Mtoto usiye na uhakika nae

Bayo

Senior Member
Jul 2, 2009
195
34
jaman mwenzenu nahisi nimesingiziwa mtoto maana nafanana nae vidole tu, nahisi hio ni coincidence.... Mana huyu mama yake hakuwa mtulivu sna... People!!!!!!! DNA ya bei rahisi ni sh. Ngapi?
 
tumezoea kusingiziwa,angalia kama kuna faida ya kuwa na huyo mtoto,wanawake wanatusumbua sana kwenye kutusingizia watoto,mkuu hiyo ni serious issue
 
Vidole tu???na sura je ni ya mtu mwingine? Watoto wengine wakiwa wadogo hawafanani na wazazi lakini kadri anavyokua ndo anavyofanana na baba na mama some features ofkoz not everything...hebu nenda pale Regency na uhakika watakua na hiyo huduma kama uko dsm lakini
 
ndo maana kuna makabila mtoto anakuwa mali ya mama akipelekwa shule anaandikishwa jina mama mfano Alex sophia
 
Unaishi na huyo mama yake au vp? Kama unaishi nae na ukafanya ufanyalo kupata ukweli kuwa sio wako utaamua nini? What is in your mind about currently/future life ya huyo mtoto?? Kama utaona huyo mtoto hatapata msaada wowote wa matunzo endapo utammwaga mama yake, nakushauri usihangaike kuchunguza just mlee for the sec of the kid's life Bro! No matter people would talk about, just mlee kwa kuokoa maisha yake ya sasa na baadae coz who knows after? Kwa sie wacha Mungu huo ni mtego wa kiimani na malipo ni hapahapa. Nina true story ya case kama yako (about 25 years ago na Baba aliyepewa mtoto akakataa anajuta hadi leo na mtoto aliokolewa na uncle wake) sema ndio hivyo muda na kutype kuna kaba.
 
ndo maana kuna makabila mtoto anakuwa mali ya mama akipelekwa shule anaandikishwa jina mama mfano Alex sophia
<br />
<br />

Hahahah.....Alex Sophia...hiyo kali! Huwa naangalia matokeo ya wanafunzi waliohitimu darasa la saba nchini karibu kila mwaka sijawahi kukutana na jina la namna hiyo...inawezekana huwa hawamalizi shule hao.
 
Vumilia mkuu kitanda hakizai haramu. Huwezi jua labda hata dingi wako alisingiziwa na mama yako. Hayo huwa hatusemi tunanyamaza tu. Mwenye uhakika ni mama. Hata hivyo una bahati kama unaona vidole ni vyako. Si lazima mtoto ukimzaa akufanane wewe, anaweza hata kumfanana babu wa babu yake au bibi wa bibi yake. Kama umesoma biolojia nadhani kuna somo la genetics linaeleza vizuri kuhusu suala hilo.
 
usikute unataka kukimbia majukumu. Ungefanana vp vidole na mtoto kama sio wako? Wapi iliandikwa mtoto lazima afanane na baba? Anyway kapime dna
 
usikute unataka kukimbia majukumu. Ungefanana vp vidole na mtoto kama sio wako? Wapi iliandikwa mtoto lazima afanane na baba? Anyway kapime dna

una hakika dna inasema kweli??kwa taarifa yako inategemea na jamaa aliyempa mimba kama damu ni group moja na wewe mtoto ataonekana ni wako,bora kukubali yaishe
 
Nenda kapime DNA kwa nini ukae na wasiwasi muda wote wa maisha yako?

Kuna ndugu yangu wa karibu sana alimwoa mama mmoja na mimba akaambiwa ni ya kwake. Baada ya miaka kama 15 mama akamgeuzia kibao na kumwambia yule first born siyo wa kwake na baba halisi alikuja kumchukua. Kwa kweli tulisikia uchungu sana maana ilikuwa ni kama kudhalilishwa hivi.
 
Siku zote nilikuwa najua DNA Tanzania inafanywa sehemu moja tu kwa mkemia mkuu kama sikosei. Kweli una uhakika regency wanafanya DNA? Lakini kuaccess DNA si kitu rahisi kwa Tz nadhani inabidi uwe na hoja ya msingi.
Vidole tu???na sura je ni ya mtu mwingine? Watoto wengine wakiwa wadogo hawafanani na wazazi lakini kadri anavyokua ndo anavyofanana na baba na mama some features ofkoz not everything...hebu nenda pale Regency na uhakika watakua na hiyo huduma kama uko dsm lakini
 
DNA has nothing to do with blood group. Na wala haikosei. Ndio maana nchi zilizoendelea wanakamata sana wahalifu hasa wa mauaji kwani hata nywele inatosha kupima DNA ya mtu.
una hakika dna inasema kweli??kwa taarifa yako inategemea na jamaa aliyempa mimba kama damu ni group moja na wewe mtoto ataonekana ni wako,bora kukubali yaishe
 
kwa sasa wamekataza mpaka uwe na karatasi toka mahakamani, maana ilipoingia hadi waliogombana tu walienda kupima watoto kukomoana, na kweli walikuta wengine sio wa baba huyo
 
kwa sasa wamekataza mpaka uwe na karatasi toka mahakamani, maana ilipoingia hadi waliogombana tu walienda kupima watoto kukomoana, na kweli walikuta wengine sio wa baba huyo

That's just unnecessary bureaucratic red tape.
 
huyo ni mwanao bana.....sasa unataka usema vidole ni vyako...kichwa ni cha mwingine,,,,sikio ni la mwingine????
 
Back
Top Bottom