Uchaguzi 2020 Mtoto Mashaka na ndoto za kuwania urais 2020

Abdalah Abdulrahman

JF-Expert Member
Aug 29, 2019
222
201
Mzee James Ndalilwa na Anna Ndalilwa walijaaliwa watoto watatu,Mtoto wao wa kwanza alikua na jina la Sikudhani,Mtoto wa pili aliitwa Bahati na mtoto wa tatu alijulikana kwa jina la Mashaka.Wazazi hawa waliishi na kuwakuza watoto wao kwenye misingi ya kumcha Mungu,upendo mkubwa, usawa na huruma.Licha ya kuwepo na hali ngumu ya maisha iliyorithiwa kutoka kizazi na kizazi kwenye familia ya Mzee James.

Mzee James alifanya kazi kwa juhudu ili kuiondoa familia yake katika wimbi la umaskini ambao ulisabaishwa na mambo mbalimbali..ikiwa nipamoja na wanafamilia kutowajibika,matumizi mabaya ya kipato cha familia,wizi uliokithiri ambao miongoni mwa wanafamilia walishirikiana na majirani kuiba utajiri wa familia.

Baba James aliwahusisha wanae katika mambo mbalimbali ya kuimarisha pato la familia,aliwafundisha kazi na kuwasisitiza kufanya kazi,aliwapa mashamba ya kulima pamoja na vitendea kazi.Mzee James alimpa Sikudhani ambae ni mtoto wa kiume wa kwanza jukumu la kuwaongoza wenzake katika kuikomboa familia kutoka katika wimbi la umaskini.

Sikudhani alifanya kazi hiyo kwa umakini na uadilifu mkubwa,alifanikiwa kuondoa ubadhirifu,wizi,na kuboresha kipato cha familia kwa kiwango ambacho Mzee James aliridhika nacho.Maadui wa familia waliona wivu na kuanza kuwatumia baadhi ya wanafamilia kuhujumu juhudi za familia ya Mzee James.

Mashaka kwa kipindi chote cha kuijenga familia alikua ni sehemu ya mfumo wa upigaji na baada ya kuona fursa za wizi na ubafhirifu zilizokuwa zinamfaidisha yeye binafsi zimekatika alianza kubadilika tabia na kuwa mlevi,muongo,mzinzi na tamaa za utajiri wa haraka pamoja na uchu wa madaraka katika kusimamia mali za familia. Mashaka hakujali wake za watu mpaka watoto wa shule na vyuo licha ya kuwa na mke.

Mashaka hakujali kuficha siri za ndani ya familia na aliziuza kwa maadui wa familia kwa manufaa madogo na ya muda mfupi,Mashaka alifurahia majanga yaliyoipata familia na kujiondoa katika kuleta ufumbuzi. Ndani ya familia alianza kugombana na mama yake mzazi,baadae akaenda Kwa ndugu zake.

Mashaka alijenga uadui ndani ya familia na nje ya familia kiasi cha kutokua na amani hata yake mwenyewe.Siku moja Mashaka alimwarifu baba yake kuwa,kuna watu wabaya wanamfuatilia kwa nia ya kumdhuru.

Lakini kutokana na tabia za Mashaka za uongo,na kupinga kila ushauri mzuri aliopewa na watu wake wa karibu akiwemo baba yake pamoja na kaka yake mkubwa hakuchukua tahadhari yakutosha kutokana na watu hao wabaya waliotaka kumdhuru.

Haikupita muda mrefu Mashaka alishambuliwa na watu wasiojulikana kwa mishale mingi,baadhi ya mashuhuda walisema ni kisasi alilipizwa na rafiki yake aliyelala na mke wake,wengine wanasema ni ugomvi na yule rafiki yake waliokuwa wakihujumu pamoja pato la familia na pengine wamedhulumiana na wahalifu wenzake,au ametembea na mke wa mtu,au ni masuala ya visasi wao kwa wao.Majeraha yalikua makubwa na haikudhaniwa Mashaka anaweza kupona,ama hakika wale watu walikua na dhamira mbaya ya kumuua.

Kutokana na uwezo wa zahanati ya familia Mashaka alichukuliwa na marafiki zake aliokua akishirikiana nao kuhujumu familia yake kwa ajili ya matibabu,malipo ya matibabu yalikua makubwa na marafiki wakamkimbia.Kipindi chote cha matibabu ya Mashaka familia ilimpa ushirikiano mkubwa ikiwa ni pamoja na sala ili arudi nyumbani kuendelea na juhudi za kuijenga pato la familia.

Akiwa kwa marafiki zake baada ya kupona alianza kutumia wasaa huo kuihujumu familia kwa kuituhumu mambo mbali mbali,alifikia kumtukana baba yake na ndugu zake wengine.Akiwa anafanya yote haya alitoa sharti la kurudi nyumbani kuwa anataka ulinzi wa masaa 24.

Hii hadithi haihusiani na Lissu
 
Back
Top Bottom