Mtoto miezi mitano atelekezwa nje ya nyumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto miezi mitano atelekezwa nje ya nyumba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 7, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MTOTO anayekadiriwa kuwa na umri wa miezi mitano, ameokotwa akiwa ametelekezwa nje ya nyumba ya mtu huku mama wa mtoto huyo akiwa hajulikani.

  Mtoto huyo aliokotwa usiku wa manane wa kuamkia jana katika mtaa wa Itongo jirani na chanzo cha maji cha mto Nzovwe katika kata ya Mwakibete jijini Mbeya.

  Mashuhuda wa tukio hilo, walisema majira ya saa nane walisikia sauti ya mtoto akilia nje ya nyumba ya mkazi mmoja wa kitongoji hicho, aliyefahamika kwa jina moja la Mama Beather lakini kwa kuwa nyumba hiyo ipo jirani na njia wakajua kuna mtu aliyekuwa naye.

  Mashuhuda hao walisema tofauti na matarajio yao, mtoto huyo aliendelea kulia hali iliyosababisha mama mwenye nyumba hiyo kutoka nje na kumkuta akiwa ametelekezwa mbele ya nyumba yake.

  Baada ya kumkuta mtoto huyo, mama huyo aliwaamsha majirani walioungana naye kumkagua mtoto huyo wa jinsia ya kiume aliyekuwa amevalishwa nguo vizuri na hakuwa na jeraha lolote.

  “Tulijaribu kuulizana iwapo kuna mtu kati yetu anayemtambua mwanamke yeyote aliye na mtoto wa umri huo, lakini baadaye tukaridhia kwamba katika eneo letu au jirani hakukuwa na mtu anayeweza kuwa mama au baba wa mtoto huyo,” alisema mmoja wa mashuhuda aliyeomba kutotajwa jina lake gazetini.

  Alisema baada ya kubaini kutokuwepo kwa mzazi wa mtoto huyo, walikubaliana kwa pamoja na askari polisi Nasibu Njozi anayeishi mtaani hapo, kumpeleka kituo cha polisi.
   
Loading...