Mtoto Mwingine wa Miaka 9 Abadili Jinsia Uingereza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto Mwingine wa Miaka 9 Abadili Jinsia Uingereza

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Dr. Chapa Kiuno, Sep 24, 2009.

 1. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0


  Mtoto wa kiume wa miaka 9 abadili jinsia kuwa mwanamke
  Tuesday, September 22, 2009 3:55 AM
  Baada ya mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 12 kubadili jinsia kuwa mwanamke nchini Uingereza mtoto mwingine wa kiume mwenye umri wa miaka 9 na yeye amebadili jinsia kuwa mwanamke.


  Baada ya taarifa za mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 12 kuanza elimu ya sekondari akiwa amebadili jinsia yake kutolewa kwenye vyombo vya habari wiki iliyopita na kuzua mtafaruku nchini Uingereza, mtoto mwingine wa kiume mwenye umri wa miaka tisa amerudi kwenye shule yake ya msingi kutoka likizo akiwa amebadili jinsia kuwa mwanamke.

  Tukio hilo pia kama lile la awali limetokea kwenye mji mmoja kusini mwa Uingereza.

  Wanafunzi katika shule ya msingi anayosoma mtoto huyo wa miaka 9 waliambiwa kuwa mwanafunzi mwenzao wa kiume amehama shule na nafasi yake imechukuliwa na mwanafunzi mwingine wa kike.

  Lakini wanafunzi wanaomjua vizuri mtoto huyo walirudi majumbani mwao na kuanza kuwauliza maswali wazazi wao kwanini mwenzao ameamua kuvaa nguo za kike.

  "Mwanangu alirudi toka shuleni na kuniuliza kwanini rafiki yake mmoja amekuwa msichana, mwanzoni nilidhani anatania lakini aliendelea kunisumbua kwa swali hilo na kunifanya nitie shaka inaweza kuwa kweli", alisema mzazi wa mtoto mmoja katika shule hiyo.

  Hata hivyo baada ya kuona wanafunzi wamegundua kuwa mwanafunzi huyo ndio yule yule wa awali ma wala hakuhama shule, walimu waliwakusanya wanafunzi wote na kuwataarifu kuwa mwanafunzi mwenzao amebadili jinsia amekuwa mwanamke na waliwataka wanafunzi wote waanze kutumia jina lake jipya la kike ambalo lilibandikwa kwenye ubao wa matangazo wa darasa lake.

  Wazazi wa wanafunzi katika shule hiyo ya msingi walikasirishwa na hatua ya mwalimu mkuu wa shule hiyo kuwapa taarifa hiyo watoto wao kabla ya kujadiliana nao kwanza.

  "Sijui nitajibu vipi maswali ya mwanangu wa kiume, ni mdogo sana na hajui chochote kuhusiana na masuala ya jinsia", alilalamika mmoja wa wazazi wa mwanafunzi wa shule hiyo.

  "Sijui nitasemaje kama na yeye akisema kuwa anataka kubadili jinsia kuwa kama rafiki yake", alilalamika mzazi huyo.

  Kitendo cha mtoto wa miaka tisa kubadili jinsia kuwa mwanamke kimechochea moto kwenye mjadala mkali uliozuka baada ya taarifa za mtoto wa miaka 12 kubadili jinsia kutolewa katikati ya wiki iliyopita.

  Taarifa hiyo ilisababisha wazazi wa mtoto huyo kupewa ulinzi kutokana na vitisho vya kuuliwa walivyokuwa wakitumiwa na watu wasiojulikana wanaopinga kitendo hicho.
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  hIVI HII DUNIA NDO INAELEKEA UKINGONI AU INAKUWAJE MAANA MAMABO YANAYOTENDEKA NI MAGUMU NA YA KUTISHA.

  1. Kwanza mtoto wa miaka tisa ni mdogo sana mpaka yeye mwenyewe atoe maamuzi ya kubadili jinsia

  2. na hao ma DR wanaomfanyia operation hizo akili zao sijui kama zinakuwa sahihi .
  sitaki hata kuamini kambo hili
   
 3. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wazungu wehu wakati mwengine.
   
 4. D

  Darwin JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  Si watu wengine wanawaona wazungu kama Miungu!?


