Mtoto kupenda kutafuna kokoto ni tatizo gani?

Parachichi

JF-Expert Member
Jul 22, 2008
510
102
Wadau poleni na mashughuliko!kuna kitu kinanisumbua kichwa naombeni msaada wenu!hivi ni tatizo gani kwa mtu kupenda kula vijipande vya mawe?

kuna mtoto wa ndugu yangu anasumbuliwa na hilo tatizo!huwa anachukua vipande vidogo vidogo ya mawe anavitia mdomoni anakaa navyo hata usiku akilala anapendelea kumumunya kama pipi!ni tatizo gani hilo?na dawa yake ni nini?

Nawasilisha wakuu
 
Anakula vipande vya mawe au anachotaka ni ule mchanga tu unaopuputika kwenye hivyo vipande vya mawe? Je, anakula na mchanga?
 
Anakula vipande vya mawe au anachotaka ni ule mchanga tu unaopuputika kwenye hivyo vipande vya mawe? Je, anakula na mchanga?

Ndugu asante kwa msaada!huwa anachukua vipande vya mawe anavitia mdomon anamumunya kama pipi!vile vigumu na huwa anaviosha manake tulipopekua kwenye mfuko wake wa madaftari ya shule tulivikuta vingi visafiiiiiii!!!ina maana kabla ya kuvitia mdomoni huwa anaviosha kabisa!sasa hapo nashindwa kuelewa tatizo ni nini haswa!
 
Wadau poleni na mashughuliko!kuna kitu kinanisumbua kichwa naombeni msaada wenu!hivi ni tatizo gani kwa mtu kupenda kula vijipande vya mawe?kuna mtoto wa ndugu yangu anasumbuliwa na hilo tatizo!huwa anachukua vipande vidogo vidogo ya mawe anavitia mdomoni anakaa navyo hata usiku akilala anapendelea kumumunya kama pipi!ni tatizo gani hilo?na dawa yake ni nini?

Nawasilisha wakuu

Anaweza kuwa na eating disorder inayoitwa PICA, check hapa

http://en.wikipedia.org/wiki/Pica_(disorder) kwa hiyo waone wataalam wa

magonjwa ya watoto.
 
I had some kind of PICA when i was a pupil back then. Nilikuwa napenda sana kutafuna mkaa, ila nilikuwa siumezi. Nilikuwa tu navutiwa na ka-certain harufu na sio kila mkaa ulikuwa univutia.

I dont know how or when i started, and i dont remember how call a quiter..lakini sikutumia aina yeyote ya dawa..huenda ni matatizo flani tu ya muda. I am not sure.
 
Umesahau character moja ya mwisho kwenye link

http://en.wikipedia.org/wiki/Pica_(disorder)
 
Ohoo pole sana. Huyo mtoto ana ukosefu wa madini ya aina mbali mbali mwilini kama chuma nk pamoja na vitamins.

Kwa hiyo jaribu kuhakikisha mlo wake umekamilika yaani balanced diet. Hasa mpe nyama ya ngombe kwa wingi, matembele, mchicha nk.

Hili tatizo ni kama la mama mjamzito anayetafuna udongo.
 
Back
Top Bottom