Mtoto wa balozi wa ccm achana bendera ya ccm njombe,kisa mgomo wa walimu

lutondwe

Senior Member
Dec 20, 2010
150
74
Katika kudhirisha kuwa sasa CCM imechokwa leo juzi mtoto wa balozi wa CCM kata ya Mjimwema Njombe aliamua kuchoma bendera ya CCM kwa imani kuwa chama hicho ndicho kimesababisha mgomo wa walimu na yeye kukosa fursa ya kupata masomo wakati huu wa mgomo wa walimu.Mtoto huyo ni darasa la saba na anayetarajia kufanya mtihani wa kumaliza shule mwaka huu.Baada ya kufanya tendo hilo mama yake mzazi ambaye alikuwa balozi mpya wa CCM aliamua kujisalimisha kwenye mkutano wa CHADEMA na kuchukua kadi ya CHADEMA mbele ya mwenyekiti wa vijana Taifa aliyefanya ziara hapa Njombe.Tukio hili limeleta hamasa kubwa kwa wananchi wa Njombe kwa uamsho mpya toka kwa watu ambao zamani wasingewezA kufanya hivyo.
 
haya ndio ukombozi unaanza taatibu kuanzia kwa kizazi kipya ccm na kizazi chakavu
 
Ni utukufu wa Mungu unajidhihirisha, kila kiumbe alichokiumba alikipatia nguvu ya kuweza kujipatia ufahamu na maarifa ya kutosha kuweza kuishi katika nyakati zote alizoziamuru hapa duniani. Watanzania sasa wanafunguka.
 
Safii sana kijana naona sasa somo la nani anatufikisha hapa tulipo linaanza kuwafikia wananchi.nice to hear!!!!
 
mtoto amejitambua hataki ujinga bravo mtoto kwa kujua nani analeta kiwingu kwenye maisha yako
 
Back
Top Bottom