Mtoto miaka 14 auawa kwa Wivu wa Mapenzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto miaka 14 auawa kwa Wivu wa Mapenzi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwitongo, Aug 13, 2012.

 1. Mwitongo

  Mwitongo JF-Expert Member

  #1
  Aug 13, 2012
  Joined: Jan 30, 2009
  Messages: 311
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu, someni hapo kwenye RED!!!!


  Na Luppy Kung’alo wa Jeshi la Polisi Dodoma.

  DODOMA JUMATATU AGOSTI 13, 2012. Mwanafunzi wa Darasa la Saba shule ya msingi Hogolo, aliyefahamika kwa jina la Matha Mazoea Mwenye umri wa Miaka (14) ameuawa kwa kunyongwa na kufukiwa kwenye shimo nyuma ya nyumba yao karibu na choo baada ya kubakwa.
  Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Zelothe Sephen alisema tukio hilo limetokea mnamo tarehe 11/08/2012 majira ya saa 08:00 asubuhi katika mtaa wa Ikulu Kijiji cha Hogolo Kata ya Hogolo tarafa ya Zoisa Wilaya ya Kongwa.
  “Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi kwani marehemu alikuwa amevunja uhusiano na mpenzi wake wa muda mrefu aliyejulikana kwa jina la Heri Aboubakar na kuanzisha uhusiano na mpenzi wake mpya aliyefahamika kwa jina la Wilfredy Muhaha @ Kabo mwenye miaka (17) “ Alielezea Kamanda Zelothe


  Katika tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji hayo ambao ni Asha Jafari Mohamed mwenye umri wa miaka 16, mkulima, mkazi wa Mtaa wa Nyerere Hogolo ambaye ni rafiki wa marehemu na Rino Mazoea mwenye umri wa miaka 21, Mkulima, Mkazi wa Ikulu Hogolo Wilayani Kongwa ambaye ni kaka wa marehemu.

  Bw. Zelothe alieleza kwamba ili kufanikisha uchunguzi wa awali Jeshi la Polisi pia Wilayani humo linamshikilia mpenzi mpya wa marehemu Bw. Wilfredy s/o Muhaha pamoja na kumtafuta mpenzi wa zamani wa marehemu Bw. Heri s/o Aboubakar ambaye amekimbia kijijini hapo na hajulikani alipo mpaka sasa.  Aidha kamanda Zelothe alisema Katika tukio hilo Kaka wa marehemu ambaye anashikiliwa na Jeshi la Polisi, katika maelezo yake ya awali alidai kusikia purukushani zikitokea usiku wa tukio hilo la mauaji lakini hakuweza kutoka usiku huo ili kushuhudia nini kinaendelea.
  Kamanda Zelothe alisema Marehemu alikuwa akiishi na babu na bibi yake hapo Kijijini na kwamba siku ya tukio walikuwa wameondoka kwenda katika Vijiji vya jirani, ambapo bibi yake na marehemu alikuwa amekwenda Kongwa kwa ajili ya kujengea makaburi na babu yake alikwenda kijiji cha Banyi banyi kwa Shughuli za kutemebelea wagonjwa.
  Wakati huo huo Gari lenye namba za usajili T. 750 AEU aina ya TOYOTA CHASER likiendeshwa na Kenedy James mwenye umri wa miaka 48, Mkazi wa Mpwapwa liliacha njia na kupinduka na kusababisha kifo cha Salum Kaduma mwenye umri wa miaka (13) Mwanafunzi wa kidato cha kwanza Katika shule ye sekondari ya Mpwapwa, na kusababisha kifo chake.

  Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma alisema ajali hiyo ilitokea mnamo tarehe 12/08/2012 majira ya saa 09:00 asubuhi katika eneo la Kisima Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.
  “Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka kwa magurudumu mawili ya upande wa kulia kitu kilichopelekea gari hilo kuacha njia na kupinduka.” Aliongeza Bw. Zelothe

  Mwisho:

  CONTACT:

  POLISI MKOA WA DODOMA

  DAWATI LA HABARI, ELIMU NA MAHUSIANO,

  Phone: 0715 006523, Luppy Kung’alo – Mrakibu msaidizi wa Polisi (ASP)

  Phone: 0712 360203, Silyvester Onesmo – Police Konstebo (PC)
   
 2. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,076
  Likes Received: 1,812
  Trophy Points: 280
  Ukiistajabu ya Mussa.....
   
Loading...