Mtoto wa Chacha Wangwe ndiye Kapeleka fomu kwa Lissu? Hapo ndio mwisho wa majungu

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,795
71,214
Mwanasheria kijana ambaye pia ni mwanaharakati maarufu wa haki za binadamu Bob Chacha Wangwe majuzi alikuwa Brussels Ubeligiji kwa kushughuli zake ambazo hazijaainishwa pengine zikiwa za binafsi zaidi.

Kijana huyu machachari (ndiye aliyefungua kesi kupinga DED's kuwa mawakala wa NEC) pia ni mtoto wa mwanasiasa mashuhuri marehemu Chacha Wangwe aliyekuwa Makamu mwenyekiti wa CHADEMA taifa na kufariki kwa ajali ya barabarani huko Dodoma miaka kadhaa iliyopita.

Lissu kajaza fomu kugombea makamu mwenyekiti taifa. Fomu zimefikaje kwake? Jee ni online au kapelekewa na mwanasheria huyu kijana mtoto wa makamu wa mwenyekiti wa zamani?
Bila kutumia akili hili laweza kuwa jambo dogo lakini kwa jicho la tatu la kisiasa waweza kuona calculated benefits ambazo Chadema wanaweza kujipatia kama kweli fomu hizo zimepelekwa na kijana huyo.

Zile blabla zilizokuwa zinaenezwa na CCM kuhusu baba wa kijana huyo dhidi ya CHADEMA ndio zimekufa rasmi watafute kingine maana wao ni kama wachawi hata ukivaa kitenge kipya ni sababu tosha ya kukuloga.
bob_chacha_wangwe___B5XxsaXJCxM___.jpeg
 
Itapitishwa sheria kuzuia wanachama wanaotaka kugombea uongozi wa vyama vyao kujaza fomu za kugombea wakiwa nje ya nchi, maana sheria zetu tunazitunga ili kudhibiti mbinu, mbwembwe, juhudi au ubunifu wowote unaoweza kuwapa umaarufu na political mileage wapinzani🤣🤣🤣
 
Hofu kuu ya CCM ni Chadema mara Zote.
Washukuru Mzee White hair alizingua 2015, ingelikuwa siyo yeye tusingekuwa hapa tulipo. Maana Jiwe alitangazwa kihuni wala hakushinda.
 
Kasahau Baba yake alikufa kisa kutaka kugombea Uenyekiti. Lissu nimemdharau sana. Kwa nini hajagombea Uenyekiti ?
 
Mtu anapogeuka prophet kuanza kubuni vitu bwana!

Halafu katika kubuni huko anakimbia kuja kwaambia ulimwengu what his shitty brain is lying to him!

Who cares what you unahisihisi?

Nobody cares about hisia za mtu mwingine maana kika mwanadamu ana mihisia chungu nzima!
 
Kasahau Baba yake alikufa kisa kutaka kugombea Uenyekiti. Lissu nimemdharau sana. Kwa nini hajagombea Uenyekiti ?

Ndilo hilo nilitaka mlianzishe, mumesingizia Chadema uzushi huo mkaenda Tarime wanapoujua ukweli mkaishia kupigwa mawe.
Mkamkabili Bob alipokuwa mdogo,sasa kasoma na kuujua ukweli wa ndani anaishirikisha Chadema katika maisha yake kama salamu kwa CCM kuwa unafiki wenu anaujua.
Nyie mnajifanya mnauchungu kwa baba yake kumbe uchawi tuu umewajaa mioyoni mwenu!
 
Dogo kachagua upande wa kipuuzi sana..ambao ataishia kumtesa tu mama yake..stupid
 
Hakuna mwenye akili ambaye anaweza hata kufikiria kuwa kiongozi au mfuasi yeyote wa CHADEMA aliwahi kuuawa na CHADEMA yenyewe.

Serikali mara kadhaa imekuwa ikihangaika kuwatengenezea mashtaka bandia watu wa CHADEMA (ref. Kifo cha Akwilina, kesi na hatimaye kumfunga Sugu kwa kumwonea, kumfunga Lijuakali kwa kumwonea, mashtaka lukuki ya bandia kwa viongozi wote wa CHADEMA), halafu iupate mwanya wa wazi wa makosa ya jinai dhidi ya CHADEMA, iache kuutumia? Lazima uwe mjinga wa kudumu kulifikiria hilo, achilia mbali kuliamini.

Uzuri ni kwamba hakuna hata mtu mmoja, hata yule ambaye ana ujinga wa wastani ambaye amewahi japo kufikiria kuwa kifo cha Wangwe kwa namna yoyote kulikuwa na kuhusika kwa CHADEMA.
 
Hao wanafahamu fika waliomuua baba yao na hawahitaji kuwa lectured na mtu.

Wanakumbuka vema wakati wa msiba ukoo wao ulihitaji kuleta Forensic Pathologist toka Kenya kuja kuchunguza mwili lkn serikali ilikataa katakata, why..!! Mchezo unaishia hapo.

Pia kufuatia kifo hicho hakuna hata kiongozi moja wa Chadema aliyetiwa nguvuni kuhusiana na hilo sakata na ndio maana wengi wa jamii ya wakurya bado wanaiunga mkono Chadema hadi leo na hata Waitara analifahamu hilo na ndio maana Tarime hawamtaki katakata wanamwambia ubunge akagombee Chattle.
 
Back
Top Bottom