  Hii style ya Europe isije ikasambaa dunia nzima.
   
 5. K

  Kicheche Member

  #5
  Sep 24, 2009
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 46
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  wazazi wa hao watoto pamoja na viongozi wa serikali yao ambao wanafumbia macho ushenzi huo wote ni wendawazimu
   
 6. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280

  na kweli bwana naona hata wazazi ni mataahira kama huyo aliyesema hapo juu
  wazungu sometimez hamnazo
   
 7. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #7
  Sep 24, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  huyo mtoto hajabadilisha jinsia, amebadilishwa jinsia, mtoto wa miaka tisa kuna uwezekano mkubwa sana kujutia uamuzi huo pindi atakapoanza kubanduliwa na vijeba. hayo ndiyo mazao ya kutetea haki za ushoga.
  naipenda Tanzania
   
 8. J

  JackieJoki Member

  #8
  Sep 24, 2009
  Joined: Sep 24, 2009
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  I totally agree with you 100%
   
 9. K

  Kagoma Member

  #9
  Sep 24, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  May be that is what they call "Children Rights" in Europe!
   
 10. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #10
  Sep 24, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ha ha ha! yah ryt mkuu
   
 11. m

  mafanikio Member

  #11
  Sep 24, 2009
  Joined: Jul 23, 2009
  Messages: 51
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 15
  kuhusiana na hili ninapenda kabisa kuwasihi watanzania wenzangu ninajua kabisa BAADHI YETU hupenda kuiga kila kinachotoka kwa Ulaya jamani jamani tuanze kuchagua yapi ya kuiga na yapi ya kuyaacha yapite.

  nimefarijika sana na baadhi ya wachangiaji hapo juu kwa kukemea jambo hili ambalo halipendezi na ni fedhea kwa taifa kubwa na lililoendelea kama hilo, ila ninawaomba tujaribu kutumia lugha zilizostarabika ili hata hao wanaosoma kwa lengo la kupata habari na kujifunza waweze kutuelewa ila kila mtu akikemea kwa lugha isiyokuwa ya kistaarabu wot tutaonekana hamnazo na hatuna tofauti na hao wanaoendeleza kumkosoa Muumba na kuona wanaweza kubadili jinsia zao kila watakapo kwa kifupi naweza kusema hali hii inachangiwa na mambo makubwa manne kama ifuatavyo:
  1. Jeuri ya fedha ambazo mtu anazo hajui afanyie nini, zaweza kuwa za halali ama lah? maana fedha ya halali mara nyingi Mungu humpa mtu hekima ya kuitumia.
  2. ninasitita kukubali kuwa hao wazazi kweli wamesoma au wamemaliza madarasa? kama ni wamesoma basi wamekusanya vyeti ila hawakuelimika kabisa.
  3. Hao wazazi, madaktari na baadhi ya walimu waliokubaliana na jambo hilo naweza kusema hawa hofu ya Mungu ndani yao hata kama ni waumini basi wanaenda kujaza viti huko wanakoabudu, sipaswi kuhukumu ila ninamashaka na imani zao.
  4. ni ulimbukeni wakutaka umaarufu kumbe si kila umaarufu ni mzuri. umaarufu mwingine kama huu unawafanya watu wenye busara zao kuwatoa maanani na kuwaweka katika kundi maalumu lenye kuitaji msaada wa kisaikolojia.

  ninaomba niishie hapo nikikubali kukosolewa na kuendelea kujifunza kutoka kwa wengine. ila tusiige kabisa upuuzi huu maana si kwa watoto tu hata sisi watu wazima baadhi yetu tunaweza kuona na haya ni maendeleo ya kuiga ni aibu na upuuzi mtupu.
   
 12. h

  hatmoh Member

  #12
  Sep 24, 2009
  Joined: May 20, 2008
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh! Yaani nimejiuliza maswali kibao bila jibu la msingi.
  Labda alikuwa na jinsia 2 sasa hiyo ya kike ndio iko active! Au labda wamepata watoto wote wa kiume wanataka wa kike... ha ha ha... kwa kifupi sielewi. Hawa watu ni watata...!
   
 13. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #13
  Sep 24, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hawa wazungu jmn
   
Loading...