na majadiliano ya kina gazeti la Mtanzania ili taarifa hiyo iweze kuchapishwa kwenye magazeti ya kesho ingawa zipo tetesi kuwa Mtanzania wana wasiwasi mkubwa na hatua hiyo ambayo inaweza ikazaa kesi mahakamani kwa kuchapisha taarifa ya siri kati ya mgonjwa na daktari wake na vilevile kukiuka haki ya faragha ya kikatiba.

  Hongo hiyo ya mil. 40/= ilichangamkiwa na wafanyakazi wa Wizara ya Afya mapema wiki hii ambao waliweza kukwapua taarifa hiyo kutoka kwenye Ofisi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Blandina Nyoni. Tatizo linalomsumbua mtoto huyo wa kigogo ni uhalisia wa taarifa yenyewe maana Wabongo hawaaminiki sana. Lakini baba yake anataka ichapishwe kwa udi na uvumba; kama yatajitokeza matatizo, watapambana nayo mbele ya safari.

  Kwa kuwa suala hili limeshavuja kwa kiasi, huenda Dk. Mwakyembe mwenyewe ana taarifa za suala hili. Lakini ni vigumu kumwingiza kwenye mazungumzo hayo. Leo ameonekana ofisini kwake na wanasheria wawili maarufu jijini, pengine wameenda kumjulia hali au kwa majadiliano kuhusu suala hili au masuala mengine.
   
 2. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #2
  Feb 1, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  walahi wasipochapisha kesho basi tutamwaga hapa jf......
   
 3. L

  LAT JF-Expert Member

  #3
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  dahhhh, jioni ifike nikagide ugimbi
   
 4. K

  Kapela Msonda Member

  #4
  Feb 1, 2012
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 39
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nilitaka kuuliza nani huyo mtoto wa kigogo mwenye ukwasi? Ah, naelewa, lazima ni manywele Jr.
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  Feb 1, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hadith hizi za alfu lela ulela
   
 6. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #6
  Feb 1, 2012
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kama ipo si iwekwe hapa JF
  acheni kusubiria magazeti, magazeti yachukue kutoka hapa
  acheni story, kama ipo, wekeni hapa twende kazi
   
 7. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #7
  Feb 1, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  mtoto wa lowassa?
   
 8. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #8
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,659
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Ndiyoooooooooooooooooo.
   
 9. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #9
  Feb 1, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Cha ajabu mgonjwa pia hataki kuweka wazi once and for all; ametoa tu kama heading details hataki, sasa TZ tutafanyaje???
   
 10. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #10
  Feb 1, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 0
  We jamaa umeshindwa kuitunga hii story unajikanyaga kanyaga mno.
   
 11. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #11
  Feb 1, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,407
  Trophy Points: 280
  Ukifuatilia haya maelezo ni wazi anamzungumzia Fred Lowassa
   
 12. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #12
  Feb 1, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  tusububiri kama kweli ni udaku au la?LAKINI YOTE YANAWEZEKANA MBELE YA PESA
   
 13. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #13
  Feb 1, 2012
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hii taarifa ina ukweli fulani. Akina MAMVI ambao wamekuwa wakituhumiwa kumpa sumu Mwakyembe wanahaha sana kuupotosha umma kwa kutoa taarifa ya awali kuhusu ugonjwa wake ambayo haizungumziii suala la sumu. Hivi sasa wanashauriana na wahariri waliowanunua ili waone ni jinsi gani wanaweza kuchapa taarifa hiyo bila kuleta zozote. Si mnajua tena, the guilty are afraid!
   
 14. L

  LISAH Senior Member

  #14
  Feb 1, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 108
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwani huyo motto wa kigogo anawasiwasi gani?
  au ni mmoja wa wanao dhaniwa wametenda uovu huo?
   
 15. n

  nyantella JF-Expert Member

  #15
  Feb 1, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Rev. Mi nafikiri huyu jamaa ndiye anayo hiyo report maana details zoote hizo kazipata wapi? kama anayo amwage tu jamvini tuione or zitakua hadithi za alfu lela ulela kweli!
   
 16. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #16
  Feb 1, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Mnaohisi ni mtoto wa LOWASSA semeni NDIOOOOOO na msiomuhisi kuwa ni yeye waseme SIOOOOOO
   
 17. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #17
  Feb 1, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  acha dharau
   
 18. Ngararimu

  Ngararimu Senior Member

  #18
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  mimi nashauri muhusika kama yupo humu jamvini aiweke habari hiyo humu sasa hivi na kwa kuwa humu hatujuani kwa uhakika basi sourse ya habari iwe ni JFna aichape kwenye magazeti kesho ili iwafikie hata wananchi wengine ambao siyo member humu na kwa njia hiyo atakuwa ameepuka hata hatua za kimahakama ambazo zinaweza kujitokeza kama habari hii mchapa gazeti ataitoa kavum kavu maana itabidi aieleze mahakama sourse ya hiyo habari - HUU NI USHAURI WANGU WA BUUURE bila senti moja
   
 19. N

  Nyampedawa Member

  #19
  Feb 1, 2012
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hapo kwenye red ni kweli kabisa MzeePunch. Naona uliwahi kusoma novel ya James Hardley Chase "the guilty are always afraid"
   
 20. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #20
  Feb 1, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,953
  Likes Received: 1,509
  Trophy Points: 280
  Du na walipe sumu na hilo faili bana,kwa zama hizi kuchukua hilo faili haisadii sana sana wananunua kesi kwa kutoa siri za mgonjwa bila idhini yake,anyway lakini si wana hela za bure hawajui pa kuzipeleka,oh nilisahau wanazipeleka kwenye harambee makanisani
   
Loading...