Somoe
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 754
- 282
Hi, jamani, naombeni msaada wenu wa mawazo. Nina somesha mtoto wa dada angu, shule ya secondary, mama yake alisha fariki na baba ake katiwa ndani, kafungwa kiufupi. Huyu mtoto sasa amenichanga. Jana mama kanipigia sim na kaniambia huyu mtoto anarudi home saa sita za usiku, kila siku sasa. Na anamtukana bibi yake na kugombana nae, hawaelewani. Wiki iliopita kuna kijana alikuja na kisu kwa mama na kumulizia huyu mtoto na kudai anataka kupiga mapanga huyo mtoto akimuona. Out out kaendekeza, masomo anafeli na anamarafiki wasio eleweka, mama kashamshinda. Sasa mie nataka aende kusoma nje ya dar, akienda kijijini labda huko atatulia na atasoma vizuri. Lakini sasa mie sijui shule nzuri huko mikoani, je kuna mtu yeyote ambae atanisaidia kunielekeza shule mzuri jamani, asanteni maana nimechanganyikiwa hata sijui la kufanya.