Mtoto wa dada angu kicheche, anafeli na nimuhuni. shule gani itamfaa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto wa dada angu kicheche, anafeli na nimuhuni. shule gani itamfaa?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Somoe, Nov 27, 2010.

 1. Somoe

  Somoe JF-Expert Member

  #1
  Nov 27, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 757
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 60
  Hi, jamani, naombeni msaada wenu wa mawazo. Nina somesha mtoto wa dada angu, shule ya secondary, mama yake alisha fariki na baba ake katiwa ndani, kafungwa kiufupi. Huyu mtoto sasa amenichanga. Jana mama kanipigia sim na kaniambia huyu mtoto anarudi home saa sita za usiku, kila siku sasa. Na anamtukana bibi yake na kugombana nae, hawaelewani. Wiki iliopita kuna kijana alikuja na kisu kwa mama na kumulizia huyu mtoto na kudai anataka kupiga mapanga huyo mtoto akimuona. Out out kaendekeza, masomo anafeli na anamarafiki wasio eleweka, mama kashamshinda. Sasa mie nataka aende kusoma nje ya dar, akienda kijijini labda huko atatulia na atasoma vizuri. Lakini sasa mie sijui shule nzuri huko mikoani, je kuna mtu yeyote ambae atanisaidia kunielekeza shule mzuri jamani, asanteni maana nimechanganyikiwa hata sijui la kufanya.
   
 2. OGOPASANA

  OGOPASANA JF-Expert Member

  #2
  Nov 27, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 35
  Pole sana dada Somoe, kwa upande wangu nakushauri usimpeleke kusoma boarding coz huko ndo kwanza atazidisha hizo tabia zake, tatizo usilikimbie...kiufupi inaonekana mdogo wako amehasirika :
  1 - makundi ya marafiki alionao
  2 - msingi mbovu wa kufuatiliwa kimasomo tangu hapo awali
  3 - mazingira aliyokuwa anaishi na aliyonayo
  4 - mwamko wa shule anayosoma
  5 - muda wa wazazi/ walezi kukaa nae mara kwa mara

  USHAURI: Nashauri kwanza msomeshe kwenye shule za hapa hapa (day schools) ili upate muda mzuri wa kumfuatilia. Pili kama inawezekana kwako muhame maeneo mnayokaa (hasa kama mnakaa uswazi), tatu jaribu kuonana na walimu wake na kuomba msaada wa ufuatiliaji na mawasiliano ya mara kwa mara anapokuwa shule, nne mpe support kielimu mfano kumnunulia vitabu, madaftari, na vifaa vingine muhimu anavyopaswa kuwa navyo shuleni, tano mtafutie tuition nzuri ya masomo anayosoma, sita mnunulie mawasiliano ili uwe unawasiliana mara kwa mara nae ili kujua yupo wapi na anafanya nini, saba msiwe mnampa kazi nyingi nying hapo nyumbani ili awe anapata mda wa kujisomea na kupumzika, nane msiruhusu rafiki yoyote afike nyumbani kumuulizia (rafiki yake awe elimu dunia, na elimu ya dini), tisa jaribu kumwambia aje na wanafunzi wanaokuwa wa kwanza kimkondo pale shuleni kwake ili ujaribu kudadisi wao wanafanyaje hadi wanafaulu na kuwaomba kumsaidia kimasomo huyo wa kwako na kuwaonganisha ili wawe rafiki zake (chuma ufua chuma) coz ukikaa karibu na waridi hukosi kunukia, kumi usikate tamaa katika kumbadili coz sio swala la muda mfupi na sio rahisi.. Mungu awe pamoja nawe.
   
 3. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #3
  Nov 27, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Mpeleke shule za RC kama kifungilo au za wasabato kama PARANE ambazo ni boarding na ulinzi wa kufa mtu ila sasa kama watamtimua ujue ndo mwisho! pia mimi ni mwalimu hapa Dar japo wa muda wa ziada, mlete nimpatie ushauri nasaha, usikimbilie kumhukumu, wanahitaji muongozo, ongea nae kama rafiki, .msikilize na mpe sababu ya madhara unayoyafikiri atayapata, kwa hili nimefanikiwa sana kukibadilisha hiki kishule hapa Dar cha sec kinachoenda kwa jina la International ya kimataifa karibu nanihii, paleeee
   
 4. Somoe

  Somoe JF-Expert Member

  #4
  Nov 28, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 757
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 60
  Asante kaka OGOPASANA. Mie nimejitaidi kila kitu, kila baada ya miezi sita namtumia Milion moja ya vifaa vya shule na matumizi yake. Simu nimemnunulia karibu 8 sasa, ila mara anasema imeibiwa mara betri mbovu, mara ipo kwa fundi. Na nampelekea ela anunue sim mpya, mara kwa mara. Sasa mama kaniambia huyu mtoto ananidanganya na kunitapeli kipesa. Simu anampa rafiki ake amshikie alafu anadanganya imempotea, nikimpelekea ela ananunua sim mpya na ile ya zamani anaiuza na ananunua vitu vingine. Katika wanafunzi wote hapo shuleni yeye ndio mwenye ela zaidi, na hao marafiki zake wanampenda kwa vile anawapa nguo, vipondozi nk. Huyu mtoto hakai na mimi, anakaa na mama angu mzazi ambae ni bibi yake. Na mama kuiama house yake kwa ajiri ya huyu, hatoweza. Shule anayoenda naskia ni wakali sana, na naskia waalim wote wanaume tupu kwaiyo hata yeye mwenyewe anataka kuamia shule ingine yenye waalim mchanganyiko. Mie hata sijui nini haswa nikifanye, maana story ndefu imeanza toka mwaka jana ila sasa imezidi,,, Nikiwa holiday home kwa mama, huyu mototo anaiogopa sana, ushenzi wake haufanyi, ila nikiondoka tu ndio anaanza uuni wake. Asante kwa kunipa mawazo nitayafanyia kazi.......
   
 5. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #5
  Nov 28, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Pole dada Somoe,huyo mtoto ni he or she?
   
 6. Kottler Masoko

  Kottler Masoko Senior Member

  #6
  Nov 28, 2010
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 179
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mpeleke shule za boarding za jeshi kama ile ya kawawa Iringa au kuna shule ipo sumbawanga nimesahau jina,then make sure unamkabidhisha kwa mwalimu senior awe ndo kama mlezi wake,likizo ndogondogo asirudi dar na kubwa mvute karibu na wewe.
   
 7. mojoki

  mojoki JF-Expert Member

  #7
  Dec 1, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 1,333
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Huyo mtoto muachishe shule kwanza akae nyumbani kisha wampe mimba ajifungue mtoto amlee weee aone mziki wake kisha mpe nafasi nyingine ya kusoma u'll experience the difference belive me sister!.Huyo kashaonja utamu wa yale mambo na sasa kanogewa
   
 8. O

  ODILI SAMALU JF-Expert Member

  #8
  Apr 20, 2014
  Joined: Dec 13, 2013
  Messages: 1,261
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  seminari
   
 9. Hebie

  Hebie JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2014
  Joined: Jul 29, 2012
  Messages: 1,319
  Likes Received: 450
  Trophy Points: 180
  1.St. Maurus sec sumbawanga iko chini ya RC they are so serious on student councelling & gaidence
  2.Ndembela sec iko Mbeya wazuri on providing concelling even on perfomance. kama uko serious ni pm
   
 10. godimpare

  godimpare JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2014
  Joined: Feb 10, 2014
  Messages: 828
  Likes Received: 173
  Trophy Points: 60
  acha kuharibu ela zako mwache aolewe nayo ni shule tosha inakuaga na mitihani nayo
   
 11. mimiks

  mimiks JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2014
  Joined: Mar 17, 2013
  Messages: 321
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Pole sana ila inaelekea wewe kazi yako ni kutuma hela tu wala hufatilii maendeleo yake kivile.

  Jaribu kumtoa kwa bibi ukae nae mwenyewe uongee nae kama mzazi na bint yake na kama mtu alivyosema hapo shule anayosoma au utakayompeleka jaribu kuwaeleza walimu hali halisi kwahiyo ataweka chini ya uangalizi wa walimu.

  Boarding ama day lakini kama wewe mwenyewe utakuwa si mfatiliaji sana tatizo litabaki palepale, mabibi wengi huwa wanadekeza watoto. Anahitaji ushauri zaidi kuliko shule ya boarding
   
 12. M

  MahinaVeterani JF-Expert Member

  #12
  Apr 20, 2014
  Joined: Aug 8, 2013
  Messages: 714
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Duh! Baada ya kusoma maelezo ya awali ya Mleta Uzi, nadhani swali lako gumu sana Mkuu. Naombea huyu Mtoto awe "she" kwa maana ya "she" na sio "he" kwa maana ya "she" kwa kuwa itakuwa balaa!
   
 13. H

  Health service Member

  #13
  Apr 20, 2014
  Joined: Mar 8, 2014
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mkuu somoe wewe unachangia kuhalibika kwa huyo mtoto, umesema unamtumia milioni moja kwa matumizi ya vifaa vya shule(siyo ada), hebu fikiria kiasi hicho cha pesa unategemea afanyie nini? kwa kukushauri ni kwamba, kwa sababu umesema huyo mtoto anakuogopa na wewe huishi nae karibu, basi nakushauri ukamtoa hapo kwa bibi yako na ukakaa naye ili umdhibiti vizuri, sikushauri umpeleke shule za boardng kwani kwa tabia uliyoisema haivumiliki boarding kwa hiyo ni rahisi kufukuza shule.
  Pisa inamuhalibu mtoto.
   
 14. Godlove Yamo

  Godlove Yamo Member

  #14
  Apr 20, 2014
  Joined: Jan 10, 2014
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ipe dunia nafasi yake ya ukufunzi!
   
 15. R

  RockSpider JF-Expert Member

  #15
  Apr 20, 2014
  Joined: Feb 16, 2014
  Messages: 6,875
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Huyo mtoto asikuyeyushe mpeleke Kolila, kibohehe, makumira, Elharaman au Ngarenaro LAZIMA atatulia tu...
   
 16. Sista

  Sista JF-Expert Member

  #16
  Apr 20, 2014
  Joined: Sep 29, 2013
  Messages: 3,216
  Likes Received: 173
  Trophy Points: 160
  huyo apelekwe veta akasomee Saloon huko atapata kufanya ayapendayo
   
 17. Mlupembe

  Mlupembe JF-Expert Member

  #17
  Apr 20, 2014
  Joined: Jan 31, 2014
  Messages: 324
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mpeleke akasomee maisha kwa macheni
   
 18. C

  Comfucious pedagogy JF-Expert Member

  #18
  Apr 21, 2014
  Joined: Mar 11, 2014
  Messages: 212
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mpeleke itamba,embaberg,agnes trust,
   
 19. mojoki

  mojoki JF-Expert Member

  #19
  Apr 21, 2014
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 1,333
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nina ka mchepuko kadenti, kana tabia hizo hizo usikute ndo huyo mdogo wako
  ImageUploadedByJamiiForums1398054315.066770.jpg


  In this world nothing is certain than Tax and Death.
   
 20. t

  tabasham Member

  #20
  Apr 21, 2014
  Joined: Jan 16, 2014
  Messages: 66
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mpeleke ST.MATTHEW'S ipo kongowe atatulia mwenyew na haina hata duka la shule la maana zaidi hata kuspend sana ni elf 5 labda kwa siku tena hapo ndo huli chakula cha shule.wanalea vzur sans
   
Loading...