Mtoto wa Bosi ni Bosi...Amini Usiamini!

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,723
Nimeshuhudia kituko leo ofisini.

Ofisi yangu ina Makao Makuu huko Dar, na huko ndo aliko Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni. Bosi wangu mimi ni Meneja wa Idara hapa Mkoani.

Leo hapa ofisini amepita mtoto wa huyo Mkurugenzi, binti mdogo wa miaka 20, ambapo alikuwa tu ana mambo yake binafsi maeneo haya!

Ajabu, bosi wangu, pamoja na difference ya umri ya miaka almost 35 na hako kabinti, ameacha kazi zake, amempokea mabegi na kuanza kumuulizia shida yake hapo kwa nia amsaidie yeye personally!
Tumejaribu kumsaidia huyu mkuu ili arudi kwenye kazi zake, wapi bana...ni kwamba amechanganyikiwa jumla,anapanda na kushuka kwenye ngazi kwa kukimbia. Leo ndo nimemwona mkuu wangu huyu kwa mara ya kwanza anakimbia, bila kujali umri wake!

Sijui ndo nini, mi sielewi. Au ndo ile wanaita nidhamu ya woga, sasa ina'apply hadi kwa mtoto wa bosi?

Angekuwa Kihiyo ningesema labda analinda ajira yake, lakini ni msomi mzuri!

Embu wanajamvi nisaidieni, hii ni behavior gani mahala pa kazi?
 
khaaaa hiyo kali!!! kabinti kakirudi kwa faza katamsifia mkubwa ile mbaya!!! may be ze boss atamfikiria siku moja in case of anything!!!!
 
Maboss wa TZ ni sawa na waalimu-ndio wenye degree mkononi so nilazima kutikisa mkia kama mbwa amwonapo mwenye nyumba karudi. Ni ulemavu wa akili zetu.
 
Huwezi jua..
Labda jamaa moyo wake umemdondokea mtoto wa bosi

Si kweli PJ ana miaka 51 na amesema bosi wake amemzidi kwa umri kwa miaka 35 so tunazungumzia 51+35=? si atafia kwenye naniliu
 
Mkuu PJ,

Kama kana miaka ishirini ina maana kakubwa hako. Unaweza kunipasia simu ya hako kabinti kalikodekezwa na Boss wako? Fanya hivyo kama Taarabu ipo. :)

Usishangae sana kuhusu Boss wako. Ndiyo hiyo inaitwa COMPLEX. Nina uhakika huyo Boss akiniona mie na Suti yangu niliyonunua NIMEINAMA, atajifanya kwanza anaongea kwenye simu na mwisho kwa mbwembwe ataniuliza shida ingawa hapohapo ubongo wake unapanga tayari jibu la kunitoa bila MSAADA WOWOTE.
 
PJ hata mtoto wa masikini ni masikini tu...mtoto wa masikini akikatiza sehemu za kazi za watu fulani fulani kwani waga wanashtuka? sana sana utasikia ningoje pale nnje nakuja na utangoja kwa masaaaa mpaka ukome!
 
Mkuu PJ,

Kama kana miaka ishirini ina maana kakubwa hako. Unaweza kunipasia simu ya hako kabinti kalikodekezwa na Boss wako? Fanya hivyo kama Taarabu ipo. :).
Mkuu Sikonge, ni kweli ni kakubwa, lakini compare na huyo Mkuu kiumri!, more than twice!
Usishangae sana kuhusu Boss wako. Ndiyo hiyo inaitwa COMPLEX. Nina uhakika huyo Boss akiniona mie na Suti yangu niliyonunua NIMEINAMA, atajifanya kwanza anaongea kwenye simu na mwisho kwa mbwembwe ataniuliza shida ingawa hapohapo ubongo wake unapanga tayari jibu la kunitoa bila MSAADA WOWOTE.

Ndo zao hizo mabosi hawa...They just want yo use the surbodinates...then wanawa'dump.
Na hiyo suti vp mkuu, ni ya utata nini!
 
Kumbe basi tusimwelewe jamaa vibaya labda anataka kuoa na kama ameoa anataka kutimiza msemo wa GEOF NA XSPIN kudumisha mila.
NI VIJANA WACHACHE SANA HUMU JAMVINI tunaodumisha mila!actually TUNAHESABIKA
 
PJ umenikumbusha ile movie ya Edy Murpy ya WELCOME TO AMERICA...
Baba wa watu alivyokua anachunga unga wake..duh
isijekua amefanya bifu tayari huyo......
 
Nimeshuhudia kituko leo ofisini.

Ofisi yangu ina Makao Makuu huko Dar, na huko ndo aliko Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni. Bosi wangu mimi ni Meneja wa Idara hapa Mkoani.

Leo hapa ofisini amepita mtoto wa huyo Mkurugenzi, binti mdogo wa miaka 20, ambapo alikuwa tu ana mambo yake binafsi maeneo haya!

Ajabu, bosi wangu, pamoja na difference ya umri ya miaka almost 35 na hako kabinti, ameacha kazi zake, amempokea mabegi na kuanza kumuulizia shida yake hapo kwa nia amsaidie yeye personally!
Tumejaribu kumsaidia huyu mkuu ili arudi kwenye kazi zake, wapi bana...ni kwamba amechanganyikiwa jumla,anapanda na kushuka kwenye ngazi kwa kukimbia. Leo ndo nimemwona mkuu wangu huyu kwa mara ya kwanza anakimbia, bila kujali umri wake!

Sijui ndo nini, mi sielewi. Au ndo ile wanaita nidhamu ya woga, sasa ina'apply hadi kwa mtoto wa bosi?

Angekuwa Kihiyo ningesema labda analinda ajira yake, lakini ni msomi mzuri!

Embu wanajamvi nisaidieni, hii ni behavior gani mahala pa kazi?
mkuu mi hiyo nimeiona hapa ughaibuni,kaja mkuu mmoja toka jirani yetu hapo basi nilishangaa bosi wetu nae katoka na viatu vya huyo mkulu kampa dereva avisafishe kila mtu ofisini aliachama,ukizingatia ilikua summer
viatu hata havikua na uchafu aisee.noma kweli
 
mkuu mi hiyo nimeiona hapa ughaibuni,kaja waziri toka nchi fulani jirani yetu hapo basi nilishangaa bosi wetu nae katoka na viatu vya huyo waziri kampa dereva avisafishe kila mtu ofisini aliachama,ukizingatia ilikua summer
viatu hata havikua na uchafu aisee.noma kweli

Bora hata huyo bosi wako alikuwa anamwogopa waziri!
Sasa inapokuwa ni mtoto wa waziri inakuwaje!

Hivi vyeo vya ujombaujomba hivi...vina shida mnoooo!
 
Back
Top Bottom