Je, Mtoto wa kambo ana haki ya kurithi mali?

Hivi siku hizi akili zinauzwa ghali sana kiasi kwamba wengine tunashindwa kununua? Mbona majibu yako wazi?!!! Mtoto wa kambo anamrithi MAMA YAKE MZAZI na sio baba wa kambo. Sehemu ya urithi atakayopata mama ndiyo atamgawia mwanaye huyo. Hauzuwii kumpa kama wosia na sio mirathi! Pili mama hana ushirika kwa vitu alivyovikuta! Hata ulivyopata akiwepo mchango wake lazima uwe calculated! HAKUNA AUTOMATIC 50-50! Usiogope kwenda mahakamani hiyo ndio sheria. Tafuta family lawyer mzuri ulinde haki zako!
Mama anapewa urithi gani hapa kama sio urithi wa watoto??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna sehemu nimekataa mkuu, Mimi siifahamu sheria vizuri so kama ipo hivyo mimi ni nani nipinge? Sheria ifuatwe sina tatizo
Demi Sheria zipo kabisa mali zinabaki kwa Mke mpaka atakapofariki na yeye ndipo watoto wanachuku.

Ipo Sheria ya kugawana mali mlizochuma km mtatengana ni pasu kwa pasu km nyumba ni 2 tangu akuoe Moj mke nyingine Mume Mahakama ikiona watoto ni wadogo watabaki kwa Mama hadi wakikua au mali isigawiwe iandikwe ya watoto na Mama akish mojawapo.
TATIZO linapokuja.

Kiuhalisia Mwaamke, Mke akirithi mali za mf Masanja na ana watoto 3 wa marehemu na mmoja kaja naye halafu amemaliza EDA anataka aolewe na Mrema ina maana Mali za Masanja zitasimamiwa na Mrema na hakuna Masanja kusogea

MADA
Huyo mtoto wa nje baba yake bado yupo, ameshamtambua sasa akadai urithi huko na hata Baba wa kambo akifa sidai chochote akapambane na wenzie ,si kawatafuta
 
Najibu hapo mwisho kwenye mchango wa mwanamke. Mke wako ana haki na mali zako hata kama amezikuta.. mchango wake sio lazima uwe pesa..Kama anatekeleza majukumu ya kulea familia na kukutunza huo ni mchango tosha. Haki anayo kama hajakiuka mambo mengine ya mahusiano yenu.
Kuhusu mtoto wa kambo subiri wanasheria wabobezi waje. Ila mtoto kufahamu baba yake mzazi ni Jambo la kheri..sema bidada kakiuka makubaliano yenu.
Binafsi niliolewa nikiwa nina mtoto. Mume akanipa masharti kama hayo nikaona poa tu maana baba mtoto hakuwa responsible kwa mwanae. Na jina akataka nimbadilishe atumie la kwake nikakubali lakini kishingo upande.
Miaka inasonga sioni akitekeleza majukumu kwa mtoto ipasavyo..hata ukaribu wa baba na mtoto hakuna, anatoa matunzo kwa kujivuta vuta as if sio mwanae vile. Uzuri ni kwamba mie sio mlalamishi naridhika na chochote kidogo ila ikawa inaniuma sioni kama mtoto anatunzwa ipasavyo na uwezo anao mkubwa tu. Napambana mwenyewe kila siku ninastress za matunzo.
Nikaona isiwe taabu.. nikamrudishia jina lake la awali..nikamtafuta baba yake na shangazi zake nikawakutanisha na mtoto wao. Maana niliona nampeleka mtoto kwenye ukoo ambao ipo wazi kabisa hawamchukulii uzito, why nimpe jina lao?Now nina amani moyoni!

Kama jamaa angelibeba jukumu ipasavyo nisingefanya hivyo. Na mbaya zaidi mtoto alianza kumuulizia baba yake mzazi..loh nikasema isije niletea matatizo makubwa baadae.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hio baba yake kawa responsible?
 
Demi Sheria zipo kabisa mali zinabaki kwa Mke mpaka atakapofariki na yeye ndipo watoto wanachuku
Ipo Sheria ya kugawana mali mlizochuma km mtatengana ni pasu kwa pasu km nyumba ni 2 tangu akuoe Moj mke nyingine Mume Mahakama ikiona watoto ni wadogo watabaki kwa Mama hadi wakikua au mali isigawiwe iandikwe ya watoto na Mama akish mojawapo...
Sawa sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nikiri wazi kuwa Wanawake katika hili wana tatizo sana nimeshashuhudia mshikaji akioa mwanamke mwenye mtoto na akampenda mtoto mapenzi yaliyopitiliza wakati anaolewa mwanaume nae alikuwa na mtoto wake.

baada ya miaka mitatu sasa zile tabia za kike za kumbagua mtoto wa mwanaume zimeshaanza hasa kukitokea kutokuelewana kidogo ndio huonyesha wazi wazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu ni chenga sana, hivyo huyo mkeo amerudisha majeshi kwa jamaa aliyemzalisha then akamtema, what a stuuuuped woman. Ndio maana lazima uwe makini unapofanya choices wakati wa urafiki hadi kuoa, kuoa mtu aliyewahi kuwa na mahusiano hadi kuzaa ni kamari, kanji hawezi kukuacha lazima uumie tu.

Badala ya kuwaza watoto, kuwaza walfare yao, unaanza kuwaza how stupid she is, how if she's dating the guy again.
 
Tofauti kidogo na hiyo kesi. Mimi na mdogo wangu tulizaliwa na wazazi waliokuwa wanaishi pamoja bila ndoa. Baadae mzee akatufukuza usiku wa manane, hii nilikuwa mdogo sana lakini nakumbuka nilivokurupushwa usingizini na kupitishwa kwenye umande usiku wa manane mama akiwa amembeba mdogo wangu mgongoni...
Nyie mna haki ya kurithi mali za baba yenu kama watoto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Najibu hapo mwisho kwenye mchango wa mwanamke. Mke wako ana haki na mali zako hata kama amezikuta.. mchango wake sio lazima uwe pesa..Kama anatekeleza majukumu ya kulea familia na kukutunza huo ni mchango tosha. Haki anayo kama hajakiuka mambo mengine ya mahusiano yenu...
You are a very WISE woman, hongera kwa hilo..
 
Huyo mtoto wa mkeo HANA haki zozote kuhusu mali zako, ila itakuwa uamuzi wako kumgawia chochote, kumsomesha n.k. Mke wako alikuja kama "package" nilidhani utawajali wote na watoto mliozaa naye.

Mkeo ANAZO haki zote kuhusu mali zako au tuseme mali zenu. Ila ikitokea mzee mzima ukatangulia kwenye haki, kuna uwezekano mali zikagawiwa kwa watoto wote wa mke, hapo ni kama mke wako atakuwa hai.

Ni swali zuri sana, uamuzi unawo wewe, na hakuna wa kukulaumu kama hutampa chochote mtoto wako wa kambo, hasa ukifikiria mali za baba wa mtoto wa kambo hazitarithishwa kwa uzao wako.
 
Ndo maan kuowa aggregate 1,0》》》moja bila sitaki...huko mbele lazima kuwe na kisanga...
 
Back
Top Bottom