Mtoto wa Charles Taylor aliyekuwa rais wa Liberia alitumia cheo cha Baba yake kuua na kutesa watu

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
MFAHAMU MTOTO WA RAIS ALIYETUMIA CHEO CHA BABA YAKE KUUA, KUTEKA NA KUPOTEZA WAKOSOAJI WA BABA YAKE

Huyu anaitwa Charles "Chuckie" McArthur Emmanuel Taylor Jr, au wenyewe walimuita Demon. Huyu ni mtoto wa dikteta wa zamani wa Liberia Charles Taylor aliyeondolewa na umma kwa msaada wa jeshi la nchi hiyo.
Charles Taylor katika utawala wake aliendesha mauaji ya wapinzania, wakosoaji na wanaharakati wengi nchini Liberia, utekaji ukishamiri, na kila aina ya maovu ya kiinchi yalifanywa ilimradi tu ulikwenda kinyume na utawala huo, .

Yote haya aliyafanya Charles Taylor kupitia mtoto wake huyu aliyeitwa Chuckie, ambapo ili kutekeleza hili, kitengo binafsi cha ushushushu wa rais (state intelligence) kilikamatwa na huyu mtoto na kukiongoza vyovyote atakavyo, .

Kitengo hiki kilikuwa na nguvu kuliko hata idara ya usalama wa taifa wa nchi hiyo (National Intelligence) ambapo mkurugenzi wa Usalama nchini hakuwa na sauti mbele ya Chuckie, kwa lugha rahisi nikuwa Chuckie alishika mamlaka ya ujasusi yote nchini ambapo sauti yake iliogopwa kama ya simba.
.

Kwasababu ya uchanga wake kiakili na kwakuwa hakuwa na mafunzo yoyote ya ujasusi, mtoto huyu alipowamaliza wapinzani na wanaharakati wa nchi hiyo, alihamia kwa matajiri akiwateka na kupora mali zao na mwisho akawa anaitumia idara hiyo kupora wanawake wazuri katika klabu za starehe na kwingine walio na wapenzi/waume zao, na walipojaribu kupinga walikabiliwa na mateso makali na vifo.
.

Baada ya baba yake dikteta Charles Taylor kung'olewa madarakani, huyu mtoto alikimbilia Marekani akidhani atasalimika, lakini alikamatwa hukohuko na kufikishwa mahakamani kwa mauaji na mateso ya raia na mwisho alifungwa jela miaka 97, tangu mwaka 2009 mpaka sasa.

1564236390191.jpeg
 
Anabahati sana kufungwa us,
Angefungwa huku africa ushenzini angefukuliwa tope,tena na alivyo mrembo
 
Back
Top Bottom