Mtoto mdogo kukosa hamu ya kula!

Omumura

JF-Expert Member
Aug 20, 2009
476
18
Wakuu, naombeni msaada wenu wa mawazo na ushauri, kwani nina mtoto mdogo wa mwaka na miezi kumi hivi kula kwake ni kwa shida sana mpaka umlazimishe na analia sana, hali hiyo ni kila siku hasa inapofika wakati wa kula.

Akipimwa wakati mwingine hana malaria!
 
Inawatokea sana watoto hali hii, na itadumu muda tuu, utakuta atamaliza hadi mwaka tena anasumbua kinyama kula...Sidhani kama ni matokeo ya ugonjwa fulani, ila naamini ni katika steji za kukua.

Lakini nijuavyo huko mbele atakuja piga sembe huyo hadi akutie hasara!...sijui huwa wanalipiza..!
 
Nakushauri umpeleke kwa daktari wa watoto,atakushauri nini cha kufanya,pia kuna uwezekano akawa na minyoo,si vibaya ukampa dawa ya minyoo ili kujiridhisha.
 
Inawatokea sana watoto hali hii, na itadumu muda tuu, utakuta atamaliza hadi mwaka tena anasumbua kinyama kula...Sidhani kama ni matokeo ya ugonjwa fulani, ila naamini ni katika steji za kukua.

Lakini nijuavyo huko mbele atakuja piga sembe huyo hadi akutie hasara!...sijui huwa wanalipiza..!

Ni kweli watoto wengi uwatokea sana hali hii.Wangu mie ukimkuta analishwa utafikiri ugomvi.
 
Pole sana.. Mimi wangu alikuwa hivyo na nilisumbuka sana, nilizunguka mahospital mengi tofauti kwa ushauri, lkn haikusaidia kitu. Alikuwa anamaliza chakula kidogo kwa mfano wa KONZI moja kwa karibu 5-6 hrs. Ila hivi sasa, analipiza kama alivyosema Mkuu PAKAJIMMY.. Anafukia kama katoka jela.... Jitahidi kumlisha hivyo kidogo kidogo. usegeze umri..
 
Omumura,
Pamoja na kumpima minyoo, kumbadilishia aina ya vyakula mbalimbali vya laini, nashauri umpe MAFUTA YA SAMAKI yenye ladha ya machungwa. Hii watoto huipenda sana kutokana na ladha yake. Ina ina vitamin ambayo itamuongezea hamu ya kula. Nimelea watoto na sasa wajukuu, hii dawa ndio inayowalisha.
 
umejaribu kumcheki U.T.I?watoto wengi wanapata hii mara anashinda kacheza vzr but jion home,utapima malaria mpaka uchoke kumbe tatizo ni mkojo maana wanakaa sana na ma haus gals,pemba hawabadilishwi on time,au kama ni pot haioshi vizuti au anajisaidia hawamwagi,ol these are sources za U.T.I inafanya watoto wakose ham ya kula pia nakuwa yupo yupo tu haeleweki,yaribu kwenda hsp kufanya culture ya mkojo,pole
 
Back
Top Bottom