Mtoto kuongezeka uzito kwa haraka ni tatizo?

Kyenju

JF-Expert Member
Jun 16, 2012
4,561
1,500
Habari wadau, naomba tusaidiane katika hili. Ni mtoto wa kiume ana umri wa miezi 3, alizaliwa na uzito wa kilo 4 baada ya miezi 2 akawa na kilo 7 na sasa mwezi wa 3 amefikisha kilo 9.3.

Je hii imekaaje kiafya?
 

rosita

JF-Expert Member
Oct 18, 2013
482
250
Kwenye ile chat ya clinic akifikia kwenye red atakuwa na obesity....but kama yupo kwenye green au white besi yupo kawaida tu.
 

Kyenju

JF-Expert Member
Jun 16, 2012
4,561
1,500
Kwenye ile chat ya clinic akifikia kwenye red atakuwa na obesity....but kama yupo kwenye green au white besi yupo kawaida tu.

Yupo kwenye green mkuu, ila clinic walitoa onyo kuwa ongezeko la uzito ni kubwa.
 

LUPITA

Member
Mar 5, 2014
6
0
Sio kawaida, sio kawaida hata kidogo na asikudanganye mtu pia usiifurahie hali hiyo. hilo ni tatizo..mtoto akifikisha miezi 3 anatakiwa awe na double weight ya ile aliyozaliwa nayo. wakwako alitakiwa awe na kilo 6 kwakua alizaliwa na3. naomba kujua apart from maziwa ya mama anakula nn kingine bcoz watu huanza kuwapa watoto uji wa kuchuja akiwa na miezi 2 wengine 3. kama hivo ndo mnafanya mpunguzieni lishe....ammsaidii mtoto mnamletea matatizo ya kutokua vizuri, kuchelewa kutambaa na kutembea kwasababu ya uzito wa mwili na pia obedity, anaweza akawa kwene green but still is not good and its dangerouse ndo maana hata huko clinic wamewakataza. ushauri wangu, pelekeni mtoto kwa daktari wa watoto ongeeni nae kwa uwazi especially on his diet, atajua what to do na kama mtoto anatatizo litatatuliwa....

paliwai kutokea na mtoto wa miez 4 ukimwona ni mwembamba lakini anauzito mkubwa kumbe alikua na manyama kwene tumbo na chest yalikuja kugundulika badae baada ya tumbo kuanza kuvimba na mtoto kushindwa kupumua.

mzazi ndo mkaguzi wa kwanza wa mtoto, ukigundua kitu si chakawaida wahi hospitali, Aga khan - dar kuna madaktari wazuri sana wa watoto.. kila la kheri
 

Kyenju

JF-Expert Member
Jun 16, 2012
4,561
1,500
Mkuu LUPITA nashukuru kwa ushauri wako, samahani baada ya kusoma maelezo yako nimegundua kuwa kwenye maelezo yangu ya mwanzo nilikosea, alizaliwa na uzito wa kilo 4, ananyonya maziwa ya mama pekee. Nitamtafuta Dokta wa watoto
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom