Mtoto wa chuo kahamia kwa mwanaume kisa anapewa hela ndogo ya matumizi chuo

Baba yenu

JF-Expert Member
Jun 17, 2016
1,053
1,417
Hii ni ya kweli nimesimuliwa jana naomba wazazi mjifunze kitu tafadhali.

Kuna binti wa chuo kimoja hapa jijini anatokea Bukoba sasa jamaa yangu akaanzisha nae mahusiano ya kimpenzi. Jamaa hakuwa na nia nae ilikuwa apite tu ila binti akamganda kwasababu ya vipesa kidogo alivyokuwa akimpatia.

Mpaka jana jamaa anasimulia binti alikuwa kalipia hostel ila kahamia kwa jamaa anapika na kupakua na chuo kimefungwa kagoma kwenda kwao sijui kawadanganyaje wazazi.

Ila chanzo cha yote baada ya kusimulia sikumlumu binti bali mzazi wake kwa sababu binti hana mkopo anasimamiwa na mzazi kwa kila kitu ila inafikia hatua mzazi anamtumia binti elf 15 kwa wiki kweli jamani? Binti! Hiyo ndo ale, afanyie mambo yake yote na hapo hajampa hela ya kupigia copy za material za kujisomea na mengineyo.

Kwa usawa huo ni halali binti ahamie kwa jamaa na kutoka hostel maana akiamka ili aende chuo anapewa hela ya kutumia. Mzazi unapojua uwezo hauruhusu basi mpeleke mtoto akasomee kitu unachoweza kumudu kumhudumia mfano ualimu wa diploma ambao wanalishwa na serikali ili kupunguza hizi tamaa.

Ingekuwa mwanaume angekomaa ila binti elfu 15 kwa wiki jamani? Thi is too bad! Hebu wazazi mlioko mikoani na mnawatoto huku tafuteni namna ya kuwasimamia. Mimi binti simlaumu maana hata ningekuwa mimi halafu wa kike baba anitumie 15 kwa wiki haitatosha hata siku tatu pekee.
 
Mie niko upande wa Wazazi binti angejieleza ukweli, kuganda kwa mwanamume hakuondoi tatizo, wala hakumfanyi baba ajue kama hela haitoshi, angekula chakula cha buku mara mbili kwa siku hela ingetosha kuna watu wanashida zaidi yake lkn wanaishi, anayake ambayo hayaingiliani na hiyo pesa wala wazazi wake, hatuwezi kupeleka watoto wote wasome ualimu kisa hatuna uwezo wa kumpatia 50,000/= ama 100,000/= kwa wiki.
 
Kifuatacho jamaa ataanza kupiga mguu yote kama pogba, mpaka amalize chuo.. haha
 
Mie niko upande wa Wazazi binti angejieleza ukweli, kuganda kwa mwanamume hakuondoi tatizo, wala hakumfanyi baba ajue kama hela haitoshi, angekula chakula cha buku mara mbili kwa siku hela ingetosha kuna watu wanashida zaidi yake lkn wanaishi, anayake ambayo hayaingiliani na hiyo pesa wala wazazi wake, hatuwezi kupeleka watoto wote wasome ualimu kisa hatuna uwezo wa kumpatia 50,000/= ama 100,000/= kwa wiki.
We acha kuongea bila experience dar hii tena posta chakula cha buku unapikawewe? Mzazi anajibu hali ngumu mwanangu vumilia!! We usiongee tu kila una uhuru wa kuongea
 
Kukaa kwa mwanaume sio solution ya kutatua matatizo ya pesa za kujikimu na kupata mlo kipindi cha chuo apo binti kakosa akili ya kujiongeza sababu sio lazima kukaa hostel ambako kutakughalimu pesa ya kula kila siku,binti angefanya utaratibu wa kukaa off campus I mean apange rum ya 50 au 40 maeneo ya chuo then io 15 anayo pewa per week ajibane awe anapika at least makali ya ugumu wa maisha utapungua,.....madhara ni mengi kuliko faida za kukaa na ao wanaume kwa kisingizio cha life kuwa tyt chuoni,... Ndo mwanzo wa kupeana mimba na kuishia kuzi frash sababu wote hamkujiandaa kuwa na familia....wazazi kuweni karibu na mabinti wasikilizeni na muwashauli pia vyuoni kuna mengi Sana bila kusahau HIV/AIDS ndo ilipo lalia
 
Maisha ya dar magumu jaman. Ila nadhani kuhamia kwa mwanaume sio maamuzi mazuri , , japo mimi pia niliwahi kumhamishia binti wa chuo kwangu , ila na mm pia nilikuwa mwanachuo kipibdi hicho....
 
Hii ni ya kweli nimesimuliwa jana naomba wazazi mjifunze kitu tafadhali.

Kuna binti wa chuo kimoja hapa jijini anatokea Bukoba sasa jamaa yangu akaanzisha nae mahusiano ya kimpenzi. Jamaa hakuwa na nia nae ilikuwa apite tu ila binti akamganda kwasababu ya vipesa kidogo alivyokuwa akimpatia.

Mpaka jana jamaa anasimulia binti alikuwa kalipia hostel ila kahamia kwa jamaa anapika na kupakua na chuo kimefungwa kagoma kwenda kwao sijui kawadanganyaje wazazi.

Ila chanzo cha yote baada ya kusimulia sikumlumu binti bali mzazi wake kwa sababu binti hana mkopo anasimamiwa na mzazi kwa kila kitu ila inafikia hatua mzazi anamtumia binti elf 15 kwa wiki kweli jamani? Binti! Hiyo ndo ale, afanyie mambo yake yote na hapo hajampa hela ya kupigia copy za material za kujisomea na mengineyo.

Kwa usawa huo ni halali binti ahamie kwa jamaa na kutoka hostel maana akiamka ili aende chuo anapewa hela ya kutumia. Mzazi unapojua uwezo hauruhusu basi mpeleke mtoto akasomee kitu unachoweza kumudu kumhudumia mfano ualimu wa diploma ambao wanalishwa na serikali ili kupunguza hizi tamaa.

Ingekuwa mwanaume angekomaa ila binti elfu 15 kwa wiki jamani? Thi is too bad! Hebu wazazi mlioko mikoani na mnawatoto huku tafuteni namna ya kuwasimamia. Mimi binti simlaumu maana hata ningekuwa mimi halafu wa kike baba anitumie 15 kwa wiki haitatosha hata siku tatu pekee.
huyo binti yuko kimalengo ngoja apate kazi pengine hata huyo jamaa asimkumbuke na inawezekana ajapenda ila kutokana na ugumu wa maisha
 
We acha kuongea bila experience dar hii tena posta chakula cha buku unapikawewe? Mzazi anajibu hali ngumu mwanangu vumilia!! We usiongee tu kila una uhuru wa kuongea
Pole kaka tuanze na mama ntilie waliopo maeneo yote hapo posta, halafu tumalize na cafeteria za chuo ambazo huwa zinafixed price tofauti Dar umekuja wenzio tumezaliwa. Ninakuhakikishia kipo chakula cha Buku cha wanafunzi
 
Acha uongo wewe kuzaliwa isiwe shida...unaweza zaliwa manzese na we ukajiona wa dar.....mamantilie wa bei nafuu kabisa posta ni elf 2
 
Pole sana, manzese ndio eneo pekee Dar ambalo hata wewe walifahamu bila kuelekezwa, basi hakika ujue hapo ni Dar.
Acha uongo wewe kuzaliwa isiwe shida...unaweza zaliwa manzese na we ukajiona wa dar.....mamantilie wa bei nafuu kabisa posta ni elf 2
 
Hii ni ya kweli nimesimuliwa jana naomba wazazi mjifunze kitu tafadhali.

Kuna binti wa chuo kimoja hapa jijini anatokea Bukoba sasa jamaa yangu akaanzisha nae mahusiano ya kimpenzi. Jamaa hakuwa na nia nae ilikuwa apite tu ila binti akamganda kwasababu ya vipesa kidogo alivyokuwa akimpatia.

Mpaka jana jamaa anasimulia binti alikuwa kalipia hostel ila kahamia kwa jamaa anapika na kupakua na chuo kimefungwa kagoma kwenda kwao sijui kawadanganyaje wazazi.

Ila chanzo cha yote baada ya kusimulia sikumlumu binti bali mzazi wake kwa sababu binti hana mkopo anasimamiwa na mzazi kwa kila kitu ila inafikia hatua mzazi anamtumia binti elf 15 kwa wiki kweli jamani? Binti! Hiyo ndo ale, afanyie mambo yake yote na hapo hajampa hela ya kupigia copy za material za kujisomea na mengineyo.

Kwa usawa huo ni halali binti ahamie kwa jamaa na kutoka hostel maana akiamka ili aende chuo anapewa hela ya kutumia. Mzazi unapojua uwezo hauruhusu basi mpeleke mtoto akasomee kitu unachoweza kumudu kumhudumia mfano ualimu wa diploma ambao wanalishwa na serikali ili kupunguza hizi tamaa.

Ingekuwa mwanaume angekomaa ila binti elfu 15 kwa wiki jamani? Thi is too bad! Hebu wazazi mlioko mikoani na mnawatoto huku tafuteni namna ya kuwasimamia. Mimi binti simlaumu maana hata ningekuwa mimi halafu wa kike baba anitumie 15 kwa wiki haitatosha hata siku tatu pekee.
we hujui swaga za watoto wa kike nini,wanapenda miteremko a.k.a kitonga,hapo ataisimanga familia yake yote utasikia oooh nyumbani wananitesa,mara mama ananinyanyasa,mara oooh hawanitumii hela,ndivyo walivyo wala usimlaumu mzazi hapo tangu ameanza kumlea mpaka hapo amefika ndio ameanza kumnyima matumizi?
 
Back
Top Bottom