Mtoto kuacha kunyonya mapema kunaleta madhara kwa mama? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto kuacha kunyonya mapema kunaleta madhara kwa mama?

Discussion in 'JF Doctor' started by Mkare, Feb 15, 2011.

 1. M

  Mkare JF-Expert Member

  #1
  Feb 15, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari zenu binafsi bana...!
  Wapendwa, nina swali kwa wataalamu wanijuze...! Nimesikia kwa marafiki zangu kuwa mtoto akiacha kunyonya mapema kunaleta madhara kwa mama na hata inaweza kupelekea kupata kansa ya matiti. Sasa mimi mwanangu ameacha kunyonya miezi 3 iliyopita akiwa na miezi 6. Nimepata wasiwasi kuhusu hayo madhara. Je, ni kweli yaweza kudevelop breast cancer? Na Je, ni kweli kuna sindano natakiwa nichome kukausha maziwa yaliyobaki ili yasileta madhara?
  Naombeni majibu tafadhali. Natanguliza shukrani...
   
 2. Visenti

  Visenti JF-Expert Member

  #2
  Feb 15, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 1,031
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 133
  Ingawa hapa kuna wataalamu wazuri, issue yako itatendewa haki kama ukienda kwa kiliniki ya mama na mtoto iliyokaribu yako (MCH/RCH clinic), kule kuna wataalamu waliobobea ktk mambo ya breastfeeding, na utapata wasaa mzuri wa kujadili na hata kufanyiwa some basic examinations.

  Breastfeeding: Natures drink with superior packaging
   
 3. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mkare, Hope ur fine,

  Ninachofahamu mimi ni kwamba utafiti haujaonyesha kama kuacha kunyonyesha maziwa mapema ni risk ya mama kupata kansa ya matiti, kwa hiyo kwa ufahamu wangu mimi huwezi kupata kansa ya matiti kwa sababu hiyo.

  Madhara ya kuacha kunyonyesha mapema yako zaidi kwa mtoto kuliko kwa mama, kumbuka maziwa ya mama ndio chakula bora kuliko vyote kwa mtoto tangu anapozaliwa especially ile miezi sita ya mwanzo, thank God mtoto wako umemnyonyesha kwa miezi sita, lakini sijui kama ilikuwa exclusive breastfeeding au la.

  Kwa upande wa mama madhara ni madogo labda utapata breast congestion itakayokupa pain na discomfort ya kutokatoka maziwa, lakini yanaweza yakawa infected ukapata mastitis, pia kwa sababu umeacha kunyonyesha utakosa ile lactational amenorrhoea ambayo ni natural method ya family planning kwa hiyo unaweza kupata mimba mapema zaidi kama hutumii aina nyingine ya contraceptive.

  Kwa kukata maziwa yasiendelee kutoka tafuta vidonge vya bromocriptine 2.5mg bd for 5/7( siku tano) vitakausha kabisa maziwa yako kwa muda mfupi.

  Kama hakuna kipingamizi kingine ningekushauri uendelee kumnyonyesha mwanao. Watoto wanaonyonya vya kutosha utafiti unaonyesha hata IQ zao zinakuwa juu zaidi.

  Waweza kutembelea clinics za uzazi na malezi kwa msaada zaidi.
   
 4. M

  Mkare JF-Expert Member

  #4
  Feb 17, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru sana Kapotolo kwa useful reply. Yeah ni kweli nilikuwa natamani sana mwanangu anyonye hata mpaka afike 2 years as najua manufaa ya breast feeding. Bahati mbaya alikuja kuacha mwenyewe akawa hataki kabisa nyonyo, ukimpa ni kilio kabisa nikamlazimisha but ilishindikana. Mpaka leo hata nikisema nimuonyeshe ile kwa utani labda kama atanyonya hana time kabisa. Nimetembelea clinic moja Maarufu ya Uzazi wa mpango wamesema haina ulazima sana kumeza dawa au sindano za kukausha. Na vile ameacha kunyonya muda naona hata kutoka (ile ya kuvuja) yameacha, labda mpaka niyakamue sana ndio yanatoka. I hope kama hakuna tatizo la kiafya zaidi naona nisimeze dawa niyaache tu yataisha yenyewe. Thanx again
   
 5. M

  Mkare JF-Expert Member

  #5
  Feb 17, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shukrani Visenti kwa nice suggestion. Nimetembelea huko na nimepata ushauri.
   
 6. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #6
  Feb 17, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kama hayatoki na hakuna congestion u dont need to use medications, thanks for ur appreciation, ur always welcome.
   
Loading...