Mtoto Kula Mchanga!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto Kula Mchanga!!!

Discussion in 'JF Doctor' started by Chuma, Sep 16, 2008.

 1. C

  Chuma JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  wadau au Ma-Dr..wengi kati yetu tuliwahi kula mchanga wakati wa udogo/utoto wetu...na tukapata Minyoo si mchezo...sasa tumekuwa wakubwa tunaanza kuwaona watoto wetu au wa wenzetu wakila mchanga...wakati mwingine ndani kwako Tiles tupu...lkn the way watoto walivyo unashindwa jua...wanavyofanya hadi kuupata....


  Kuna ushauri wowote ule?
   
 2. Bonnie1974

  Bonnie1974 JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2008
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 407
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kula mchanga ni tafsiri ya mtoto kupungukiwa madini fulani mwilini.Jawabu la tatizo ni kuadhere kwenye LISHE BORA YA MTOTO.
   
 3. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,438
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Its true, kula mchanga ni dalili ya mtoto kupungukiwa na madini chuma mwilini ambayo ndiyo chanzo cha Haemoglobin (chembe nyekundu kwenye damu). Jitahidi kumpatia mtoto nafaka (cereals) ambazo hazijakobolewa.
  Tatizo hili mara nyingi huwapata watoto wa kuanzia miezi sita na kuendelea kwani hapa maziwa ya mama pekee hayamtoshi mtoto.
   
 4. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,438
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Sorry, nafaka ambazo zimesagwa moja kwa moja bila kukobolewa.
   
 5. C

  Chuma JF-Expert Member

  #5
  Sep 16, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
 6. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mtoto kula udongo sio jambo la ajabu,ni jambo la kawaida.Isipokuwa inawezekana ana upungufu wa madini fulani mwilini.Unatakiwa kuhakikisha kwamba mtoto wako anapata chakula ambacho ni bora,yaani chakula chenye virutubisho vyote.Kama huna uhakika wa chakula hicho, muona Daktari wa watoto aliye karibu nawe akupe ushauri.Mwisho hakikisha unampa mtoto wako dawa za kutoa minyoo angalau kila baada ya miezi mitatu.Halafu chuma kumbuka udongo na mchanga ni vitu viwili tofauti.Nadhani mtoto wako anakula udongo,sio mchanga!
   
Loading...