Mtoto mdogo wa kiume wa Gadafi ajiunga na maandamano

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
266
Mwana mdogo wa kiume wa kiongozi wa Libya Muammar Gadafi jana alijiunga na wananchi wanaoandama kuupinga utawala wa baba yake huko magharibi mwa nchi hiyo. Ripoti zinaarifu kuwa Saif al Arab mwana mdogo wa kiume wa Gaddafi ambaye alitumwa na baba yake kushirikiana na vikosi vya usalama kuyakandamiza maandamano ya wananchi wanaopigania demokrasia huko Libya jana alijiunga kwenye maandamano huku akidokeza kuwa baba yake huenda akajiuwa au kukimbilia Amerika ya Latini. Hadi kufikia sasa Walibya wasiopungua elfu moja wameuwa na vikosi vya Gadafi. Aidha jumla ya askari jeshi 130 wameuawa huko Libya kwa kukataa kwao kuwafyatulia risasi waaandamanaji.
Huku hayo yakiripotiwa balozi wa Libya nchini Jordan amejiuzulu wadhifa wake huo katika kupinga ukandamizaji na utumiaji nguvu unaofanywa na vikosi vya Gaddafi dhidi ya wafanya maandamano nchini humo. Mohammad Hassan Barghathi ametangaza kujiuzulu wadhifa wa ubalozikutokana na matukio yanayojiri sasa huko Libya.
Mtoto mdogo wa kiume wa Gadafi ajiunga na maandamano ya wananchi
 
huyo tayari na kwa kuwa anaondolewa kwa kuuwa watu, hata kama hatajiua, akakimbia-atakamatwa na kushitatakiwa kwa genocide naye pia.
 
Huyu kijana ni mwanaume kweli...baba mpuuzi wa kazi gani! Km kumbu kumbu zangu ziko sawa aliwahi kufukuzwa na babake akaishi Misri kwa kitambo...
 
Huyu Gadafi wiki tatu zilizopita alikuwa anamuangalia H Mubaraka alivyokuwa
anapelekwa kasi na nguvu ya umma....

Kamwe hakutegemea this soon atakuwa hapo alipo...

...sina maana hiyo...

..Ninamaanisha hapa nyumbani ..how soon are you going to work for the good of your own peolple and stop playing with the power we gave you ie Downs and all the other corruptions at the top leader ship?
.. Mnafikiri umma wa Tanzania hauwezi kufikia ..hayo yanaotokea hapo uarabuni?
..ajitokeze mtu abishe kwa dhati tumuone..!!
 
Wakujiuliza ni huyu bwana...kwenda kurubuni wazee wanaojilia pensheni ya karata zao za ujana kuja "kukagua mitambo yake"...siku ikifika hii mitambo ndiyo ya kwanza kutiwa kiberiti...haiwezi kumaliza vichwa vya habari kila kukicha bila hatua yoyote kuchukuliwa
 
Mkwere humpendi nini mbona haumtahadharishi nae atafute pa kukimbilia na jopo lake tumechoka na maisha haya magumu ya shida na taabu nyingi
SALAMU KWA MKWERE NA WEZI 400: Wakiona wenzao wananyolewa, wao watie maji. Ikiwa Ben Ali na Mubarak walinyolewa kwa mashine, na Gadafi ananyolewa kwa kiwembe, wao wakae tayari kwa kigae cha chupa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom