Mtoto Mwenye Akili Kuliko Wote duniani Aweka Rekodi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto Mwenye Akili Kuliko Wote duniani Aweka Rekodi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jul 11, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mtoto Elise Tan Roberts Saturday, May 02, 2009 1:52 AM
  Mtoto wa miaka miwili ambaye alianza kuzungumza alipokuwa na umri wa miezi nitano na kuanza kutembea akiwa na miezi minane ameweka rekodi kwa kuwa mwanachama mdogo kuliko wote kuingizwa kwenye jumuiya ya watu wenye akili na upeo usio wa kawaida ya MENSA Mtoto Elise Tan Roberts mwenye umri wa miaka miwili ambaye IQ yake imepishana kidogo na IQ ya mwanasayansi nguli wa fizikia Albert Einstein amekuwa ndio mwanachama mdogo kuliko wote kuingizwa kwenye jumuiya ya watu wenye akili sana zisizokuwa za kawaida inayoitwa MENSA.

  Ili kuwa mwanachama katika jumuiya ya MENSA inabidi mtu ufaulu kwa asilimia 98 au zaidi katika mtihani maalumu wa IQ.

  Elise alianza kuzungumza alipokuwa na umri wa miezi mitano na kuanza kutembea alipofikisha miezi nane na hivi sasa akiwa na umri wa miaka miwili ana uwezo wa kutaja miji mikuu 35 duniani, kutaja na kuzipanga alphabet na kutaja majina yote ya maumbile ya pembe tatu.

  "Huongea vitu ambavyo hukuacha mdomo wazi ukifikiria amevitoa wapi" alisema mama yake Louise mwenye umri wa miaka 28.

  "Anapenda kujifunza vitu na huvishika katika muda mfupi".alisema mama yake.

  Mensa walithibitisha kwamba akiwa na umri wa siku 845 ( Miaka miwili na miezi minne) , Elise ndiye mwanachama mdogo kuliko wote wa Mensa, akimpiku Ben Woods, aliyeingizwa kwenye jumuiya ya Mensa alipokuwa na umri wa 1,035 mwaka 1990.

  IQ ya Elise ni 156 wakati mwanasayansi mkongwe wa fizikia Albert Einstein maarufu kwa kanuni yake ya nishati ya
  E = mc2
  alikuwa na IQ ya 160.


  nifahamishe.com
   
  Last edited by a moderator: Jul 11, 2009
 2. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  huyu mtoto aliwashangaza wengi sana, ingekuwa huku kwetu waswahili wangesema ni uchawi, maana kuna kitoto kiliwahi kuzaliwa huku kikiongea lughakibao mama yake akatengwa na jamii.
   
 3. O

  OkSIR Senior Member

  #3
  Jul 11, 2009
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyo miezi 5 anaogea huyu dar katoka anaulzia uji...
   
 4. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #4
  Jul 11, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Sasa jamani si kalizaliwa kakiwa na njaa, wewe ulitaka asemeje?

  Vipi na kale katoto kaliko zaliwa Russia!?
   
Loading...