Mtoto mchanga atolewa kwenye kifusi Nairobi akiwa hai

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Mtoto.jpg

Mtoto wa umri wa mwaka mmoja unusu amepatikana akiwa hai kwenye vifusi vya jengo lililoporomoka Ijumaa jijini Nairobi.

Jengo hilo la ghorofa sita liliporomoka katika mtaa wa Huruma baada ya mvua kubwa kunyesha.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, msichana huyo alitolewa kwenye vifusi mwendo wa saa kumi usiku na kukimbizwa hospitalini.

Kamanda wa kitengo cha taifa cha kudhibiti majanga Pius Maasai anasema hali ya mtoto huyo ni thabiti, kwa mujibu wa gazeti hilo.

Watu 22 wamethibitishwa kufariki na wengine karibu 90 hawajulikani walipo.

Juhudi za uokoaji bado zinaendelea siku ya nne baada ya mkasa huo kutokea.

Kufikia sasa, watu 136 wameokolewa.

Polisi wanasema wamiliki wa jumba hilo, ambalo maafisa wa baraza la jiji wanasema halikufaa kuishi watu, wamekamatwa na wanazuiliwa na polisi.

Taarifa zinasema watafikishwa mahakamani baadaye Jumanne.

Chanzo: BBC
 
Poleni waliofiwa na warehe.miwe waliotangulia mbele ya haki watoto ni malaika na ndio maana kwenye marukio ya ajabu utasikia mtoto kanusurika. Mungu anadhihirisha uwepo wake
 
Mamlaka za Serikali zetu za Afrika siku zote zina majibu ya ajabu sana, kwa nini basi waliruhusu jumba hilo kuhamiwa. Wakisema kwa sasa kuwa halikustahili kukaliwa walikuwa wapi
 
wow, what a good news! lakini hebu tuulizane, hilo jengo lilijengwa siku moja na kubomoka siku hiyohiyo? kwa nini wakamatwe wamiliki wa jengo hilo peke yao, as if it was built on no man's land? haki haijatendeka bado! hapo hata viongozi wa mamlaka walitakiwa nao waingizwe ndani! in Africa, we are victims of our own brothers & sisters
 
View attachment 344352

Mtoto wa umri wa mwaka mmoja unusu amepatikana akiwa hai kwenye vifusi vya jengo lililoporomoka Ijumaa jijini Nairobi.

Jengo hilo la ghorofa sita liliporomoka katika mtaa wa Huruma baada ya mvua kubwa kunyesha.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, msichana huyo alitolewa kwenye vifusi mwendo wa saa kumi usiku na kukimbizwa hospitalini.

Kamanda wa kitengo cha taifa cha kudhibiti majanga Pius Maasai anasema hali ya mtoto huyo ni thabiti, kwa mujibu wa gazeti hilo.

Watu 22 wamethibitishwa kufariki na wengine karibu 90 hawajulikani walipo.

Juhudi za uokoaji bado zinaendelea siku ya nne baada ya mkasa huo kutokea.

Kufikia sasa, watu 136 wameokolewa.

Polisi wanasema wamiliki wa jumba hilo, ambalo maafisa wa baraza la jiji wanasema halikufaa kuishi watu, wamekamatwa na wanazuiliwa na polisi.

Taarifa zinasema watafikishwa mahakamani baadaye Jumanne.

Chanzo: BBC
Pole sana kwa wote waliofikwa na mkasa huo. Waliolala Mungu Awape mapumziko ya amani. Waliojeruhiwa tunawaombea wapone haraka.
Angalizo mtoto wa mwaka mmoja siyo mtoto mchanga. Mtoto mchanga ni 'infant', mtoto wa mwaka mmoja na zaidi ni 'toddler'.
 
Kweli watoto ni malaika! Mungu amemlinda salama salimini. Amkuze ili aweze kuwasimulia watu matendo makuu ya Mungu
 
Back
Top Bottom