Mtoto mwizi nifanye nini nimuokoe? Naomba ushauri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto mwizi nifanye nini nimuokoe? Naomba ushauri

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Goldman, Feb 7, 2011.

 1. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,262
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Kaka yangu ana mtoto ambaye inatakiwa aanze form one mwaka huu, tatizo ni mwizi alikuwa anakaa kwa dada yetu mkubwa akawa anaiba hela kwake wakati yuko darasa la 6 mpaka 7, anaiba ananunua sim, nguo,viatu etc anaweka kwa majirani. Dada alipomshtukia akamrudisha kwa baba yake ambaye hana uwezo kivile, dada yetu mdogo akamchukua kakaa naye miezi kadhaa akawa anaingia chumbani anaiba hela akamtimua. Wiki 2 zilizopita akiwa kwa baba yake aliondoka akaenda kwa Mke wa zamani wa baba yake akaiba deck ya dvd, siku hiyo akaenda kwa majiran wanao mfahamu akaiba simu na nguo, wakamkamata navyo wakampeleka kwa baba yake hajui cha kufanya, leo amemleta kwangu jamani akili imesimama, nikae naye? Nimrudishe kwa baba yake ambaye uwezo kidogo, nimpeleke police wakamnyoshe? Ningekuwa na hela sasa hivi ningemtafutia shule ya watoto watukutu uwezo huo upo lakini itachukua may be a month.
   
 2. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  mpeleke akaombewe pepo la wizi limtoke kwa jina la yesu huyo ni maombi tu
   
 3. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #3
  Feb 7, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Hebu mchekini tabia yake, siyo mla unga huyo? Otherwise hiyo ni tabia ya baadhi ya watoto hasa teenagers, asilimia kubwa huwacha wakiwa wakubwa hivi.
   
 4. s

  shosti JF-Expert Member

  #4
  Feb 7, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  mhh jamani malezi,ila mkijaribu kuongea nae kwa utulivu ataacha tu,unajua na malezi yetu kidogo wakati mwingine huwa badala ya kurekebisha yanazidisha tatizo,mtoto hawezi pigwa danadana kama mpira bwana.
   
 5. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #5
  Feb 7, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,262
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Thanks
   
 6. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #6
  Feb 7, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,262
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  hatumii unga ila nina wasiwasi laptop, simu. Roho iko juu juu naye ndo mtoto wa kaka toka nitoke, nami sina mtoto. Napenda kukaa naye swala ntaweza?
   
 7. jamii01

  jamii01 JF-Expert Member

  #7
  Feb 7, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,837
  Likes Received: 372
  Trophy Points: 180
  maombi tu....yatosha!
   
 8. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #8
  Feb 7, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Pole sana mkuu.

  Huyo mtoto anaendeleza tabia ya wizi kwa vile hajapewa discipline bado.Anaona kwamba hamumfanyi kitu chochote akiiba ndio maana anaendeleza.

  Sasa tabia yake imevuka mpaka na kufikia kuwaibia majirani siku watakuja kumpa kipigo mkampoteza.


  Muhimu cha kufanya mnaweza kumpeleka polisi wamueke rumande siku 2 tatu alafu muone kama atabadirika au hapana.Hasipo badirika mrudisheni polisi waambieni wampe adhabu ya kumshikisha adabu.

  Kuna njia zao wanatumia ambazo ni nzuri kwa kumfunza mtu kama huyo,hawato mpiga kama wezi wengine watampiga kwa njia ya kumtia adabu.
   
 9. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #9
  Feb 7, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,262
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Thanks mkuu ushauri wako mzuri, ni kweli hajawahi kuadhibiwa zaidi ya vibao viwili vitatu. Thanks
   
 10. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #10
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Huyo mtoto alitakiwa akung'utwe kisawasawa mpaka aone wizi ni mbaya na haufai kwa jamii..... yaani nyie watu wazima na akili zenu mmekaa mnafikiri kumwambia tu wizi ni mbaya ataacha. Kwanza nadhani nyie ni wavivu wa kufikiri ndio maana unakuja kuomba ushauri kabla hata ya kujaribu kutibu tatizo zaidi ya hilo nyie ndo mlosababisha mpaka huyo mtoto sasa anaibia majirani zenu.... h:twitch:aya endeleeni tu kumwangalia muone kama hakuja kuwatoa roho ninyi wenyewe...
   
 11. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #11
  Feb 7, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,262
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Thanks
   
 12. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #12
  Feb 7, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  Stealing is wrong, and the best way to understand it ni kuchunguza mawazo ya mtoto wako. Mtoto ambae huiba often feel entitled to what they’re stealing, even though they or their parents can’t afford it. Kuna mashindano mengi sana yanaendelea kati ya watoto siku hizi regarding having the cool stuff,kkuvaa nguo kama jay zee, and sporting hot make-up or accessories. Many kids will resort to stealing as a response to this phenomenon.

  Sometimes kids even steal for the sense of excitement it gives them, or do it under peer pressure. A big part of the problem is that our society’s message is completely absent of a strongly objective morality. In most movies and songs today, the bad guys do good things and the good guys do bad things, and everybody looks the same. So kids justify what they’re doing. It’s not surprising when kids develop these ambivalent feelings about integrity, character and the difference between right and wrong.
   
 13. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #13
  Feb 7, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,262
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Thanks
   
 14. MUREFU

  MUREFU JF-Expert Member

  #14
  Feb 7, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,230
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  kwan shule czimeanza mpeleke bodi ili akaalibike vzur awe jambaz kwanini uumize kichwa ka2pe bodi huko
   
 15. Chizi Fureshi

  Chizi Fureshi JF-Expert Member

  #15
  Feb 7, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,710
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Watchout! Atapigwa kiberiti soon. Strongly mwonye ukimdekeza,utampoteza.
   
 16. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #16
  Feb 7, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,262
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Thanks
   
 17. m_kishuri

  m_kishuri JF-Expert Member

  #17
  Feb 7, 2011
  Joined: Jan 27, 2010
  Messages: 1,489
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Pole sana ndugu yangu kwa mkasa huo, lakini nadhani haujatupa picha kamili ya huyu mkasa. Kwa mfano, haujatueleza mama wa huyo mtoto yupo wapi na uhusiano wake na mtoto uko vipi. Upo uwezekano mkubwa kwamba wazazi wake wawili hawana uhusiano mzuri (may be a messy divorce) ndio maana huyo mtoto anafanya hivyo vitendo ili kuseek attention.

  Mara nyingi utaona kwamba watoto wengi ambao wanaingia balehe wakati wazazi wao wanafaraka (DIVORCE) huishia kujiingiza kwenye mambo kama haya, haswa kwa wavulana, wakati watoto wa kike wanajiingiza kwenye umalaya na pia udokozi. Kama mama yake mzazi yupo, basi na yeye ashirikishwe katika utatuzi wa hilo tatizo, vinginevyo atafutiwe mganga wa psychologia ili na yeye ajaribu.
   
 18. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #18
  Feb 7, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,262
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Kaka yangu aliachana na mama yake huyu mtoto akiwa ana miaka ka miwili, akalelewa na bibi yake ambaye ni mama yetu tukawa wote tunakaa naye home pamoja na baba yake. Sasa mama yetu alipofariki familia ikasambaratika kila mtu akaenda kwake, ndo akachukuliwa na dada yetu mkubwa akawa anakaa naye tabia ya wizi ilianzia hapo, alizungukwa na watoto rika lake wote vichwa shuleni hata yeye anajitahid masomo na amefaulu kwenda shule ya kata!. Dada mkubwa alipomfukuza akaja kwa dada yetu mdogo mambo yaleyale. Ok tatizo linaweza likawa kwa kaka yangu maana amezaa watoto lakini hawajari ndo maana ndugu wakawa wanakaa naye, mda huu alikuwa kwa baba yake ndo anazidi uwizi naye hajui amfanye nini ndo leo kamleta kwangu, mama yake mtoto hajari mi sijawahi muona last time I checked it was 15 years ago!
   
 19. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #19
  Feb 8, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Mjengeeni mazingira ya upendo halafu hakikisheni anapata mahitaji yake yote muhimu.
  Inawezekana nyie ndio mnamfanya awe mwizi kwa kujijali wenyewe halafu yeye mnampotezea.
  Mahitaji muhimu unayajua ila kulala na kulala tu haitoshi.
  Kaeni nae mmuulize ni kitu gani angependa kufanya au kama kusoma ni shule gani mumtaftie.
  Mtafutieni mshauri awe nae karibu. Inawezekana nyie akawa anawaogopa kuwaeleza ila mtu wa nje akawa huru kuongea nae matatizo yake.
  Poleni sana.
   
Loading...