Mtoto na Baba waoa nyumba moja-Matatizo katika familia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto na Baba waoa nyumba moja-Matatizo katika familia

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Fidel80, Jun 4, 2008.

 1. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,981
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Source;Mzee wa Sumo.
  Jamaa wawili walikutana kwenye kituo cha basi wakafanya mazungumzo. Mmoja aling'ang'nia kuzungumzia kero za familia yake hatimaye mwenzake akasema " Unadhani familia yako ina matatizo?"
  Basi sikiliza kisa hiki.
  "Miaka michache iliyopita nilikutana na mwanamke mjane aliyekua na binti mkubwa tu na tukaamua kuoana. Baadaye baba yangu akamuoa binti yangu wa kambo hivyo huyo binti yangu wa kambo akawa mama yangu wa kambo na Baba yangu akawa mtoto wangu wa kambo wa kiume ambapo mke wangu akawa mama mkwe wa mkwe wake.

  Baadaye binti yamke wangu yaani binti yangu wa kambo alipata mtoto wa kiume. mtoto huyo wa kiume alikua ndugu yangu kwa sababu tulichangia baba mmoja. lakini kwa vile alikua ni mtoto wabinti wa mke wangu papo hapo akawa mjukuu wa mke wangu na mimi nikawa babu yake ndogo wangu.

  Lakini hayo yote yalikua si kitu mpaka mimi na mke wangu tulipopata mtoto wa kiume. Sasa msichana ambaye ni ndugu wa mtoto wangu huyo wa kiume kwa kuchangia mama yao mmoja, akawa pia bibi yake. Hali hiyo ilimfanya pia baba yangu kua shemeji wa mtoto wangu ambaye ndugu yake wa kike kwa upande wa mama yao ndie mke wake baba yangu. Kwa hiyo mimi ni shemeji yake mama yangu wa kambo ambapo mke wangu ni mama mdogo (anti) wabinti yake mwenyewe . Mtoto wangu wa kiume ni mpwa wa baba yangu ambapo mimi nikawa babu yangu mwenyewe.
  SWALI.
  Je, unadhani mpaka hapo wewe una matatizo ya kifamilia? Acha kulalamika
   
 2. Kilinzibar

  Kilinzibar Senior Member

  #2
  Jun 4, 2008
  Joined: Mar 6, 2008
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  duh kweli mimi na fidel castro tuna undungu kwa mfumo huu
   
 3. Shishi

  Shishi JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2008
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,245
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  duh! hapo nimechanganya kabisa, too complex!!
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,981
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  ndo hali halisi mwanae alioa mama na baba yake kamwoa binti........too complex
   
 5. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #5
  Jun 4, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 9,220
  Likes Received: 4,112
  Trophy Points: 280
  Inabidii hapo baba na mwana wawe washikaji wakitaka ku solve tatizo hilo...la sivyo....haliwezekani
   
 6. C

  Chief JF-Expert Member

  #6
  Jun 5, 2008
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,403
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Imenibidi nichore kwenye karatasi kwanza ili niweze kuelewa
   
 7. Kesa

  Kesa Member

  #7
  Jun 7, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukiona kwako kuna ungua, kwa mwenzio kunateketea????!!!!
   
 8. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #8
  Jun 7, 2008
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,712
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  ...kesi namna hiyo inakuwa ajua!, kisha mnaanzia mazungumzo kwenye ngazi ya ushemeji na baba yako!
   
 9. B

  BABU KIZEE JF-Expert Member

  #9
  Sep 28, 2013
  Joined: May 18, 2013
  Messages: 452
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  wamekuwa kama mbuzi
   
 10. E

  Edison JF-Expert Member

  #10
  Sep 29, 2013
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 399
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Weka family tree mkuu make maelezo yananichanganya
   
 11. Ficus

  Ficus JF-Expert Member

  #11
  Sep 9, 2015
  Joined: Jul 14, 2013
  Messages: 1,194
  Likes Received: 645
  Trophy Points: 280
  Aisee hii kali'
   
Loading...