Mtoto Wa JK (Ridhiwan) Avuruga Mkutano wa UVCCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto Wa JK (Ridhiwan) Avuruga Mkutano wa UVCCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OgwaluMapesa, Mar 3, 2010.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2010
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,947
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Mtoto wa Jakaya Kikwete ,Ridhiwan Kikwete avuruga mkutano wa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa (UVCCM -Taifa) Masauni Yusuph Masahuni.

  Taarifa zinasema Ridhwan aligoma kutoka katika mkutano wa Masahuni na Wenyeviti wa Mikoa wa Umoja huo

  Taarifa zinasema baada ya kutoelewana katika mkutano wa kusimika makamanda ,Mwenyekiti (Masahuni), aliiitisha Mkutano wa Ghafla Asubuhi ya jumapili ulihoshirikisha wenyeviti wote wa Mikoa 20 ya Tanzania Bara wa jumuhia.Taarifa za uhakika zinasema mkutano huo ulivunjika kabla ya kuanza kutokana na kile kilichodaiwa Ridhwan kukataa kutoka nje ya kikao, Mwenyekiti Masahuni alikataa kuendesha mkutano huo kwa sababu Ridhwan Alingangania kuwepo kikaoni.

  Ilikuwa Baada ya Ridhwan kukataa kutoka nje ya ukumbi mkutano wa wenyeviti ulivunjika.

  Hata hivyo taarifa zinasema mivutano ndani ya jumuhia hiyo inatokana Ridhwan kutaka kumburuza Mwenyekiti Masahuni,na mikakati ya Beno Malisa(Makamu Mwenyekiti wa UVCCM) Pamoja na Ridhwan Kutaka kutehua Makamanda na Makatibu wa Uvccm Wilaya Na Mikoa pasipo mshirikisha Mwenyekiti Masahuni kwa matakwa yao maalum kwa ajili ya kumwekea Ridhwan mazingira mazuri kwa ajili ya Uchaguzi ya U-Rais 2025.

  Pili inadahiwa Ridhwan na Beno Malisa Wamekuwa Wakipew Rushwa na Wafanyabiashara ili wawape Ukamanda wa Vijana,Ni hiki ndicho kilichomuhudhi Masahuni hadi kufikia kuitisha mkutano wa ghafla jumapili asubuhi ulioshirikisha wenyeviti wote wa mikoa 20 ya Tanzania bara wa jumuhia hiyo kujadili mienendo ya Makamu wa UVCCM Taifa na Ridhwan Kikwete

   
 2. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Tuletee source ili hoja ijadiliwe vizuri au wewe ndiyo source ya habari yenyewe
   
 3. K

  Kabengwe JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2010
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kageuza viongozi wa UVCCM kama wajakazi wake, kisa mtoto wa Rais?!

  Hongera Mwenyekiti, tunahitaji viongozi kama wewe!

  Wangemuitia Polisi, halafu tuone ingekuaje?!
   
 4. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kuna source tena hapa mkuu??
   
 5. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #5
  Mar 3, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,754
  Trophy Points: 280
  -Duh,wakuu wa dataz mko wapi?

  -kwani Beno Malisa si makamu mwenyekiti?sasa nae angetoka vipi nje ya Mkutano?

  -Kama ni kweli Ridhiwan atakua amekosea sana
   
 6. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #6
  Mar 3, 2010
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kama hii kweli imetokea, naye (Ridhwani) sio Mwenyekiti wa Mkoa, na hana cheo kinachomruhusu kuingia kwa huo Mkutano. Huu ni utoto na kujisikia, na tena ni kiburi cha hali ya juu.

  Lakini pia mleta mada, Tanzania bara ina mikoa 21 na sio 20. Pia huu mkutano ulifanyikia wapi?.
   
 7. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,900
  Likes Received: 1,133
  Trophy Points: 280
  Nafiikiri mwenyewe ndiye source kulingana na namna alivyoandika(not proper Kiswahili tizama). Beno na Ridhiwan ni marafiki wakubwa mno!!!!! Na Beno yuko pale kuhakikisha maslahi ya mtandao ule wa wakubwa yanatekelezwa. SSM na jumuiya zake wanatia aibu. Nafurahia uhuru wa demokrasia ya kufanya maamuzi hata ya kuamua kuwa katika political party fulani!!! Hakuna penye nafuu, ni mizwengwe tu.
   
 8. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,808
  Trophy Points: 280
  source kama sijakosea ni MwanaHalisi ya March 3-9, 2010
   
 9. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 5,009
  Likes Received: 2,534
  Trophy Points: 280
  Kwanza jifunze kuandika kiswahili fasaha, yaani hata kusoma hamu inaisha paragraph ya kwanza tu.
   
 10. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #10
  Mar 3, 2010
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,862
  Likes Received: 2,618
  Trophy Points: 280
  Ameikopi kwa gazeti la Mwanahalisi la leo!
   
 11. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #11
  Mar 3, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,754
  Trophy Points: 280
  -Halafu pia hii ishu ya kumjadili mtu asiyekuwepo imekaaje?

  Atapewa vipi uhuru wa kujieleza?
   
 12. A

  Albano Member

  #12
  Mar 3, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadau hiyotaarifa kwa kweli kwa kiasi kikubwa sana ni ya uongo na inapotosha ukweli wa mambo. Kwa kawaida ndani ya jumuiya ya Umoja wa Vijana kuna utaratibu wa wenyeviti wa mikoa kukutana na mwenyekiti wa Taifa na hali kadhalika makatibu wa mikoa wanakutana na katibu mkuu kama mtendaji mkuu na wao wasaidizi wake mikoani kwa ajili ya kubadilishana mawazo nje ya utaratibu wa agenda za kawaida za baraza kuu la umoja wa vijana.


  Wanakawaida ya kukutana popote pale panapo wakutanisha na kwa sababu yoyote ile ya kuwakutanisha iwe Dar es salaam, Dodoma, Iringa n.k. Kimsingi kikao cha aina hiyo siyo kikao rasmi ila ni cha wenyeviti na mara nyingiene hata wasiokuwa wenyeviti wanaweza kuwepo kwenye kikao hicho kwa sababu hakuna kikao chochote cha kikatiba au kikanuni kinacho wakutanisha wenyeviti na mwenyekiti wa Taifa wala makatibu wa mikoa na Katibu wao Mkuu.


  Kilichotokea Moshi ni kikao cha kawaida kabisa cha kubadilishana mawazo na katika kikao hicho Ridhiwan hakuwepo na hatahilo suala la yeye kukata kutoka kwenye kikao halikuwepo.

  Jingine ambalo ninaliona mtoa mada ana lengo la kupotosha au ana agenda binafsi ni suala la kupatikana kwa makamanda wa Umoja wa vijana wa CCM. Kwa mujibu wa kanuni ya umoja wa vijana na ndivyo hali halisi ilivyo kikao cha uteuzi wa makamanda wa wilaya na mikoa kinaongozwa na mwenyekiti na uteuzi wa makatibu wa wilaya na mikoa hufanywa na kikao cha kamati ya utekelezaji ya Taifa ambacho huongozwa na huyo huyo masauni. Hivyo kusema mwenyekiti anazungukwa na hivyo yeye akaamua kuwaita wenyeviti wa mikoa 20 kuongea nao haimake sense. Hii ni hoja ya hovyo hovyo kujadiliwa na mtu mwenye akili timamu na mchambuzi wa mambo.

  Natoa ushauri wa bure kwa mtoa agenda ni vema akafanya kwanza utafiti kabla hajacopy na kupaste mambo kutoka kwenye magazeti. Haya mambo ya uchochezi na ugombanishi ni yaaibu tunataka mijadala yenye maslahi kwa Taifa letu na siyo kukifanya kiringe hiki kuwa kama kitchen party hatuhitaji mijadala mwepesi na yenye sura ya udaku.

  Tupe data na uzithibitishe tutakuelewa na tutakupongeza kwa kazi nzuri ya kulisaidia Taifa letu.
   
 13. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #13
  Mar 3, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,840
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ah, ccm as usual.
   
 14. F

  Fernandes Rodri JF-Expert Member

  #14
  Mar 3, 2010
  Joined: Apr 11, 2009
  Messages: 424
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Kama hujui lugha nyepesi kama ya kiswahili, basi bora uandike kilugha. Mbwenu
   
 15. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #15
  Mar 3, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Naomba unieleweshe kinachomaanishwa kwenye sehemu zilizotiwa alama nyekundu.

  Naona wenzangu mnachangia mjadala, nadhani mmeuelewa. Naomba mnieleweshe kidogo tafadhali.

  Natanguliza shukrani.

   
 16. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #16
  Mar 3, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 368
  Trophy Points: 180
  And wea is Agwambo? Agwambooooooooo! Please comeback 'ere !
   
 17. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #17
  Mar 3, 2010
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  2025 huyu kilaza awe rais wa wapi?lol We need bright people sio watu wa Thames Valley University..
   
 18. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #18
  Mar 3, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,484
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Swali la kujiuliza ni ..

  Je , ni kipi kipya hapa?? :D
   
Thread Status:
Not open for further replies.
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...