Umri sahihi wa mtoto kuota meno

swtlady

Senior Member
Oct 22, 2013
156
102
Habari wakuu,ninataka kujua upi ni umri sahihi wa mtoto kuota meno, nasikia habari kuhusu natal na neonatal teeth ila sizielewi vizuri mwanangu ana umri wa miezi miwili na nusu na ameshaanza kuota meno.

Je ni plastic teeth au?

Na kipi cha kufanya kama ni hizo plastic teeth?

Kuota meno

Mtoto wako atakapofikisha miezi sita, ataanza kuota meno. Watoto wengine huanza

kuudhika kwani huumia kabla meno hayajatokea kwa ufizi. Watoto wengi humwaga mate sana na hutaka kutafunatafuna vitu. Wakati mwingine watoto hutapika au kuhara wakiota meno.

Kwa kawaida kuota meno hakufanyi mtoto kupandwa na joto. Kama mtoto wako atapata joto. Kama mtoto wako atapata joto, yaweza kuwa jambo lingine. Hakikisha umemwona daktari wa watoto.

Mawaidha wakati mtoto anaota meno

  • Wakati wa kulala, weka kitambaa safi chini ya kichwa cha mwanao ambapo ule utamwagika. Unaweza kibadilisha kitambaa hichi kitakapo loweka ute.
  • Mpatie mtoto kitu cha kutafuna ambacho hakitamdhuru. Usimpatie kitu kidogo sana kwani anaweza kukimeza. Unaweza kumpatia vidunde vya mpira visivyokuwa na majimaji ndani kwani vyaweza kupasuka. Unaweza kumpa kijiko cha mpira au kitambaa safi.
  • Usifungilie kidunde cha kutafuna kwa shingo ya mwanao. Kinaweza kushikwa na kummyonga.
  • Kuna dawa nyingi dukani za kupiunguza maumivu wakati mwanao anaota meno. Hata hivyo, mwone daktari wa watoto kabla jujampa mwanao dawa yoyote

Baada ya mwanao kuota meno hakikisha unayatunza
 
swtlady Neonatal teeth ni meno ambayo mtoto anazaliwa nayo na natal teeth ni meno yanayoota ndani ya mwezi mmoja wa mtoto kuzaliwa. Haya meno hayana uimara na hata mzizi wa meno haujishiki vyema kwenye fizi.

Wataalamu wanasema ni muhimu yakatolewa kwa sababu yanaweza kumzuia mtoto kunyonya na  kutokana na kukosa uimara yanaweza yakatoka mtoto akiwa ananyonya na kuleta madhara zaidi kama litamkaba.

Nenda kwa mtaalamu wa afya za watoto kwa ushauri zaidi.
 
swtlady Neonatal teeth ni meno ambayo mtoto anazaliwa nayo na natal teeth ni meno yanayoota ndani ya mwezi mmoja wa mtoto kuzaliwa. Haya meno hayana uimara na hata mzizi wa meno haujishiki vyema kwenye fizi. Wataalamu wanasema ni muhimu yakatolewa kwa sababu yanaweza kumzuia mtoto kunyonya na -kutokana na kukosa uimara yanaweza yakatoka mtoto akiwa ananyonya na kuleta madhara zaidi kama litamkaba. Nenda kwa mtaalamu wa afya za watoto kwa ushauri zaidi.

Kwahyo huyu mwenye 2 1/2 months ni sahihi kuota meno sijakupata vizuri
 
Mwanangu alianza kuota meno alipofikisha miezi kumi,na sasa ana mwaka na nusu ana meno mengi though bado yanaota
 
mtoto wangu alianza kuota meno akiwa na mwaka i was worried nikaambiwa ni kawaida wengine wanawahi kwanzia miezi mitatu ya mwanzo, kama mwanao ana miez 2na nusu sidhan kama kuna tatizo, ila jaribu kuonana na dentist wa watoto kwa ushauri zaidi.
 
Habari wakuu,ninataka kujua upi ni umri sahihi wa mtoto kuota meno.nasikia habari kuhusu natal na neonatal teeth ila sizielewi vizuri.mwanangu ana umri wa miezi miwili na nusu na ameshaanza kuota meno.je ni plastic teeth au? Na kipi cha kufanya kama ni hizo plastic teeth?
Kuota meno

Mtoto wako atakapofikisha miezi sita, ataanza kuota meno. Watoto wengine huanza

kuudhika kwani huumia kabla meno hayajatokea kwa ufizi. Watoto wengi humwaga mate sana na hutaka kutafunatafuna vitu. Wakati mwingine watoto hutapika au kuhara wakiota meno.

Kwa kawaida kuota meno hakufanyi mtoto kupandwa na joto. Kama mtoto wako atapata joto. Kama mtoto wako atapata joto, yaweza kuwa jambo lingine. Hakikisha umemwona daktari wa watoto.

Mawaidha wakati mtoto anaota meno

  • Wakati wa kulala, weka kitambaa safi chini ya kichwa cha mwanao ambapo ule utamwagika. Unaweza kibadilisha kitambaa hichi kitakapo loweka ute.
  • Mpatie mtoto kitu cha kutafuna ambacho hakitamdhuru. Usimpatie kitu kidogo sana kwani anaweza kukimeza. Unaweza kumpatia vidunde vya mpira visivyokuwa na majimaji ndani kwani vyaweza kupasuka. Unaweza kumpa kijiko cha mpira au kitambaa safi.
  • Usifungilie kidunde cha kutafuna kwa shingo ya mwanao. Kinaweza kushikwa na kummyonga.
  • Kuna dawa nyingi dukani za kupiunguza maumivu wakati mwanao anaota meno. Hata hivyo, mwone daktari wa watoto kabla jujampa mwanao dawa yoyote

Baada ya mwanao kuota meno hakikisha unayatunza

Subiri kidogo Madaktari Wa JF Wanakuja! @dr Dr.Mo MziziMkavu Et el
Mkuu Ibradehustler
 
Last edited by a moderator:
Mm wangu amechelewa kuota meno! Na sasa ana mwaka na miez 7 lkn ana vijino vinne tu! Juu viwili na chini viwili! Na hana dalili yakutoa jino lingine..ndo kibogoyo ama!
 
Salamu zenu wanajamvi, naomba kufahamu mwanangu ana miezi tisa na nusu hana jino hata moja, je yaweza kuwa anatatizo? Nimechanganyikiwa ni mwanangu wa kwanza.
 
nashukuru sana wadau nmewaelewa na mm mwanangu kaanza kuota meno kama miez miwil na nusu tareh 17/09 anatimza miezi 3
 
Naomba kufahamu ni umri gani sahihi ambao mtoto anatakiwa kuota meno maana kuna mtoto wa binamu yangu ana miezi kumi sasa lakini hakuna hata dalili ya jino kutokeza!
 
Naombeni msaada kwa yeyote anaefahamu kuwa mtoto anatakiwa kuota meno hadi awena umri gani(miaka mingapi)
 
miaka? mtoto anaanza kuota meno akiwa na miezi, wakwangu wote wameanza kutoka meno wakiwa na miezi 8
 
Usiwe na haraka sister ikifika mda wake yataota yenyewe hayo wengine wanawahi wengine wanachelewa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom