Mtoto mmoja kati ya mapacha waliotoka kutenganishwa Saudi Arabia, amefariki dunia

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mtoto Anisia Bernatus mmoja wa mapacha waliorejea nchini siku chache zilizopita kutoka nchini Saudi Arabia walipokuwa wamepekekwa kufanyiwa upasuaji wa kuwatenganisha amefariki dunia katika hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu
*****

Anisia, pacha aliyetenganishwa na mwenzake Melnes baada ya kuzaliwa wakiwa wameungana amefariki dunia jana Jumatatu Septemba 2, 2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), ikiwa ni nne tangu waliporejea nchini Tanzania kutoka Saudi Arabia walikofanyiwa upasuaji.

Akizungumza leo Jumanne Septemba 3, 2019 mkurugenzi wa huduma za upasuaji wa MNH, Dk Suphian Baruan amesema Anisia amefariki jana usiku wakati madaktari wakimpatia matibabu.

“Kama mnakumbuka tangu siku walivyorudi mmoja alionekana kuwa na tatizo, madaktari waliliona hilo na kuanza kumfanyia uchunguzi na matibabu ila nasikitika kuwataarifu kuwa amefariki,” amesema Dk Baruan.

Akizungumzia chanzo cha kifo cha mtoto huyo daktari bingwa wa upasuaji wa watoto, Petronilla Ngilino amesema wakati wanaendelea kumfanyia uchunguzi alianza kutapika.

“Ile hali ya kutapika ilitushtua lakini baada ya kumuuliza mama yake akasema alianza kutapika tangu wakiwa kwenye ndege na akawa ameishiwa nguvu.”

“Tukaanza kumuwekea maji kwa kuwa yalikuwa yanapungua, na tukazuia matapishi yasiingie kwenye mfumo wa hewa. Tuliendelea na uchunguzi tukabaini kuna tatizo kwenye tumbo lake,” amesema Dk Ngilino.

Amesema utumbo wa mtoto huyo ulikuwa umejifunga ndipo walipofikia uamuzi wa kumfanyia upasuaji kurekebisha hilo.

“Tulifanikisha upasuaji na alipopelekwa ICU (Chumba cha Uangalizi maalum) tukaanza kuona upokeaji wake wa hewa ya oksijeni si mzuri licha ya kusaidiwa kupumua na mashine, tulijaribu kuokoa maisha yake ila usiku wa jana akatutoka,” amesema.
 
Mtoto Anisia Bernatus mmoja wa mapacha waliorejea nchini siku chache zilizopita kutoka nchini Saudi Arabia walipokuwa wamepekekwa kufanyiwa upasuaji wa kuwatenganisha amefariki dunia katika hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.
Pole sana kwa ndugu, na jamaa wa marehemu. Mwenyezi Mungu akawape nguvu hasa wazazi wake. Hakuna jambo gumu kwenye hii dunia kama mzazi kuzika mtoto.
 
Waarabu walimchoma sindano ya kufikia Tanzania au?
IMG-20190617-WA0000.jpg
 
Madoctor Bingwa nchi za Kiarabu ni Wahindi, hata Waarabu wenyewe hawawaamini Madoctor wa Kiarabu....

Sitaki kuuliza kwa nini hawakwenda India.... Yote ni kazi ya Mungu.
 
Bora wangebaki tu huko huko hadi changamoto zote zinazowakabili ziishe kabisa. Pole nyingi kwa wanafamilia.
 
Poleni Sana
Juhudi Zilifanyika Ila Mungu Ni Mwema Wakati Wote
Kampenda Zaidi
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom