Mtoto miaka 14 atwanga wazazi risasi kwa kutumwa kazi za nyumbani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto miaka 14 atwanga wazazi risasi kwa kutumwa kazi za nyumbani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Jan 27, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,155
  Trophy Points: 280
  COLORADO,Marekani

  MTOTO wa kiume raia wa hapa mwenye umri wa miaka 14 anadaiwa kuwaua wazazi wake kwa kuwapiga risasi baada ya kuagizwa kufanya kazi ndogondogo za nyumbani.

  Kwa mujibu wa nyaraka za mahakama, mtoto huyo, John Caudle, alikuwa amekasirika kwa siku mbili baada ya kuambiwa na wazazi wake kusafisha chumba chake na kuchambua maharage.

  Imeelezwa kuwa baada ya hasira na kusongwa na mawazo zaidi mtoto huyo alimtwanga risasi mama yake, Joanne Rinebarger (38), wakati akiangalia televisheni na kisha kumtwanga risasi ya kisogoni baba yake wa kambo aliyetajwa kwa jina la Tracy wakati akirejea kutoka kazini.

  Nyaraka hizo zimeeleza kuwa Caudle alidai kuwa baada ya kufanya mauaji hayo alicheza michezo usiku kucha wakati maiti za wazazi wake zikiwa zimelala sakafuni.

  Katika nyaraka hizo za mahakama imeelezwa kuwa ilipofika asubuhi mtoto huyo aliendesha gari la baba yake hadi shuleni ambapo walimu wanasema alikuwa akionekana mwenye furaha kabla ya ndugu zake kuzikuta maiti nyumbani kwao katika eneo la Fairplay, Colorado.

  Imeelezwa kuwa licha ya kuwa na umri huo mdogo, Caudle amefunguliwa mashitaki ya mauaji kama watu wazima.

  Nyaraka hizo za mahakama zimeeleza kuwa Caudle alidai sababu iliyomfanya kumpiga risasi mama yake, Joanne Rinebarger ni kwa kuwa hakutaka kufanya kazi za nyumbani.
   
 2. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Nafikiri si kusafisha chumba tu kulikomfanya kijana afikie maamuzi ya kuwatwanga risasi wazazi wake hao wawili, nafikiri ni siku nyingi hawakuwa na mapenzi na mtoto huyu ukizingatia yule jamaa si baba yake mzazi - sasa kijana aliona ametengwa so kuchanganya na hasira za kutumwa tumwa akaamua kuwafumua risasi.

  Cha kujifunza hapa ni kuwa makini sana na vijana wa umri wa 12 -20 hapa ndiyo kwenye matatizo makubwa.

  Haya siyo yapo mbali Yanakuja bongo karibuni - ukijifanya baba mnoko mnoko unatwagwa risasi. - matunda ya utandawazi ngoja tusubiri itakavyokuwa next 10 years.

  Cha msingi ni kujiandaa kikamilifu na huu utandawazi - na hizi games na movies wanazoangalia hawa watoto mmhh
   
Loading...